Tuesday, July 31, 2012

Watch Live Tarawih Prayer Stream From Makkah In This Ramadan Kareem




kama hautopenda kuitazamia ukiwa Kumkichwa fuata link hapo chini.......... if you will find it difficult to watch it through Kumkichwa then follow the link below...
http://www.youtube.com/user/MakkahLive?v=cMgnsrJXTOc

Fahamu Hatua Sita (6) za Kutengeneza Blogu/Blog kutumia BLOGGER


Blog
         Blogu ni teknolojia mpya inayowezesha watu binafsi kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao wa tarakilishi. Blogu inaweza kuchukuliwa kama ni shajara pepe. Neno "blogu" ni tafsiri ya Kiswahili inayotokana na neno la kiingereza, "blog." Neno "blog" limetokana na neno jingine, "weblog." Kimsingi, blogu ni aina ya tovuti ambayo huandikwa mara kwa mara na kwa mpangilio wa mambo mapya kutokea ukurasa wa mbele kuendana na tarehe na mwezi.

         Zipo blogu za aina mbalimbali. Kwa mfano, blogu za maandishi, blogu za mkononi, blogu za picha, blogu za sauti, na blogu za video.

         Blogu ya mradi wa Global Voices inaandika muhtasari wa majadiliano na habari zinazojitokeza katika blogu mbalimbali duniani, hasa nje ya Marekani. Mradi huu una wanablogu katika nchi mbalimbali duniani ambao wanaandika juu ya masuala muhimu yanayojitokeza katika blogu za nchini mwao au katika bara lao...soma zaidi kutoka wikipedia kuhusu Blog kwa kiswahili http://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu

kwa kiingereza Read more about Blog in English through Wikipedia http://en.wikipedia.org/wiki/Blog


     Zifuatazo ni hatua sita za namna ya kutengeneza Blogu..kutengeneza na kumiliki blogu ni bure...ukitaka kujua faida zake usikose kusoma makala ya Faida na Hasara za blog:


1.Ingia kwenye Google Search
  
 2. Search Blogger kisha chagua Create your Free Blog au Create blog

3. Ingia (Sign In) kwa kutumia Gmail Account Yako na Password yako..hizi ndio zitakua utambulisho wako kwa blog yako.
 

 
4. Chagua Create a Blog 


5. a. Andika Jina la Blog kwa Herufi KUBWA 
    b. Jina Blog Address kwa Herufi ndogo.
    c & d. Kisha Bonyeza Check Availability ikionesha Sorry, this blog is not available basi jaribu jina lingine mpak ioneshe kijani yaani This blog address is available. 

  e.Jaza hayo maneno hapo ili kiunesha kua sio robot bali ni mtu
  f.The bonyeza continue hapo chini kulia kisha kuendelea

 

6. Baada ya hapo utakua tayari umeshatengeneza Blog yako…unaweza kubonyeza New Post ili kuweka habari au picha, au ukabonyeza View Blog ili kujua muonekano wa blog yako.

huu ndio muonekano wa kwanza wa blog baada ya kuitengeneza


Mpaka hapo nadhani utakua umeshafahamu namna ya kutengeneza blog kwa kutumia Blogger...kwa maoni, maswali au ushauri tuandikie hapo chini kwenye sehemu ya maoni....Ahsante Sana Kumkichwa

Call For Interview 4260 (Kuitwa Kwenye Usaili Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma)

Nafasi za Kazi Wizara YA Fedha

Nafasi za Kazi kwa vijana wa Tanzania

Ondoa Facebook Timeline kwa Profile yako

Facebook Timeline

              Timeline ni mtindo mpya wa muonekano wa kurasa ya mtumiaji wa facebook, ambayo huonesha vitu muhimu kama picha ama tukio jipya ambalo huonekana kwa mfumo wa hadithi ya mtu. Mtindo huu mpya ulianza kuonekana mwaka 2011..ambapo kwa wale waliokua mfumo wa zamani walitakiwa kuutazama(preview)mfumo huo mpya kisha kama utawavutia basi mtu huyo hukubaliana nao na kuanza matumizi yake..
 

Faida za Timeline..
Ni kwamba unaweza uka ongeza habari au ukaificha kabla mtu yoyote hajaiona.
Kugundua vitu na kuchangia(share) na wenzako
Kukusanya matukio yako muhimu kwa pamoja
Kusikiliza mziki kwa facebook
n.k
                             

             Tatizo lililo jitokeza ni kwamba mtindo huu umewachosha watu wengi sana, na wengi wao wanataka kuondokana nao..lakini kwa namna ilivyowekwa ni kwamba hauwezi kuondokana na mtindo huo..ila unaweza ukaondokana nao kwenye Browser yako peke yako..ila kwa wale watakaotembelea ukuta(WALL) yako watakuta Timeline kama zamani.

