Saturday, August 20, 2011

"SoMeTHiNG WeNT RoNG SuM WeRe"

Ni halali na kawaida kwa mtu asiyejua kitu fulani kwake kukikosea, hivyo ndivyo ilivyo kwa mtu huyo kushindwa kukieleza kitu hicho kwakuwa ni kigeni kwake kwenye fikra zake, na siku zote unapojitambua kwamba haujui kitu fulani basi unakuwa haujiamini, na mwisho inapelekea wewe kuwa muoga na kuanguka kwakua hauwezi. Kama ni halali kwa mtu asiyejua kukosea, pia kwa mtu asiyejua lugha ngeni ni halalikwake kuikosea kwakua anafikiria kwa lugha yake kisha anaibadili kwa kuitamka kwa kutumia lugha ngeni..yes i wanted to write this article because of this reason..ndio nilitaka kuandika makala hii kwa sababu hii .."something went wrong somewhere" kuna kitu kilikwenda ndivyo isivyo mahali fulani". Kwa kutazama tu hali ilivyo na muonekano wake, kama wewe ni banadamu unayefuatalia nini kinachoendelea basi utakubaliana nami kwamba, kuna jambo lilikwenda ndivo isivyo na kama halikwenda ndivyo isivyo basi, lilipangwa ndivyo isivo na kama halikupangwa ndivyo isivyo basi limeleta matokeo ndivyo isivyo.
Ni wengi wetu bado tuko kwenye mchakato wakutafuta chochote kitu ili tuendane na mdundo wa ngoma tuliyoitengeneza, lakini kwa mfumo tulionao wa this, that, what and where ndio unaofanya wengi wetu washindwe kufika wanapotaka kwenda kwa mfumo ngeni wa fikra kwa lugha ngeni. Kunausemi unaosema "fikra sahihi kwa lugha sahihi zinaunda maana sahihi", hii ni kudhirisha ya kwamba kwakutumia lugha sahihi katika kufikiria na kisha ukatumia lugha sahihi katika kujielezea basi utaeleweka ulichokifikiria baada ya kukisema bila kupoteza maana.
Narudia tena kuna jambo lilifanyika kimakosa, na kama halikufanyika kimakosa basi lilikua sahihi ila limetoa matokeo yenye makosa. Tazama mwanafunzi wa kitanzania amekua kwenye mazingira ya fikra Lugha ya kiswahili ndio Lugha ya Taifa, ila anapokwenda kutafuta Elimu anakutana na Lugha ngeni ndio Lugha ya mawasiliano. Je? atakapokosea katika kujieleza atakua amefanya makosa? lengo sio kutaka kumjua aliyefanya kosa, lengo ni namna gani tutarekebisha kosa lisoloonekana kwani ninayechekwa nikikosea ni mimi wakati mimi sijui kwamba kosa ni langu ama sio langu."Fikra sahihi zinaundwa kwa lugha sahii" sasa nimeunda fikra sahihi ila kwa lugha niliyotumia kujielezea nikawa siko sahihi “Sum sing went rong sum were"
Ukitazama tulipotoka, tulipokuwapo, tulipo na tunapoelekea tupo sawa?, kama hatuko sawa nadhani utakubaliana nami kwamba kuna jambo wakati fulani lilienda ndivyo isivyo. Na kwa hali hii tumejikuta ndani ya matatizo, ingawa matatizo nayo ni sehemu ya walimwengu, ila walimwengu ni walimu na pia ni matatizo, kila penye uzuri mwingi tutegemee pia kupata ubaya mwingi, lakini huu wakwetu umezidi. Kwakua hawatujali nasisi pia hatujali, kwakua hatujali na sisi pia hatujijali, na kwakua hatujijali na wao pia hawatujali. Juzi, Jana, Leo na Kesho imekua kila siku, hakuna tofauti kwakua hatujijali . Hivi tunategemea nini ?,muda unaenda na nguvu zinamalizwa na umri. Kwakua babu alilala, baba nae akalala, sasa  watoto wa baba nao wamelala, je wajukuu wataamka wakati watoto wa baba, baba na babu wao wamelala?.  Tusitegemee miujiza tusipotatua matatazo yetu wenyewe. Tatizo lipo ndani yetu, tatizo ni sisi na tunajiogopa kujitatua. Tunasubiria yule aanze kutatua tatizo, na yule anasubiria wewe uanze kutatua tatizo, mimi na yule pia ni tatizo. Kwanini isiwe mimi na mimi ili tuondoe ubinafsi kisha tulitatue tatizo, nimechoka kuchekwa mimi, hali hii inanipa ari yakutaka kufanya mapinduzi ya kuondoa ubinasi wa mimi na yeye.  Mapinduzi ya ubinafsi ndio yanatakiwa yawe ya kwanza, kisha tupindue uoga ndani ya nafsi, tukishapata ushindi mimi na mimi tulete umoja wa kupigania kilicho haki yetu.
Nakuambia jambo nadhani utaelewa  nilichokimaanisha, “wewe uko na shida yako, kisha nikausaidia shida yako, ukapata shida nyingine, nikakusaidia shida yako, lakini nilipokuuliza tatizo linalosababisha shida zako, wewe hukuniambia tatizo ukaniambia shida yako, badala yakutatua tatizo, ukatatua shida, hivyo tatizo linalosababisha shida zako lipo pale pale na litaendelea kuleta shida kwako”.
