Wednesday, October 31, 2012

New Video SIJUTII - Joh Makini Ft. Dunga Official Music Video

Moment of Silence for Our Brother Lex J-bWanene's Cypher#2...

      RIP Lexa Julius.. Hiyo cypher ya pili tumeidedicated kwako:


#With 10 seconds moment of silence for our brother Lex J. Wanene's Cypher presents Cypher #2 - Daz Naledge (Watengwa), Chabba (Watengwa), JCB (Watengwa) and Boywonda (FlyButGhetto-FBG)

Tuesday, October 30, 2012

IN MEMORY OF BROTHER Lexa Julius





The 5th Edition of Arusha Poetry Club APC was dedicated to the memory of Bro Lexa Julius, a S.U.A. brother who was recently killed. We included libations to him and our Ancestors and many poems dedicated to him. S.U.A. reps, Biggie and Daz unveiled a new graffitti creation that was dedicated to Lexa also. After APC Wakunga Zamani went to the Empire and jammed a little bit with Bro Nicko P and his band. It was an enjoyable evening!!
 



 
 
Rest In Peace Comrade Lexa Julius.....

Monday, October 29, 2012

MAHOJIANO NA DAZ NALEDGE JUU YA UTATA WA TAARIFA ZA KIFO CHA LEXA




      HII NDIO TAARIFA KAMILI............ Lexa Julius ajachomwa kisu kama inavyo andikwa kwenye vyombo vya habari....
Marehemu alivamiwa na kundi la Makapurwa kwa nia ya kumuibia ...katika hali ya kujihami..walimpiga na jiwe kichwani ...ndugu zake walimrudisha Marehemu Lexa nyumbani..Kwa bahati mbaya alifariki usingizini..Report ya POST MORT UM inasema Damu ilivujia kwenye ubongo... ....kABLA YA MAUTI YAKE .alimtaja mmoja wa wahusika... ambayo mpaka sasa wamekamatwa wote na wamekubali kua wao ndio wahusika.... MAREHEMU HAKUCHOMWA KISU KAMA TAARIFA ZISIZO RASMI ZINAVYO ANDIKA....NA JCB HAUSIKI NA CHOCHOTE ..............................r.i.p ALEX JULIUS..................

Wakunga jamming with indigenous instruments (.c.) Kyomushula


I love the way Wakunga Zamani just lets it flow and flow and flow...we building indigenous instruments and learning to play them from each other. What an absolute 'trip' this is!!!

Dj Fetty HAPA UMEIPOTOSHA JAMII

 

hii ndio status ya DJ Fetty aliyoipost kwenye Page yake ya Facebook...
Dj Fetty
Lexa wa watengwa achomwa kisu, jcb ashikiliwa kwa mahojiano maana alikua wa mwisho kuwa nae, waliomchoma beto wakamatwa story ipo kwenye djfettt.blogspot.com


huyu ni mdau aliyekerwa na taarifa zisizo na ukweli ndani yake
presenter gani ww sasa, kama unaweza kutoa habari zisizo na ukweli tena kuipotosha jamii. Tafuta ukweli wa habari ndo utoe habari hewani. Kuwa wa kwanza kusambaza habari haimaanishi ww ndio wa kwanza kuipata. Usikurupuke, habari kuhusu kifo cha Lexa umekurupuka. Unatuzidushia machungu
baadae Daudi Bakari aka Daz Naledge ambaye ni mtu wa karibu na Familia ya Lexa akamshauri Dj wetu
Daudi Bakari I BET ITS BETTER YOU SEARCH FOR INFORMATION BEFORE YOU PUBLISH IT......WHO TOLD YOU LEXA GAT STABBED....?????
kAMA UMEPATA TETESI....WAAMBIE WA2 HII SIO TAARIFA RASMI....
ACHA WENGE ILI IONEKANE WE NDIO WAKWANZA KUPATA TAARIFA NA KUISAMBAZA...
HAKUNA ALIECHOMWA KISU TAFUTA TAARIFA...
 baadae Daz Naledge akatos taarifa kamili
Daudi Bakari
‎..............HII NDIO TAARIFA KAMILI............
Lexa Julius ajachomwa kisu kama inavyoandikwa kwenye vyombo vya habari....Marehemu alivamiwa na kundi la Makapurwa kwa nia ya kumuibia ...katika hali ya kujihami..walimpiga na jiwe kichwani ...ndugu zake walimrudisha Marehemu Lexa nyumbani.. Kwa bahati mbaya alifariki usingizini..Report ya POST MORT UM inasema Damu ilivujia kwenye ubongo...
....kABLA YA MAUTI YAKE .alimtaja mmoja wa wahusika...
ambayo mpaka sasa wamekamatwa wote na wamekubali kua wao ndio wahusika....