            Hivyo ningependa kuwashauri ambao tayari wameshaingia kwenye mtindo huu basi wauvumilie tu…kwakua kuna baadhi ya mitandao inayotoa taarifa kua unaweza kuondokana na Timeline, kisha wanakupa link ya kuifata..link hizo zinaweza kua virusi(virus)..hivyo ningewashauri na wale ambao bado hawajaingia kwa Timeline..wasiingie huku kama watataka kutoka…huu ndio ujanja wa mitandao ya kijamii…ukishaingia ni ngumu kutoka.
 

             Tafadhali Changia makala hii na marafiki zako wanaousumbiliwa na Timeline, Pia usisahau kutoa maoni yako na ushauri, kama una maswali hii ndio sehemu ya kuuliza…kumbuka Kumkichwa ni wewe!

Friday, July 27, 2012

Ukweli uko wapi?


              Ni miaka kumi tayari imeshapita toka nihitimu elimu ya msingi, na kwa kipindi hicho fikra zangu na za utoto wa rika langu huwa tunamini na kufuata kila tunachokisikia na kuambiwa, ila baada ya miaka hiyo kwa sasa sina tena uwezo ule, kwani maswali mengi yamekua yakiibuka kwa nia na shauku ya kutaka kujua undani wa baadhi ya vitu kama sio kila kitu. Na swali moja wapo ni "Je ukweli uko wapi?"

             Nakumbuka wakati huo wa udogo Wazazi wetu walituambia mimi na pacha wangu "Mkishindwa kufaulu kwenda kidato cha kwanza basi mjue mtakua waendesha mikokoteni”, Mzee akatuahidi kua atatupa matairi ya gari lake ya nyuma na mbele, kila mmoja mawili mimi na pacha wangu na Mama naye atatupa mbao ili tutengeneze mikokoteni kwakua tulikua hatupendi kujihusisha na elimu au tulikua hatutilii mkazo elimu kama namna tulivyokua tumewekeza muda kwenye michezo. Tuliamini kua ni kweli wangetuacha tuwe wasukuma mikokoteni na walikua wanatuadhibu kama wakitukuta hatujasoma na tumeenda kucheza mpira. Bakora zile kwa upande wangu sikuzipenda kabisa kwa wakati ule, niliona kama naonewa ila kwa sasa kwa fikra hizi ndipo natambua umuhimu wake. Ukweli ni kwamba bakora zile zilikua ni za kutujenga na sio uonevu kama nilivyodhania mwanzoni.

             Sasa nimekua kifikra na kiakili, maarifa yameongezeka kiupeo, na uchambuzi wa mambo umekua mkubwa. Kutokana na maisha yalivyo nikajikuta najiuliza “Je Ukweli uko wapi?”

             Kwa ninavyofahamu Muda ni kitu muhimu sana, ambacho ukiwekeza kwa umakini basi faida yake itakua nzuri sana. Sasa kama ukweli ndio huu Je! ni kweli muda wetu tunauwekeza kwa umakini ili kupata faida ama tunategemea hasara?

             Wanasema vijana ni taifa la kesho na taifa la kesho linajengwa leo, ikimaanisha muda wa vijana wa leo umewekezwa katika kulijenga taifa la kesho lililo bora kwa kuwa hakuna anayewekeza penye hasara. Sasa ukweli upo wapi, Je! kwa hali halisi ya mambo yanavyokwenda, ni kweli vijana tumewekeza/zwa kwa ajili ya kesho ama tunatumiwa leo ili waijenge kesho yao?. Anza na wewe, jitazame wewe mwenyewe, kisha tazama kwenye mtaa wako, chambua hatua kwa hatua mpaka ufikie Vijana wa taifa zima. Kama ndio tumewekeza/zwa kwa faida yetu, huenda basi tukafaidi taifa letu la kesho, ila kama sio jiulize ukweli uko wapi?

             Tazama vijana kwenye biashara ya siasa, wanajaribu kuwekeza pasipo kujua kuwa wao ndio rasilimali ya mwanasiasa. Wanahangaika kutafuta mgodi wakati wao ndio madini.

             Chanzo ni nini? UTEGEMEZI. Tumaini la vijana lipo kwa mtu/mwanasiasa, shida za vijana ni mtaji wake, ambaye atautumia muda wao kuwakusanya ili awapumbaze kwa ahadi za mabomba ya Asali na Maziwa. Vijana hawa wataishia kupukutika na kuwa vilema kwa tip za toyo na vibajaji. Hivi hamjajua kua matatizo yetu ndio mitaji kwao. Unataka tiba, elimu, mtaji, ajira ila hautovipata bure. Unadhani watakuchapa bakora? unadhani watakutisha kua utasukuma mkokoteni? Laah.. bali watakuahidi vizuri ili ubweteke na uwe tegemezi kwao. Wakirudi wakukute pale pale na shida nyingine nyingi. Kijana amka, utawategemea mpaka lini, jaribu kusimama na miguu yako miwili, ila kabla ya hapo jiulize UKWELI UKO WAPI?.. Kumkichwa ni wewe!

