Thursday, May 31, 2012

AMKA,ELIMISHA,IMARISHA,OKOA,UNGANISHA..(a,e,i,o,u)

a,e,i,o,u

-Je unataka kujua namna kutengeneza blog,fb page,group?
-Je una makala au maandiko kukuhusu wewe, maisha yako, biashara au fani yako ungependa yachapishwe katika blog yetu ya jamii?
-Je unataka kutangaza biashara yako nasi?
je una hadithi/story kali au una kipaji unataka dunia ikifahamu?
-Una kitu cha muhimu ulichokifanya/alichokifanya mtu ungependa jamii itambue mchango wako au wake?
-hata kama ni link wewe tutumie tutaunganisha..


-usisite wala usiogope kuhusu gharama,Ni BUREE, tunarudia tena tutaifikisha kwa jamii yako BUREE..


Tutumie kupitia email ya kumkichwa@gmail.com tutawasilisha kwa hadhira wako..tuma wala usihofu..uamuzi ni wako iwe ni nyimbo, picha, makala, hadithi, video au tukio/event yoyote ile, ama kitu chochote kitakachoifanya jamii yako iamke, ijifunze, ijiimarishe, ijiokoe na kujiunganisha..kumbuka kumkichwa ni wewe!
..Vigezo na masharti kuzingatiwa.. 
Tembelea link hii kwa maelezo zaidi.. www.kumkichwa.blogspot.com

Site Under Construction....Please Come Back later...................


Wednesday, May 30, 2012

S.U.A Episode 2 @ Kijenge Juu Arusha,Tanzania

It’s a free stage or platform to the youth who are uprising to become artists, S.U.A is a short form of Saving Underground Artists
Visit our Facebook Page S.U.A

Kijenge Juu Stand Up

Nyomii ilipoanza kutimba

kila raia anatafuta pozi lake
Daz Naledge na Dj Gekko
DJ Gekko

JCB akifungua S.U.A Episode 2

Biggie akifanya short listing ya Artists

Raia wa rika zote walikuwepo

People walikua wakutosha...wakishow LOOOVE

That's whatsap...Kjuuuu stand up...

Battle zikaanza ka hivi
AKACHABA na SiGHT Mo

Black Nakoz
Mystic Vibes

hakunaga supra

Underground Rapperz

Lovely Ladies
Battle inaendelea

Nyomiiiiiiiiiiiiiiiii

Back benchers

Back Stage
Freestyle Battle
Akachaba...Kibaooooooooooooo
                                                    Tanzanias Got Talent

Akachaba-Kibao ft. Wiseman(Prod. Daz Naledge)

Akachaba performing his new song Kibao at Kijenge Juu- Arusha,Tanzania

Thursday, May 17, 2012

"KOMBOLELA"

I can be President...Yes! you can baby brother..Kwa sala naanza kuhesabu, moja mpaka hamsini,
tucheze kwa adabu, huku tunajiamini,
mchezo huu wa mababu, sijaoteshwa na majini,
ninaposema kombolela, kumkichwa ni wewe!.


Tumeganga kumtafuta mchawi, tukasahau vya akilini,
uchumi wa jirani unastawi, sisi upendo na amani,
baada ya kutoa matawi, mti tukaubwaga chini,
ninaposema kombolela, kumkichwa ni wewe!.


Aliyestaafu kala jana, leo twamfatilia nini,
tutaishia kumtukana, ana hisa mgodini, 
kama ukweli na uwazi havikufana, sasa maisha bora ya nini,
ninaposema kombolela, kumkichwa ni wewe!.


Nchi yetu masikini, umekua wimbo jukwaani,
sera za jembe la mpini, zinamzeesha babu shambani,
kwanza kilimo redioni, fuko la pipi bungeni,
ninaposema kombolela, kumkichwa ni wewe!.


Kama za mwizi arobaini, mbona kafikisha hamsini,
tokea miaka ya sitini, vifaranga tutanyonya lini,
kwa zetu fikra masikini, wametugeuza majinuni,
ninaposema kombolela, kumkichwa ni wewe!.