Nadhani utakua umelielewa tatizo letu, sasa ili tuachane na shida yatupasa tatue tatizo. Inachukua miaka kujenga ila sekunde kubomoa na tusipotatua tatizo tutazunguka na kurudi tupotoka. Kiukweli hakuna anayetaka kutatua tatizo linalorudisha nyuma maendeleo ya jamii yetu. Ni dhahiri ya kwamba lugha ya kiingereza ina tija katika kurahisisha mawasiliano, lakini mbona tatizo linakua kubwa sana. Embu tazama vipengele hivi kwa umakini na kisha uvichambue kwa fikra zako, kumkichwa haitoi suluhisho ila inakupa nafasi ya kufikiri.
Lengo la Kiswahili kufanywa lugha ya taifa ni kwa ajili ya kutuunganisha na kuondoa ukabila wa kila mtu kutumia lugha yake ya kikabila kama lugha ya mawasiliano, tusingeweza kuelewana kama kila mtu angetumia lugha ya kabila lake, hivyo nawapongeza kwani hawakukosea kukifanya Kiswahili lugha ya taifa.
Kufanywa lugha ya kiingereza kuwa lugha ya pili ni kama kufuata matakwa ya mkoloni wa mwisho aliyetutawala, sidhani  kama mitaala yetu ingekua kwa lugha kiswahili mpaka katika ngazi ya chuo kikuu, nchi yetu ingekua kichwa cha mwendawazimu, kwakua watu wangejifunza kwa lugha sahihi na pia tungekua huru kufikiria kwa fikra sahihi, kama tungekiheshimu kiswahilli nadhani ingekua ni moja kati ya lugha ambazo zingekua ni nguzo imara ya maendeleo ya nchi yetu. Hatuna lugha moja kivipi tutaweza kuwa na maendeleo, tumeikimbilia lugha ya watu sasa hata mitaala imekua ni ya watu. Tazama sasa tumeshindwa kujiendesha sasa tunaendeshwa tu na mkoloni wetu. Nadhani ni kikwazo kikubwa katika kulisongesha gurudumu letu, nasema hivyo kwa kua ni asilimia kubwa sana ya watanzania walioshindwa kujieleza kwa lugha ya kigeni  ingawa vichwani mwao wako na jambo la muhimu sana wanalotaka kulieleza, na pia watanzania wana akili yakutosha ya kuweza kuendelea mbele, ila tatizo la lugha ndio linawarudisha nyuma. Sasa kama lugha ya kigeni inatusaidia mbona tunashindwa kutafsiri mikataba tunayoingia na hao wageni, tunaishia kuibiwa tu kila siku.Kwa Tanzania ya sasa janga la nne kubwa tulionalo ni Lugha, hatujui matumizi ya lugha yakiswahili na pia hatujui matumizi ya lugha ya kiingereza, tumekua majununi funun wa kiswanglish.
Kutumika kwa lugha ya kiingereza katika shule ya msingi/awali  kama somo, kisha kama lugha ya kufundishia katika ngazi ya sekondari sidhani kama hapo kuna malengo ya kumuendeleza mwanafuzi wa kitanzania aliyekulia katika mazingira ya Kiswahili. Wote tunatambua kwamba katika ujenzi imara msingi ndio unatakiwa uwe imara, lakini sisi tunaimarisha juu wakati chini hapako imara. Kama vipi wafanye lugha ya kiingereza ifundishwe kuanzia elimu ya msingi ili fikra za wanafunzi hawa zijengeke kwa fikra sahihi na kwa lugha sahihi, tunawapa sana shida vijana wetu kwa kuwafanya wafikirie kwa lugha hii na kisha wajieleze kwa lugha nyingine, kivipi tutafikia malengo kwa malengo potofu kama haya.
Maono yangu ni kwamba kuna jambo linapelekwa ndivyo isivyo, na kama halipelekwi ndivyo isivyo basi linakwenda ndivyo isivyo, na kama haliendi ndivyo isivyo basi limetoa na litaendelea kutoa matokeo ndivyo isivyo, ninaposema ndivyo isivyo namaanisha haliendi kwa namna tuliyotarajia litakwenda hivyo na pia, halitendeki kwa namna tuliyotarajia litatendeka hivyo pia halileti matokeo tuliyoyatarajia. Sina maana ya kuwakosoa walioamua iwe hivyo ila nawonesha namna tunavyoathiriwa na mfumo huo mliouweka wa this, that, where and what kwa kizazi chetu cha fikra Swahili lugha Inglishi. Na kwakua hatujui vizuri lugha ya Kiswahili sahili hata tunapotafsiri lugha ya kiswalili kwa lugha ya kiingereza tunajikuta ni wenye wa makosa.
Ningependekeza tuchague moja kama ni Kiswahili basi kianzie chini mpaka juu, mbona China, Urusi, Hispania, Italia na nchi nyinginezo duniani zinatumia lugha zao kama lugha ya kufundishia na nchi hizo ziko imara na wako na maendeleo kwakua wanatumia fikra sahihi kwa lugha sahihi. Au tufuate mfumo wa Kenya lugha ya kiingereza kuanzia elimu ya awali, ili tupate wataalamu wenye fikra sahihi watakaoleta maendeleo katika nchi yetu yenye Amani na Upendo kwa wananchi wake. Tuonyeshe upendo kwa fikra sahihi, tuonyeshe upendo kwa lugha sahihi, sio mnatuambia kwa kiingereza nchi yetu ni yaPiece and theft”, halafu mnatutafsiria kwa kiswahili kuwa ni nchi ya “Amani na Usalama” tunashindwa kuelewa mnamaanisha lipi...kumbuka ya kwamba KUMKiCHWA Ni WeWe!
    