Tuesday, July 24, 2012

HUU NI MFANO MZURI WA KUIGWA NA VIJANA












              Tungependa kuwapongeza vijana hawa waliotembelea Makao YA Kulelea Watoto Yatima, kituo cha CHAKUWAMA, Ester Lily Wazza'red, Rama Ruginair, Jointy Johnson Jay kwa kufanya kitendo cha kijasiri na chakujitolea ambacho kwa rika letu kuwaona vijana wanafanya kitendo kama hiki basi ujue kweli wameguswa na matatizo ya jamii yao. Tungependa pia kuwaasa vijana wenzetu ya kuwa Jamii inatutegemea sisi..Tuwakumbuke kila wakati..Tukumbuke kwamba sio kwamba wao wasionacho wamekosa au wamenyimwa ila huenda RIZIKI YAO imepitia kwenye mikono yako wewe..usiikwamishe.. bali wafikishie riziki hiyo na M/Mungu atakuongezea..Kumbuka "MKONO WA KUTOA NI BORA KULIKO MKONO WA KUPOKEA"..

New Song_Hard_STREET TAPE_ Prod. Daz Naledge


               

                 Dab Muzik Entertainment na watengwa recs Wanakuletea Street-Tape iliotengenezwa na  Daz Naledge Kwenye studio za Watengwa ‘Imeitwa Street-Tape kwa sababu imetengenezwa bila kuwa na dj wa kuchanganya nyimbo hizi katika mfumo wa mixtape’ amesema Daz…Wakati tape hii inaingia mtaani Naledge amemtumia Deejay Ph wa ufaransa mzigo mzima, kwa ushirikiano wa huyu jamaa pamoja  watatengeneza MIXTAPE ambayo itauzwa world-wide kuanzia mwezi wa kumi mwaka huu. Street-Tape hii inapatikana kwa TShs.3000/=. Nyimbo hii iko kwenye Street-Tape hii na kuanzia sasa imeachiliwa rasmi kama promo ya mzigo mzima….Kwa wale ambao wako nje ya Arusha Mcheki Daz kwenye Facebook Page yake ya Daz Naledge ama kwa namba 0719 300 204 Jipatie nakala yako sasa. 

Friday, July 20, 2012

Vijana na Ujana-Mwisho/Vibaya na vibaya sana (Nimejaribu nimeshindwa kutoka)



             Kundi hili ni la wale vijana wanaopenda kujaribu vitu venye kuhatarisha, kundi lililo karibu na maji ya moto na lililo makini kwani linajitambua kua maji haya ni ya moto na yanaweza kuwaunguza wakati wowote, kundi hili liko bora ila sio sana na hapenda kuutumia Ujana wao kwa mambo kwa kujaribu ili kujua kipi chenye kufaa na kipi kisichofaa kwa manufaa ya baadae ya maisha yao, lakini kundi hili hujaribu kisha hushindwa kuacha walichojaribu ingawa kinahatarisha.

Kundi hili huendesha maisha yao vile nafsi zao zinataka.

Kundi hili halina fikra za mara mbili pale wanapotaka kufurahia maisha yao.

Kundi hili pia ni wazuri kwa kujitetea kwamba wanachofanya kina faida maishani mwao kwakua hisia na fikra zao huwa zimeshatekwa na kitu hicho.

Kundi hili pia huona fahari kufanya wanachikafanya kwakua wanakua wao na hawana haja ya kujificha kua hawafanyi. Ni moja kati ya kitu kizuri kwa kundi hili ni wakweli mbele ya nafsi zao.

Kundi hili hukubaliana na hali halisi ya kua nafsi zao zimeshindwa kushindana na matakwa ya nafsi.

 Changamoyo wanazokutana nazo:-
“Stay Away from him/her””kaa mbali nae”Moja ya changamoto ni kutengwa na wale wanaowapenda kutokana na msimamo wa kundi hili kushikilia wanachokifanya kua ndio bora kwao kwa wakati huo.

“Bird of the same feather””ndege wafananao”Kujichanganya kwao na watu ni kwa mashaka kwani huwa wanahisia kila mtu anawazungumzia wao. Huwa ni wagumu kuamini mtu labda wapate mtu aliye katika kundi lao ili waruke pamoja.

“Have change””nimebadilika”kundi hili hata kama likifanikiwa kubadilika hupata wakati mgumu sana kukubalika tena na wana jamii kwamba ni watu wa kawaida kama wengine. Hujikuta wanarudi tena walipotoka kutokana na kauli rejeo za jamii kwamba wanazuga au wanajidai wamebadilika. Ila kiukweli huwa wanabadilika.