 MAREHEMU HAKUCHOMWA KISU KAMA TAARIFA ZISIZO RASMI ZINAVYOANDIKA....NA JCB HAUSIKI NA CHOCHOTE

..............................r.i.p ALEX JULIUS..................


 USIKOSE KUIPITIA KUMKICHWA BLOG AMBAPO TUTAKUA NA MAHOJIANO MOJA KWA MOJA NA DAZ NALEDGE JUU YA KIFO CHA LEXA JULIUS...USIKOSEE HII NI YA UHAKIKA...KUMKiCHWA NI WEWE!

Saturday, October 27, 2012

REVOLUTION THROUGH POETRY

ARUSHA POETRY CLUB presents REVOLUTION THROUGH POETRY
27th Oct.2012
Arusha Masai C@fe
6pm - 9pm

Revolution means different things to different people. But revolution is CHANGE...personal...community...the planet. Bring your poems and bring your ears. The Revolution through poetry is on!!!! Countdown to Saturday at Masai Cafe!! Plus Wakunga Zamani will have a jam in the gallery space at Masai Cafe. Brings your poems! Bring your ears! Bring your Friends!! Let's GO Arusha!
Wakunga Zamani will be in the house drummin' up the spirits through poetical music tonight at the 5th edition of Arusha Poetry Club...REVOLUTION THROUGH POETRY...in honor of our departed brother Lexa Julius and all the brothers and sisters
around the world who have gone too doggone soon. We can change the world comrades. Be there tonight! Bring your drum...your instruments...your words of poetry for Revolutions of Love!!! Yebo!!

 photo by George Kyomushula

R.I.P Lexa Julius

26th October 2012,,,no words to describe this day,U were a true brother and a friend to many,gone to soon ma brodah,,we got so much love for ya,,RIP brodah,,,,,,,

‎##LEXA JULIUS MASAI##
*Team SUA
*Team Nyakubi
*NYAU Director
***Raia Wako Tutakukumbuka Daima***(MAP)
I announce that I lost our dear comrade Lexa Julius.... 3rd of my brother whom has been killed caused by the violence.. REST IN PEACE MA BROTHER Lexa Masai R.I.P Fatha Nelly of X Plastaz ..R.I.P Pacha Izzy ....Im scared ! — with Bro Natty.
My heart is mourning a lot. Rest In Freedom my brother Lexa Julius. I will forever mourn you.
 
‎...R.I.P Lexa Julius...
Rest In Freedom Ma Boy LEXA JULIUS,,,,,Umetangulia hommies cc tutafuatia,,,,,Daaah Why Lexa???????????
Another young spirit has been lost in Arusha. Brother Lexa Julius, rest in peace. Many will miss you. Poleni sana to Brother Lexa's friends and family. Find comfort in the good memories of being with him! Aaiiieeee

NEW VIDEO SONG VVU- NASH MC (OFFICIAL VIDEO)



  • Abdul Mtamaduni Rutona ..LIKO WAZI HILO..!!

    Moni Awadh Charming Nishakamata wa nane wa tisa ni bele,vitend dhid ya manen

    Inno Classic hatariiiiiiiiiiiiiiiii.

    Moni Awadh Charming Tumefany mkon na uno,songa na kadigo! Huku dom ilikuwa mzuka maalim hukuwepo! Bonge moja la tamaduni

    Maalim Nash safi sana

    Ally Arsenal Podolski Vipi maalim kwani iko hewani.

    Mwalimu Daudi Yap yap yoo

    Andrew John Kazi nzuri kaka,hongera aisee
      
    Odonko Tyme Pamoja we can maalim tunaizindua mitaa 
    Dagger Mbarouq Jambya chapeni kazi wazaz kitaaa mnaeleweka ile kichiz wacha wakate viuno watoto wa juz toen video mkemee upuuz.
    Ibrahim Eto'o Saafi xana jembe kwakufanya kazi nzuri c wenyewe 2nawapa darasa wa2kibao kuhusu TAMADUNI MUZIK

    Kala Jeremiah True hip hop

    Abdulqadir Kiff Harakati zinaendelea, big up mzaz.

    Michizo Ahmed Hongera Sana Kaka!!
      
