Thursday, November 29, 2012

PASS THE MIC AROUND (SEASON 1 EPISODE 11) BACK TO THE SUA

At Kijenge ya Juu as always from 0300hrs to 0600
freestyle Battle,Cypher,Graffit and Djn...
Mtumbuizaji Maalim Nash (Nash Mc) atakuwepo

HAKUNA KIINGILIO
Stopa Rhymecca Yokoi WATURUTUMBI THE A TEAM ndani ya S.U.A
kikamchape kuwakilisha team!
Fredy Mlay hip hop knowledge is at S.U.A niggaz..
Tsaruh Dwayne Mc-cartney Pass da microphn pa pa pass da microphone ...!
Johnson AyoEvarlasting movement

POETRY AND JAZZ NIGHT @ MASAI CAFE

Come out on Saturday, Arusha Poetry Club lovers. Let's flow pamoja! Gonna also be some jazz music up in there!!! I am excited about that. This is such a taste of heaven to me!! Join us y'all! If you are a poet...bring your word! If you are a musician...bring your instrument/voice...if your are a lover of both, bring your ears!! We gonna have a great time! Karibuni Wote!!


If you are POET and member of APC - ARUSHA POETRY CLUB write A poem about KHANGA and TRADITIONS, you may win a chance to recite your poem on a stage of the festival organized by AAC - ARUSHA ARTS COLLABORATIVE 9th December at ALLIANCE FRANCAISE Arusha 8PM..only 2posts are available for the winners,while 10dollars will be given for each POET as transport fees.....post your poem on the timeline of ARUSHA POETRY CLUB on our facebook page..Ahsanteni.

-by George Kyomushula (Founder,Co-director of APC)


Wednesday, November 28, 2012

Picha za Siku 28th Nov 2012













Picha Zote zimepigwa na Kumkichwa

"Dunia ya Ushindani"

Photo by Af Arusha

Hizi mbio za sakafuni tazama ukingo wako ndio mwisho wako, kila mmoja macho kwenye mstari wa mwisho, pumzi na malengo visije vikapotea njiani, katika hii dunia ya washindani na mshindi hajulikani, kuna watakao anza kwa nguvu na kukaa mstari wa mbele na kuna watakao baki nyuma na kusubiria kufika mbele, kwa aliye mbele malengo yake kumpita aliye mbele yake lakini moyoni anahofia kupitwa na aliye nyuma yake.

Siku zote aliye nyuma humtazama wa mbele yake kwa makini kwa lengo lakutaka kumpiku na aliye mbele huwa anamhofia aliye nyuma yake kua anatambua huenda akampiku. Dunia ya ushindani ya mwenye kisu kikali ndie mlaji, wenye makali wanapowanyima vinoleo wasio na makali ili wasije wapiku kwa makali.

Dunia ya ushindani imejaa fitna na visa, tazama kwa makini usije ukawa mtumwa wa mtumwa wako, tazama waliopita na walioko juu namna wanavyohaha kuhofia walioko chini yao. Walio chini nao hawajui kua wananguvu kushinda walioko juu, ila fikra huru zimeingiwa na mdudu chuki, aliyemsafi kachafuliwa na wachafu kwa kuogopa usafi wake, hivi ni visa juu ya kisa. Kinachosemwa sio kilicho/wala kinachofanyika.

Panga kisha pangua, wagawe kisha watawale, nani asiyejua kua umoja ni nguvu, ili kuvunja vijiti vilivyoungana basi vigawe kisha vunja kimoja kimoja. Waahidi wanachohitaji ili upate unachohitaji, dunia ya ushindani, mwenye kisu ndie mlaji, asiye na makali ndio mtaji.

Tuanze na wewe kwanza, je upo kwa ajili yako ama kwa ajili yao? ubinafsi wa nafsi unavyozitesa nafsi . Mimi kwanza imefana machoni na mioyoni, kila kizuri kianze na mimi, moyo wa imani ya tule kwa pamoja kwa jasho imeshatoswa kwenye maji yenye kina kirefu.

Ongea pasipo kutenda, tenda pasipo kuulizwa, jenga kisha bomoa, jichotee kisha kana, mawazo ni mawazo hata kama hayana maana. Fikra za kweli hazifai wala hazina faida, changanya maji na mafuta ili twende sawa.

Nakusihi usichanganywe, usichanganye wala usichanganyikiwe, hizi ni fikra za ushindani ndani ya dunia ya washindani. Utakapo amua kufanya ukubali changamoto, hakuna atakayekuacha uteremke palipo na mlima, mkwamishaji wa kwanza ni wewe na nafsi yako, kumbuka ukiamua kufanya fanya, hakuna atakaye kuzuia, ila ni changamoto zinazokufanya uwe na fikra za kushindwa kwakua umeyaita ni matatizo/vikwazo badala ya changamoto. Kilicho bora kimeundwa kwa changamoto, kimeruka vikwazo, hakikutetereka, kilisimama na kutazama wapi kinakwenda na sio tu wapi kinakanyaga...!