Ushauri wangu kuhusu kundi hili
Hakuna kinachoshindikana chini ya jua, ingawa ni furaha na ni raha kufurahia maisha tofauti na wengine ila umakini katika kitu unachokifanya ni muhimu kwani kama hautajiumiza wewe mwenyewe basi ujue utawaumiza wale walio karibu na wewe.

Ndio ni halali yako kufanya unachopenda ila je tumeumbwa ili tuwe wabinafsi?. La hasha ni fikra zetu na nafsi ndizo zinatufaya tuwe hivyo..na pia ni rahisi kwa wao kutuelewa ila ni vigumu kwa wao kutufanya sisi tuwe wabora.

Kitu cha kuzingatia ni kutochanganya malengo yetu na hatari tunazotaka kuzijaribu. Hatari nyingine zinavutia kweli na zinatufanya tufurahie pale tunapozifanya ila kwa ndai nafsi inajaribu kupingana na hali hiyo kua “unajua unachokifanya sio sawa kwako ila hauna nafasi ya kuacha kukifanya kwa wakati kuo  kwakua nia kinaleta faraja, matumaini na furaha kwa wakati huo ila baada ya hapo ni maji ya moto”.


            Kwa ujumla maisha yana changamoto nyingi sana, na kwa vijana ni mara mbili ya changamoto hizo. Ukishafikisha umri wa kuanza kujitegemea kwa kijana kichwa huwa kiko katika hali ya mabadiliko transicion ambapo majukumu yanapokuwa juu yako na wewe unalazimika kukubaliana na majukumu hayo , na ndipo kijana hufikiria ni bora apate kitu cha kumpunguzia msongamano wa mawzo ili apate kutazama na kuchanganua nini kinakuja mbele yake. Hivyo kauli moja ya vijana ni “life Is short banaa lets us have fun”…je unajua ni majuku gani hayo? Je unajua umri wako na unachotakiwa ukifanye? Je unatambua kua umeshapiga hatua kadhaa kutoka pale ukipo na je unaelekea wapi na je umetazama hatua zako? Usikose sehemu ya pili ya makala hii ya “Vijana ja Ujana” ya "Tambua umri wako na majukumu muhimu kwako"…unataka uje uwe nani? na umejiaandaaje?usikose mfululizo huu wa a,e,i,o,u..amka,elimisha,imarisha,okoa na unganisha…kumbuka KUMKICHWA NI WEWE.

Monday, July 16, 2012

Amazing Photos

CREATIVE ART
TWIN TOWERS
THE CITY ON TOP
PORT OF DAR ES SALAAM
THE KUMKiCHWA

Tuesday, July 10, 2012

Jogoo Kichaa-Ordinally(Grandmaster)

                                 

"ViJANA NA UJANA"-Sehemu ya pili (Vizuri na Vibaya)


Amka, Elimika, Imarisha, Okoa, Unganisha

II.    Vizuri na vibaya (Najaribu/Jaribu kisha nitaacha- ingia kisha toka)
 
                  Kundi hili ni la wale vijana wanaopenda kujaribu vitu vyenye kuhatarisha, kundi lililo karibu na maji ya moto na lililo makini kwani linajitambua kua maji haya ni ya moto na yanaweza kuwaunguza wakati wowote, kundi hili liko karibu sana na bora wakati wakutaka toba na hapenda kuutumia Ujana wao kwa mambo ya kujaribu ili kujua kipi chenye kufaa na kipi kisichofaa kwa manufaa ya baadae ya maisha yao.

Hufikiria kua kama wakikosea wataomba tu msamaha, kwakua wanajua watasamehewa.

Kundi hili katika makundi ya vijana huwa linaonekana bora kwakua kundi la juu la wasiojaribu huwa halionekani kabisa kwani huwa wanajificha au ni wachache.

Pia halionekani kwani katika kundi hili kuna makundi tofauti kutokana na aina ya kitu kijana alichoamua kukijaribu. Kuna makundi ndani ya makundi, kuna waliojaribu hiki na wasiotaka kujaribu kile, kuna waliojaribu kile na wasiotaka kujaribu hiki. Huwa ni kundi la kufundishana, kuonyana, kushawishiana na kutahadharishana kuwa acha hiki jaribu kile acha kile jaribu hiki

mfano: “rafiki yangu uongo sio mzuri, acha uongo” na rafiki yake atamwambia “rafiki yangu acha wizi, wizi sio mzuri”. Wote wako katika hatari ila hatari zinazotifautiana. Na wengine wataonyana kwa kushawishiana “kuliko uibe bora udanganye” huku mwenzake atamwabia “kuliko udanganye bora uibe”.kumkichwa ni wewe!