Tukikubali kua waamuzi, tusikatae pia lawama,
tusisahau ule uchaguzi, kwenye mstari tulisimama,
sasa nani mwamuzi, aliyechaguliwa au aliyesimama,
ninaposema kombolela, kumkichwa ni wewe!.


Ninaposema kombolela, naomba unielewe,
umwamshe aliyelala, mwambie KUMKiCHWA ni wewe,
kwakua tuliaanza kwa sala, mwenye niambaya asinielewe,
nitakaposema tena kombolela,wa kujikomboa ni WEWE.


Kajiabeid(c)kumkichwa2011

by Abeid Kajia on Saturday, April 23, 2011 at 5:38pm ·


"JE Ni WAPi TULiKOSEA?"

Je! ni wapi tulikosea?

Tulisali dhambi zilipozidi, ukame ukapotea,
baraka za mvua zilipozidi, mafuriko yakatokea,
maisha yakapotea, Je! ni wapi tulikosea?

Tukajenga kwenye miinuko, wakasema tumekosea,

kila mahali tulipo, alama ya x imekolea,
maisha yanapotea, Je! ni wapi tulikosea?

Pazuri ndio kwao,
kicheko kirefu wameotea,
kwetu mabondeni vilio, jamani huku tunaelea,
maisha yanapotea, Je! wapi tumekosea?

Utawasikia hameni mabondeni, kukaa huko mnakosea,

Mara unasikia kaposho haka kadogo jamani, sio vibaya tukikaongezea,
maisha yakapotea, Je! ni wapi tulikosea?

Nakosea bure bila senti, natupwa Jela nikafundishwe,

wamekwapua fuko la vijisent, wanaunda Tume wasafishwe,
maisha yakapotea, Je! ni wapi tumekosea?

Japo hasira zetu ni kali, misaada yenu tutaipokea,

nyie mpini sie makali, sauti ya vuta ikitokea,
maisha yatapotea, Je! ni wapi tutakosea?

Bora maisha niyaonayo, kuliko
maisha bora ya ndoto
Za mjomba kama Mpoto, za kudanganywa kama toto,
ninaposema tena kumkichwa ni wewe! Je! utasema nimekosea?


by Abeid Kajia on Thursday, December 29, 2011 at 9:11am ·

"MTO HUU WENYE MAMBA"

Baada ya kuvuka mto wenye mamba

Mto huu una mamba wengi,

walio na madhara mengi,

wenye kutaka vingi,

vyenye gharama nyingi,

kivipi utafika ng'ambo?

 

Ng'ambo ya mto vizuri vingi,

vyenye manufaa mengi,

kupata vizuri ni kujitolea vingi,

kwa umoja huu wa kutafuta wingi,

kivipi utafika ngambo? 

 

Silaha uliyonayo kigingi,

maswala unayoyafanya ya msingi,

malengo uliyonayo mengi,

mamba wanaokutamani wengi,

kivipi utafika ngambo?

 

Daraja upitalo ni la kamba,

sio lipana ni nilembamba,

upitapo usiwe unajigamba,

ukiiga unapasuka msamba,

kivipi utafika ng'ambo?

 

Waliovuka walishasema,

vyema ukifanya yaliyokutuma,

usijaribu kufanya kwa kupima,

ukichanganya malengo na mtima.

Kivipi utafika ng'ambo?

 

Wakasema usajaribu ndumba,

kuuvuka kudra za muumba,

wala usichoke kumuomba,

Ndiye atakayekuvusha viumba, 

Vya Mto huu wenye mamba.

 

Kajiabeid(c)2011

by Abeid Kajia on Friday, February 4, 2011 at 3:07pm ·


Monday, May 14, 2012

At last THE KUMKiCHWA AGE...

                                    

WELCOME TO OUR NEW GENERATION, THE AGE OF KUMKICHWA...FOLLOW THE LINK BELOW TO VIEW THE PRESENTATION...Don't forget to comment either by using your yahoo, google, facebook or anonymous account..kumichwa ni wewe

https://skydrive.live.com/fullscreen?cid=b81df4a68a719b77&sc=documents&resid=B81DF4A68A719B77!140&filename=The%20Kumkichwa%20Age..pptx&wx=p&wv=s&wc=officeapps.live.com&wy=y