"UNSUSPECTED STORY"


She said "It's an awesome story,
get ready to hear it"....BiRD
              
                It all started at the concrete jungle. A bird from the small farm with love, thinking that she will never be in love again, enter the jungle and met a monkey from the bush, a cool monkey, long tail with Rastafarian color, though a monkey gat no dreads.
               These two main characters of my story met at the center of the concrete jungle. At first sight a bird automatically got interested into monkey, and he was this type of monkey who doesn’t speak much or interacts with other fellows in the jungle. A bird tried to get close to him, and she succeeded and they became friends. Without bird notice a monkey liked the bird, well then bird trusted a monkey enough to tell him all about her miserable past life, but a monkey stood up for her by helping her realizing herself and what's worth of her, it was not an easy task for the monkey in counseling her. As things goes they fallen in love, but this time a bird was not sure if she really loves the monkey, because the bird was the apple of somebody's eye. She was in some kind of dilemma. A monkey tried his best but a bird didn’t understand, then monkey decided to step back, that's when bird knew the real meaning of the say "you will never know what you have till it's gone".
               Monkey decided not to see the bird anymore because he thought the bird can’t stand for what she loves. He succeeded somehow, the bird felt sorry for him but she could not go back to him, because she belongs to someone else, and the love she had for him was magnificent ,and the love she had for someone else was declining. So she told the monkey to live her alone, so that she can decide what is best for her, but she offered him friendship. There it came a time where the bird had fallen in love with the monkey, and the monkey without prejudice gave her a chance. Monkey and bird, went well though in life there are ups and downs. 
           Let me tell you about Monkey a little bit. Monkey was ambitious and serious, using his tail to jump and to escape obstacles. A bird knows him but there are some things about him that bird has some difficulties to get used to, though she knows him well. A bird uses her wings than her tail (she wished it were vice versa).
               Now she is into monkey more than she thought, the sad moment was here, the monkey had to leave the concrete jungle. It was like nuclear bomb explosion to her, though she knew the sad moment will come but she was not prepared for it, and she never thought it will happen so soon. Bird hates goodbye's, it makes her felt like it is the end of everything, she didn't get time to say goodbye to a monkey because she had a tight schedule at her nest, but on the other side she thought maybe it’s good not to say goodbye!.But she regrets it now not seeing the monkey for the last time.
               The 1st days after monkey had left the concrete jungle was hard for her to believe he is gone, thus why she decided to write this UNSUSPECTED STORY no one had ever doubted about her in the Center of the Concrete Jungle to easy the painfully inside her and to make herself feel blameless. 
Thanks for listening. It's me  MOoNdayKEY

Sunday, August 14, 2011

"KumRECRUiTeaMembers"

Je? unataka kuwa mmoja kati ya wana Kumkichwa Team?