Kundi hili ni la wale waliojaribu kisha wakaacha walichokifanya kwa kuona hatari zake. Kundi hili huwa linawafunza wenye kutaka kujaribu kua sio vizuri kuingia humu, wengi wa vijana walio katika kundi hili hujikuta wameshikilia kitu kimoja kama ndio kinachowasaidia katika kufanya mambo yao yaende sawa, namaanisha pasipo kurudia tena anachokifanya hataweza kuendelea, ila ni kundi ambalo hufika mahali na kusema basi nimechoka kua mtumwa wakudanganya, nimechoka kudhulumu, nimechoka na wizi, nimechoka na kuwaumiza marafiki zangu.

 Changamoyo wanazokutana nazo:-
“wakati ni ukuta” baadhi ya watu kundi hili hukutana na changamoto ya muda kwani hujikuta wanajaribua wakati muda wao wakujaribu umeshapita. Hujikuta bado wanaendelea kuchezea matope ukubwani.

“I was young and foolish” “nilikua mdogo na mjinga” Baadhi yao hujikuta ni wenye kukosea na huishia kujilaumu kwanini walifanya na kujaribu pasipokuangalia ni yapi matokeo ya wanachotaka kujaribu/kujifanya. Huwa wanahatarisha maisha yao kipindi hiki cha maji ya moto na pale yanapopoa huishia kusema nilikua mdogo na mjinga, sikujua hatari iliyokua mbele yangu, kwakua nilifurahia nilichokua nakifanya.

“Follow your heart” “fuata moyo wako” kundi hili hupenda kufuata moyo unavyotaka, moyo huu kwa makala hii ni “nafsi”, nikimaanisha kufuta nafsi yako vile inataka hata kama ni kitu kitakacho hatarisha maisha yako. Eti kwakua nafsi imetaka uweke kidole kwenye moto wewe weka tu kwakua unafanya vile nafsi yako inataka.

“Have fun life is short” “furahi maisha ni mafupi” kundi hili pia hujikita katika wakati mgumu kwakushindwa kwao kuelewa baadhi ya maneno yanamaanisha nini. Inaposemwa kua furahia maisha haimanishi hatarisha maisha eti kwakua ni mafupi. Kundi hili huishia kujaribu kila kitu, na mwishowe pale wanapo poa wanakosa cha kufanya kwakua wameshafanya kila kitu, kinachofuata ni ugomvi na mwenzako, kwakua mlifanya kabla ya wakati.

“Mbona nani hii alifanya/anafanya” kuna hii kauli ya kujitetea kua mbona Yule anafanya na hajapata madhara yoyote, mbona Yule alijaribu na hajaumia?. Kundi la kutazama nani kafanya nini na mimi nifanye nini, lakini bila kujua kwanini Yule kafanya vile na kwanini yeye hajapata madhara au hajakamatwa.
 

Kuna hadithi moja ya mtu alienda kuiba kisha wakati anaondoka akadondosha kitu, kelele zikasikika na mwenye nyumba akaamka kauliza nani?, jamaa akajibu “nyaaauuu”. Mwenye nyumba akasema kumbe nyau kisha akapuuzia. Yule mwizi akaondoka na vitu na kwenda kumhadithia mwenzake. Mwenzake alivyosikia vile naye akaenda kuiba kwenye nyumba ile ile, nae wakati anaondoka bahati mbaya akadondosha sufuria ikatoa kelele mwenye nyumba akauliza nani? Yule mwizi wa pili akajibu “mimi nyau”, mwenye nyumba akamkamata na kumpatia kichapo cha paka mwizi. 

Hivyo tusijaribu vyenye kuhatarisha kwakua Yule kajaribu, kumbukeni ya kwamba tunatofautina kiakili, kiujuzi, busara hekima na heshima. Usije ukajikuta wewe umeshindwa lakini mwezako kaweza kisha ubaki unajilaumu “why me?”

Ukweli kuhusu kundi hili:-
Ni kundi lililo katika hatari kubwa sana kwani haliamini kua hauwezi kuacha kuajaribu. Ni kundi lenye kubeba vijana wengi wa sasa na wengi wao hushindwa kujimudu na huishia katika kundi la nimejaribu nimeshindwa kuacha.


Kundi hili pia linaona ni ufahari kujua vitu vingi vyenye kuhatarisha, na huwaona ambao hawajajaribu kua ni watu waliopitwa na wakati. Ni kundi lisilo bora mbele ya aliyobora ila wao hujiona ni wabora kuliko aliye bora.
 

Kundi hili hujisahau na walio wengi wao hukumbuka shuka wakati jua ndio linachomoza.

Kundi hili huwa na malengo mazuri ila wengi wao hishia kusema nilifikiriaga kuafanya ila nanihi ndio alisababisha nikaacha, halipendi pia kuchukua mzigo wa lawama wa walio yafanya, hupenda kuwabebesha lawama wenzao kwa makosa yao.