Amkaa, Elimisha, Imarisha, Okoa kisha Unganisha. Panapo mwangaza angaza kwa kuamsha, pia elimisha kwa kutoa na kuingiza unavyovijua na usivyovijua, imarisha kwa kuvipa muongozo, okoa vilivyokosa tumaini na nafasi yakuona nafasi, waunganishe wawe kitu kimoja. Unapogawa unaondosha nguvu, unapounganisha unaongeza nguvu. Tazama kwa makini malengo yako je ni wewe au wewe na wao? Je kama ni wewe peke yako kwanini unalaumu wao kua hawana ushirikiano na wewe wakati hautaki kutambua umuhimu wa wao. Bila wao hakuna wewe, wewe na wao ni umoja, panda bora uvune bora..kiushindani kilicho bora ndio mshindi. Kuwa sehemu ya bora kwa kusaidia vilivyo bora..kumkichwa ni wewe!

Tuesday, November 27, 2012

UJUMBE WA MUHIMU KUTOKA KWA Maalim Nash


KWA HESHIMA NA TAADHIMA KATIBU WA TAMADUNI MUZIK NAPENDA KUCHUKUA NAFASI HII IKIWA NI MOJA YA JUKUMU LANGU KUWATANGAZIA KUA, TAMADUNI MUZIK TUMEPOKEA TAARIFA ZA MSIBA ZA MSANII MWENZETU, RAMADHAN HUSSEIN MKIETY AU SHARO MILIONEA KWA MAJONZI MAKUBWA NYOYONI MWETU, HATUNA LA KUSEMA ZAIDI, ILA TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AKUWEKE MAHALA PA AMANI KABISA, MBELE YAKO NYUMA YETU.. TUTAMALIZA MANENO YOTE LAKINI HISIA ZETU KWAKO HAZIWEZI KUZIDI MAPENZI YA MOLA WETU KWAKO NA NDIO MAANA AMEKWITA KWAKE..KWA HIYO TUMEGHAIRISHA UZINDUZI WETU JUMAMOSI HII KWA KUTOA HESHIMA ZETU KWA HAYATI SHARO MILIONEA.. NA UZINDUZI UTAFANYIKA JUMAMOSI IJAYO YA TAREHE 8/12/2012!M.A.P SHARO MILIONEA!OH MAMA! kutoka kwa  Maalim Nash

PHOTOGRAPHY EXHIBITION COMPETITION- ARUSHA...well done Brother George



George n Mama C

SWAHILI HIP-HOP EXHIBITION ni Bonge moja la DARASA by Scooby Askari Wa Miguu


 THE HIP HOP SUMMIT WAS A SUCCESS

"..SWAHILI HIP-HOP EXHIBITION ni Bonge moja la DARASA;siku mbili za za Exhibition hii pale ALLIANCE FRANCIE imenifundisha mengi sana kiukweli kuhusu HIP-HOP ya Bongo na mienendo yake kiujumla..wapi penye mapungufu na strategies za kuchukua ili sisi kama wapenzi na mashabiki wa Hip-Hop kuikomboa kwenye wimbi bovu la wengi wanaoichukulia HIP-HOP GENERATION kwa dhana tofauti na ualisia..

Shukrani sa
na kwa IMAM ABBAS. na crew nzima ya ARES ENTERTAINMENT;Alliance Francie;Ubalozi wa Uswisi;Bro Locko;Father Kitime & Mama Charlotte..bila kuwasahau wengi tuliohudhuria kama vile JCB & Mo Plus way long kutoka Arusha;Salu T kutoka Mbeya;The Ghana Dude;G-Solo;Saigon;Dj Legendary himself Dj JD;Maujanja Saplaya;Isanga Family;Dani Msimamo;Kimbunga;Sister Caroline;Mbishi Real;Machizi wa Machatta;Papaya;Songa na Malle + Potrayors wa TAMADUNIMUZIK waliokuwepo juzi pia;Brother Kingston wa Bagamoyo;Dj Kelvin;PeenLawyer;Edy Show Kazi na wote ambao nitakuwa nimewasahau...


Napenda sana HIP-HOP na out of the summit nimejifunza mengi sana ambayo yatanijenga na kunielewesha kiupana..natumaini itakuwepo tena mwakani na kwa waliokosa next tym msikose!!!"







The Hip Hop Summit that took place yesterday(23rd Nov 2012) in Dar es Salaam was a wonderful experience! Such a beautiful gathering of talents in one room! You could feel the energy flowing! The presenters brought a lot of information and the freestylin' was fantastic especially with the traditional instruments! I think this is going to be a new wave of hip hop here in Tanzania and am happy to be a part of it!
And the way everybody committed to come up with viable solutions pamoja, for some of the problems facing the hip hop community in Tanzania, warmed my heart and inspired me greatly!Big Ups to Acer Entertainments Family for all of the hard work organizing and making this dream of a positive gathering of Hip Hop artists and Hip Hop lovers, come true!! Congratulations to all who made the summit happen and all who participated! One more day in hot Dar then headed back home to the foothills of Mt Meru. Have a blessed day Y'all!! by Charlotte Hill O'Neal

Monday, November 26, 2012

mapande 20 barz na Nikki Mbishi

JUMAMOSI HII 1/12/2012 New Msasani Club


Usikose Jumamosi hii TAREHE 1 MWEZI WA 12, TAMADUNIMUZIK TUNAZINDUA TENA SANTURI 4 NYINGINE, KUANZIA SAA 9 ALASIRI HADI MIDA MIBOVU PALE PALE UWANJA WA NYUMBANI NEW MSASANI CLUB, 5000/= TU GETINI.
ZAMU YA :AZMA | KAD GO | MANSU-LI | MUJWAHUKI
Tamadunimuzik. Na HII Ni Review Fupi ya Kanda Mseto ya Azma