"WE GiVE YOU CHANCE TO THiNK"

..chaguo ni lako kwakua kumkichwa ni wewe!

"..If we make every attempt to increase our knowledge in order to use it for human good,it will make a difference in us and in our world.."

Sifa za Kumkichwa TeaMember..

1."..uwe mkweli.."
katika kila kitu na mtu.

2."..uwe huru.." kushirikiana na wenzako.

3."..usiwe mbinafsi au mwoga.."
katika utoaji wa mawazo yako.

4."..uwe unajiamini uko na zawadi ndani yako na unaweza kuitumia zawadi yako.."
hakuna kisichowezekana chini ya jua mbele ya muumba.

5."..ujitoe au kujitolea.."
wewe kama wewe kwa kutumia zawadi ulizonazo..

"..if we recognize our talent, use them appropriately, and choose a field that uses those talents, we will rise to the top of our field.."

Faida za kuwa KumkichwaTeaMember...

1.kuendeleza mawazo yetu kama team.

2.kushirikiana kwa kila kitu kama team.

3.kufungua njia kwa walioshindwa kama team.

4.kutambua uwezo wako na kushauriwa ufanye nini kama team.

5.kujifunza na kugundua tusivyovijua kama Team.

Na vingine vingi ni confidential kwa watakao kuwa member tu..

"..If we live by the rule of honesty and accept our problems,we can go far down the road of Achievement.."

NOTE:KAMA WEWE Ni YUDA tutakutosa Mapema,sababu wewe ni kumkichwa..

"..When we act dishonestly, we cheat ourselves, and we cannot hide it for long.."

...mimi pia ni member kwa hiyo mamlaka yako kwenu New Members..masharti kujiunga ni marahisi tu..

Tuambie ukiwa kumkichwa TeaMember utafanya nini kwa ajili ya Kumkichwa..

Jipime uwezo wako kisha UJielezee kwa maneno machache tu..

"..YOU ARE WHAT YOU THiNK.."

Tuma kwa Email yetu..
kumkichwa@gmail.com

"..To be of use in the wolrd is the only way to happiness.."

hii ni nafasi ya pekee kwako..kama uko tayari kuwa mmoja kati ya kumkichwa Team,Jiangalie wewe na nafsi yako..kumbuka kuwa kumkichwa ni wewe..BLESS i

Tuesday, August 9, 2011

"SAFARi YA MiAKA MiTATU"


Ilipoanza ni kama safari ndefu isiyo na matumaini ya mimi kufikia mwisho wake, kwakua mengi niliyoyasikia kuhusu safari hii na changamoto zake nje ya uwanja/mfumo zilinipa wakati mgumu katika kujifikiria ya kwamba,ni kwa namna gani nitaweza kufika mwisho wa safari hii. Safari hii ni ya muda unaojulikana ingawa kuna ambao walikata tamaa tulipoianza, kuna  waliochishwa njiani mwasafari kwa sababu tofauti tofauti na kuna walioshindwa kabisa kuendelea na safari hii ingawa walishaianza. Elewa ya kwamba kusafiri kwake ni safari ya maisha, ila kwa mafunzo yake kwa miaka ilikua ni mitatu tu.

Mwanzo wa jambo huwa ni mgumu siku zote, kwakua mtu huhitaji muda wakukaa ,kujifunza, kutambua kisha kujiweka sawa, na kwa mazingira ya safari hii ilinibidi kuyajua kwanza ili niweze kuendana nayo kiuhalisia kwa kuyabadili au kwa kujibadili kama kinyonga. Mwanzo wa Safari yangu ulianza kwa ugumu, kwani ilihitajika mimi kuyafanya mazingira yaweze kuendana nami ama mimi niendane na mazingira hayo ya safari. Kwakua nilithamini umuhimu wangu na kutaka kuwa mimi na sio kinyonga, niliamua kuyafanya mazingira yaendane na mimi na sio mimi niendane na mazingira ya safari  kwani ipo nafasi ya mimi kupoteza uhalisia wangu kwa kuyafuata mazingira ya safari hii. Hapa pia  ndipo nilipotambua umuhimu wa mimi kuwa mimi na sio mimi kuwa kama kinyonga kujibadili kuendana na mazingira yasiyoniridhisha eti nami nionekane ni mmoja kati ya wao. 