Kundi hili hupenda kuona hakuna aliye mbora kushinda wao, hivyo huja na mbinu mbalimbali za namna ya kuwashawishi ambao hawajajaribu waingie katika kundi lao. 


Kundi hili huwafanya walio wema wajione hawana maana na wasio wema wenye maana. 


Kwa walio katika kundi hili huwa wanaamini ipo siku watatoka katika hali ya kujaribu walioamua kuingia, hujikuta wanashinda kutoka hatimaye kudondokea katika kundi la tatu la jaribu kisha shindwa kutoka.


Ushauri wangu kwa kundi hili:-
Kwa minavyojua maisha yakikaribia kifo furaha huwa kubwa, mfano ni mtu anayeendesha gari kwa kasi hujisikia furaha kwakua yuko karibu na kifo na huwa hajitambui kuwa yuko karibu na kifo kwakua furaha hiyo humpumbaza.

Kwa maoni yangu juu ya mienendo ya watu wa kundi hili ni kwamba itafika kipindi wenye makosa watathaminiwa kuliko wale wema walio karibu na m/mungu wao. Kwa hali ilivyo sasa wale wenye kufanya mambo ya ajabu na yenye kuhatirisha kizazi cha sasa na cha baadae wanaheshimika na kuongelewa kana kwama ni mfano mzuri kwa kuigwa najamii.

Kipindi hiki ni  kibaya sana kwani wale walio wema na wenye malengo mazuri na jamii katika kuamsha, kuelimisha, kuimarisha, kuokoa na kuunganisha hawathaminiki katika jamii na hawapewi nafasi ya kuifikia jamii, ila kwa wale wenye kuhatarisha, kuathiri, kupotosha na kuangamiza jamii ndio wanaopea nafasi ya kuifikia jamii tena kwa haraka sana. Na pale mtu anapoona kitu hicho chenye hatari na jamii hukifurahia na kisha kukisambaza kwa marafiki zake kwa ufahari na kisha kitu hicho kuishia kuiathiri jamii nzima.

Sasa ningependa kulishauri kundi hili kua unapopanda changarawe hata ukapalilia vipi utaishia kuvuna changarawe, utakapopanda mahindi na kisha ukayapalia vizuri basi utavuna kilicho bora kwa faida yako na jamii yako.


Tusiwe watu wakuharibu vilivyo bora kwa kuviua vikiwa vichanga, tusiwe watu wa kupalilia visivyobora kwetu na kwa jamii zetu, tutambue ya kwamba mti  bora hutoa matunda yaliyo bora. Kumbuka ya kua kumkichwa ni wewe!

Kwa kua walio katika kundi hili huwa wanaamini ipo siku watatoka, baadi yao hufanikiwa ila kuna ambao hujikuta wanashindwa kutoka na huishia kudondokea katika kundi la tatu la jaribu shindwa kutoka.


Itaendelea....usikose makala hii sehemu ya tatu ya "Jaribu shindwa kutoka"..je unajua nini kinasababisha?...usisite kurudi tena hapa..kumkichwa ni wewe!

TANGAZO LA KAZI

Friday, July 6, 2012

Usiku Wa Epic Bongo Star Search- Club AQ


And here z the surprise for this Friday 06/07/2012 ,,,Salama Jabir,Joachim 'Master-j' Kimaryo na Madam Ritha kesho ndani ya Club Aq na crew nzima ya Epiq bongo Star Search,,njoo tujumuike nao na tujimwage usiku mzima,,,,watu 50 wa kwanza watakaotuma majina yao kwenda 0787276352 watapata punguzo la asilimia 50 kwa kiingilio cha kesho,,,hii si ya kukosa

Thursday, July 5, 2012

Kamchezo haka.


















Nakapenda haka kamchezo,
hakana hata maelezo,
masharti wala vigezo,

porojo tu na mizozo,
lawama ni siri ya mchezo.

Katamu haka kamchezo,
tutawazuga na tuzo,
kuficha wetu uozo,
tutawapa na pambizo,
burudani ni sehemu ya mchezo.

Unaposikia haka kamchezo,
mdomo weka likizo,
sikio lipe uwezo,
uongo nao ni chanzo,
hila ni dira ya mchezo.

Jamani haka kamchezo,
hakana hata ujazo,
thumni wala tozo,
utu kwenye mauzo,
ubaya ni mwanzo wa mchezo.

Ukitambua haka kamchezo,
tumia wako uwezo,
usizubae kama chezo,
usiponielewa anza mwanzo,
kuelewa sio dhamira ya mchezo.


 by Abeid Kajia (Kumkichwa)

Wednesday, July 4, 2012

"ViJANA NA UJANA"-Sehemu ya Kwanza “Makundi”


"Vijana na Ujana"
Niliposikia wahenga wanasema "Ujana ni maji ya moto" nilipata wakati mgumu sana kuwaelewa wanamaanisha nini kuhusu msemo huu, nikajaribu kuuchambua ili nijue lengo lake ni nini hasa. Nilianza kwa kuigawa hii sentensi katika aina za maneno:-

 Ujana/ni/maji/ya/moto,
 nikapata nomino mbili ( Maji, Moto)..
viunganishi viwili (ni, ya)..
vielezi vitatu Ujana kielezi cha namna/wakati, (ni maji) na (ya moto) vielezi hali.

Ninakajaribu kulichanganua kwa kuandika

(ujana ni maji):- kwa ninavyoyafahamu maji ni kitu kilicho katika hali ya kimiminika, yanaweza kua katika hali ya baridi au ya moto.

halafu nikapata tena

 (Maji ya moto):- ikimaanisha kimiminika kilicho katika hali ya moto au joto kubwa sana, ikimaanisha yamechemka na yaliyo na hatari kama hayatatumika katika hali iliyokusudiwa.

 Nikaamua kutoa (Maji) na (ya)

nikapata (Ujana ni Moto):- ikimaanisha kitu kilicho katika hali ya kuunguza ama kuungua, ambacho ni hatari kwa kuimbe kama hakitatumika katika kusudio lililotarajiwa.

 Mwisho wa kuchanganua nikaamua kuliunganisha tena na kupata msemo wa mwanzo wa wahenga ambao ni:-

“Ujana ni maji ya moto”

 Kwa maana ya kua maji ya moto ambayo ni ujana mtu akifikia katika hatua hiyo basi atakua yuko kwenye hatari ya kuungua muda wowote na madhara ya yake yakadumu kwa muda mrefu. Nikajiuliza kama ujana ni maji ya moto basi ukiwa bado mtoto ni maji ambayo yaliyowekwa kwenye jiko au? na Je! ukiwa Mzee ni maji yaliyopoa au?. Hapo sikupata majibu ila kwa ninavyojua kabla ya umoto ni ubaridi na baada ya umoto ni kupoa tena na kua baridi. Ila nikagundua kua Ujana ni maji na pia ni moto: unaweza ukazama au ukaungua, unaweza ukawaka kisha ukazima kwa maji. Hatimaye nikapata hitimisho la kua Ujana ni muunganiko wa hatari nyingi zinazofananisha na maji na moto au maji ya moto, na katika msemo huu lengo ni kuwakumbusha wale walio katika hali hiyo ya Ujana kuongeza umakini kwani wameafananishwa na mtu aliye karibu na maji ya moto ambapo asipokua muangalifu na makini basi  mtu huyu anaweza kuungua wakati wowote na maji hayo.


Ujana = Maji + Moto


Makala hii ni maalumu kwa vijana wenzangu ambao kwa pamoja tuko karibu na maji ya moto ambayo tunayachezea kila wakati pasipo kujua kua yanaweza kutuunguza na pia tunachezea moto pasipo kujua twaweza kuungua wakati wowote.

Ukitazama maandiko mengi ya kidini yanawasihi na kuwaasa vijana wawe karibu na m/mungu ili waweze kupita usalama katika kipindi hiki kigumu, ambacho kwa vijana wao hawaoni kama ni kigumu, ila kwa wale vijana walio makini na wenye malengo na upeo wa kuona mbali watakua wamenielewa na watakua wameziona hatari hiza zinazowakabili na wanajifunza kwa namna wanavyokabiliana nazo.

Ningependa kuwagawa vijana hawa walio katika hatari hizi makundi matatu..

                      i.        Usijaribu/sintojaribu- sintoingia (excellent and good)- vizuri sana na vizuri
                     ii.        Najaribu/Jaribu kisha ntaacha- ingiakisha toka (Good and bad)- vizuri na vibaya
                   iii.        Nimejaribu nimeshindwa kuacha- ingia kisha shindwa kutoka (bad and worse)-vibaya  na vibaya sana

                           I.      Vizuri na vizuri sana (sintojaribu,sintoharibu,sintoingia)

Kundi hili ni la wale vijana wasiopenda kujaribu vitu venye kuhatarisha, kundi lililo karibu na maji ya moto na lililo makini kwani linajitambua kua maji haya ni ya moto na yanaweza kuwaunguza wakati wowote, kundi hili ni bora na halipendi kuutumia Ujana wao kwa mambo yasiyo  na faida katika maisha yao ya baadae.

Kundi hili katika makundi ya vijana ni bora kwani huwa linachanganua na kuchambua kabla ya kufanya maamuzi na huwa sio kundi la watu wa kukurupuka. Huwa wanaonekana kama ni watu waliopitwa na wakati kwa vijana walio makundi ya chini (waliojaribu). Kundi hili huheshimika na hujiheshimu, halikubaliani na usemi wa “najifunza/ntajifunza kutokana na makosa”.