Mbinu nilizozitumia zilitokana na kukubali uhalisia wa maisha niliyoishi na namna nilivyokuzwa kwa mazingira yangu, kutambua kwangu umuhimu wangu katika jamii yangu, na kukumbuka kwangu wapi nilipotoka, na kutazama kwangu wapi ninataka kufika ni mojawapo ya mbinu zilizonisaidia kufika hapa nilipo. Katika safari hii ilinibidi kuongeza upeo kwa kuchanganua na kuchunguza ni mambo gani ninaweza kuyachukua kama yalivyo, kuyaacha kama yalivyo ama kuyabalili yalivyo ili yaendane na mimi. Kipindi hiki cha mwanzo kilikua kipindi kigumu sana wakati wa safari hii, kwani ilifika wakati ilinipelekea kutoka katika mstari wa safari hii, ila kwakua nilipata muda wa kutambua nilipokosea, nilifanya mabadiliko ya haraka na kurudi katika mstari wa safari hii.

Katikati mwa safari hii kulikua ni wakati wa kufanya marekebisho na muendelezo wa mbinu za mwanzo kwa kufanya kwa vitendo vyote nilivyovidhania kwamba ni muhimu kuvifanya ili kuifanya safari yangu iwe na umuhimu zaidi ya kusafiri, nilijifunza vingi kuliko nilivyofundishwa, nilijifunza kuona vilivyofichwa kwa kutumia akili ili wanaotumia macho na masikio wasivielewe. Nilijifunza kujiandaa kabla na kukubali matokeo baada, kuthamini ulichanacho, ulivyo na matakwa yako. Kuacha kisicho, kukwepa visivyo na kung'ang'ania kilicho. Kipindi ambacho umuhimu wa safari ulianza kuonekana kwa vitendo, na watu walitambua uwepo wangu kama mmoja kati ya wasafiri kamili wanaotambua wapi wanapoenda. Ingawa vikwazo na binadamu wake hawakucheza mbali katika kunirudisha nyuma, muumba aliye juu aliniepusha na majaribu yao kwani istiqaama niliyonayo ili imarika kadiri walivyonijaribu kwa mbinu zao. Nilithibistisha ya kwamba hakuna tatizo lisilo na suluhisho, kwani kwa kipindi hicho nilimuomba  muumba anijaalie uvumilivu, usikivu na utulivu kwa matumaini ya kula mbivu.

Mwishoni mwa safari hii ndipo makumbwa mengi yenye tija yalipoibuka kwani hata lisilowezekana ilithibitika kwamba linawezekana  kama utatumia muda wako na fikra zako kwa wakati maalumu na kwa sababu maalumu. Nilikua nikiamini ya kwamba kila mtu amezawadiwa zawadi yake na maulana na kwa kipindi hiki nilikua nikitamani kuijua zawadi yangu toka kwa maulana, na ndipo  kipindi hiki nilipo igundua zawadi hiyo na kuanza kuitumia. Katika safari hii kwa ujumla nilijifunza mengi hasa urafiki wa marafiki na unafiki wa marafiki, katika maisha haya ya sasa sio kila  anayekupenda kweli anakupenda na pia sio kila anayekuchukia kweli anakuchukia, kila mmoja yuko katika maisha yako ili atimize sehemu ya maisha yake, yaani kujaza kitabu chake kwa uwepo wako.

Kiukweli  hakuna anayeaminika ila cha muhimu ni  kujiamini wewe mwenyewe na kama ukimuamini mtu usimuamini shetani aliye ndani yake. Binadamu huwa tunabadilika na pia huwa tunabadilishwa, kuna wanaomaua kubadilika kwa matakwa yao  na wanaobadilishwa kwa matakwa ya kinacho wabadilisha, mtazame uliyenae na uliokua nao sio wote wako kama zamani na sio wote watabaki kama zamani. Ndio maana tunasema akili kumkichwa  ni kwa kichwa yako wewe, usipokua makini na ulimwengu na walimwengu wake  utabaki unatupia dua lako la kuku kwao  mwewe. Wewe cheza nafasi yako na sio uchezee nafasi yako, amini usiamani ukiwa nje ya uwanja/mfumo hakuna atakayekujali/atakayekuthamini. Wakati ndio huu amka wewe uliyelala….Kumbuka kumkichwa ni wewe!