Ni kundi la watu wenye msimamamo na wanaojua ni nini wanachofanya, wengi wao hujitenga na makundi ya waliojaribu kwakua hawataki washawishike katika kujaribu.

Ni kundi lisilo na tamaa ya kutaka kujua ni hatari gani itakayotokea na hata kama litajaribu litaishia kutaka kufanya lakini likazishinda nafsi zao na fikra zao kwa pamoja.

 Pia ni kundi lisilokubaliana na usemi kua “nitaomba msamaha kwakua nitakosea”, ila huomba msamaha hata kama hawajakosea. Hujihisi ni wakosefu ingawa sio wenye kuendekeza makosa.

Kundi hili pia hushawishika ila ni kundi gumu katika kufanya maamuzi katika yakufanya kwa kujaribu chenye kuhatarisha, hivyo wanaowashawishi hukata tamaa na kuwaacha kua kundi lenye msimamo.

Kundi hili lina vijana wachache sana, kwani wengi wao huishia kwenye kundi la nimejaribu nikatoka.

Changamoyo wanazokutana nazo:-
“Uzeeni utakuja kufanya yale ambayo haukufanya wakati wa Ujana”. Sijawahi kuuthibitisha huu usemi kwa upande wangu ila kwa walio wengi walojaribu huutimia huu usemi ili kuwashawishi ambao bado hawajajaribu waingie katika kundi lao kwa kujaribu kwani watakuja kuchezea matope wakiwa watu wazima, nadhani hii ni kauli ya waliojaribu na ambao hawataki kuona aliye bora kuliko wao ambaye hajajaribu.

“Hakuna aliyebora ila kuna walio karibu na ubora” kundi hili kama hawata jaribu basi wanaweza kuwa wabora katika kundi la vijana wenzao, na pia kundi hili huwa na uoga wa kujulikana kwamba hawajawahi kujaribu, hivyo wanachokifanya huwa ni kuongea sana kuhusu wao kua wameshajaribu ili wasionekane wadhaifu kwa waliojaribu, ingawa kuna ambao hawajawahi kujaribu na huwa majasiri katika kusema kua hawajawahi na hawatajaribu. Hawa ndio wazuri sana na kwa wale wanaoficha hao ni wazuri tuu.

Ukweli wa kundi hili:-
Kwa walio katika kundi hili ningependa wawe wakweli kwa nafsi zao, kwani wanaweza kujificha wanapofanya na wanaweza kudanganya kwamba hawajawahi kufanya ila ukweli ukabaki ndani ya nafsi zao kua wamefanya sana kuliko waliojaribu kufanya. Wanaweza wakaamua kuonekana wabora lakini sio wabora kwa nafsi zao. Ukweli ni kwamba lazima kuna waliojaribu kisha wakomba msahamaha. Hivi ni kweli haujawahi kuiba? haujawahi kusema uongo? na haujawahi kutamani kisicho chako? Hajawahu kudhulumu? Je kula riba? Haujatoa ahadi ya uongo?. Ni kweli kwamba hakuna aliye bora ila kunawalio karibu na ubora. Usichezee matope kama hautaki kuchafuaka kwakua unajua maji na sabuni yapo utajisafisha..Je! kama haviko utafanyaje? Kumkichwa ni wewe!

Ushauri wangu kwa kundi hili:-
Akili kumkichwa ni kwa kichwa chako wewe, “aliyefanya ana tofauti kubwa sana na ambaye hajafanya, ila ambaye hajafanya akifanya tu atakua yuko sawa na aliyefanya, na aliyefanya hawezi kujirudisha ili awe sawa na ambaye hajafanya” hivyo kwa wewe ambaye haujajaribu chochote chenye kuhatarisha basi usijaribu chenye kuhatarisha kwani utakua sawa na aliye katika hatari. Usikubali ukashawishika kwa maneno matamu ya aliye katika hatari. Ila kwakua kumkichwa ni wewe kumbuka kutumia Akili yako katika kuamua lakufanya kabla ya kufanya. Majaribo mengine ni yenye kuhatarisha, unaweza ukajukuta kwenye hatari kubwa kuliko yule aliyejaribu kwakua alijaribu kwa umakini wewe ukajikuta umevamia bila tahadhari ya kujua mchezo unanendaje. Soma mchezo kabla haujaomba sub(haujaingia uwanjanikuucheza...

usikose kusoma sehemu yaPili ili ujue kundi la pili la "nimejaribu kisha nikaacha" likoje?...je wewe uko kundi gani?itaendelea...

RAPRACE WINNER

Fid Q feat Yvonne Mwale - Sihitaji Marafiki official video