    VVU video is tight man..Bigup kwa kufanya Hihop ya ukweli...
         NAMSHUKURU M/MUNGU KWANZA NA PILI MUONGOZAJI WA VIDEO HII,TAWAKAL KHAMIS NA TATU WAUNGWANA WOTE HUMU FACEBOOK WALIOPOTEZA MUDA WAO KUISAMBAZA SEHEMU ZA KURASA NA MAKUNDI MBALI MBALI NA KWENYE KUTA ZENU PIA,WAPO RAFIKI ZANGU WENGI TU HUMU LAKINI HAWAJAFANYA HIVYO LAKINI MAISHA YANAENDA,KAMA WEWE BADO HUJAPATA BAHATI YA KUITAZAMA VIDEO HII BASI INGIA HAPA!

Friday, October 26, 2012

SWAHILI HIP HOP INTERNATIONAL SUMMIT 2012



IJUE MIXTAPE (KANDAMESTO)YA KWANZA KUFANYA VIZURI KITAA MJUE NANI SALEH JABIR
WALIYO ANZISHA TUSISAHAU........HISTORIA ITAWEKWA WAZI SWAHILI HIP HOP NA SAFARI HII...

NJOO........KUNA POSTA ZA UKUTANI NA JEZI ZAKE AMIR MAFTAH MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA /SIMBA AMBAYE PIA NI MEMBA WA SWAHILI HIP HOP FAMILY CLUB........YUPO PIA

THE LEGENDARY SALU-T (KING T) ATAKUWAPO NA BIDHA ZAKE ZA SANAA.......USIPIME BABU...
UKISIKIA PAAAA UJUE DARASA LINAONGOZWA NA SI MWINGINE BALI JCB Makalla Toka ARUSHA CITY......FROM KIJENGE JUUU......

SWAHILI HIP HOP INTERNATIONAL SUMMIT 2012(MONYESHO YA NGUZO TANO)

TAREHE: 22 NOVEMBER 2012


MAHALI: ALLIANCE FRANCAISE -NYUMA YA LAS VEGAS CASINO UPANGA


SAA: 2:30 ASUBUHI MPAKA 4:00 USIKU


BURE.....NJOO UNUNUE BIDHA KWA MSANII UNAYEMPENDA.....


Click here to review the event

Friday, October 19, 2012

Maoni Ya Watanzania Kuhusiana Na Udini..Kumkichwa Spread LOVE

 
Tanzania ni miongoni mwa nchi chache ambazo mtu anaweza kukutana na watu asiowafahamu na kupatana nao kwa mda mfupi bila hata kujua dini wala kabila jamani tusifike mbali tukagombana ndugu sisi kwa tofauti ya dini au itikadi.
 
Mwislam, mkristo, msikiti, kanisa, padre, sheikh, biblia, quran, Mtume, Yesu.. aren't the messeges the same ? Peace, love, harmony ? Why should we fight each other instead of fighting for each other? Where is the love ?
Hakuna mtanzania mwislamu, mtanzania mkristo, mtanzania mpagani, mtanzania hindu, tupo WATANZANIA tu... nawapenda watanzania wenzangu wote... One Country - One People - CHANGE TANZANIA !
NAJICKIA VBAYA SANA NINAPOCKIA UISLAMU / WAISLAMU TUNALAUMIWA KUHUSIANA NA FUJO ZINAZOENDELEA JIJINI DAR...

ASILIMIA KUBWA YA WASHKAJI ZANGU NI CHRISTIANS NA TUNAPENDANA SANA!!
 
...unajua onyo la 'ukweli' ukiambiwa unasahau....afu unakuja kukumbuka baada ya 'tukio'...afu unajifanya bado unasahau vilevile.....
Mungu Ibariki Tanzania Kiukweliukweli .
#BoraNipoHukuNapandaaZanguUpen
doCoachTu
‎"POLISI hawawezi kukamata WAISLAMU...Polisi inawakamata wanaovunja amani..iwe ni waislamu, wakristo au hata wasio na dini...Serikali makini haiwezi kuvumilia watu wachache wavuruge amani ya nchi hii kwa kuchafua dini ya Kiislamu"
KUNA TOFAUTI KATI YA WAUMINI WA KIISLAM NA WAFUASI WA PONDA,,SIO KILA MUUMINI WA KIISLAM NI MFUASI WA PONDA,,NAWAOMBA NDUGU ZANGU WAKRISTO MSISHUTUMU NA KUTOA MANENO MAKALI JUU YA DINI YA KIISLAM ,KWANI UISLAM KWA KUPITIA BARAZA LETU LA KIISLAM HATUTAMBUI WALA HATUSUPPORT UVUNJIFU WA AMANI UNAOFANYWA NA HAO WAHUNI WACHACHE wanaochafua na kutia doa DINI ISLAM.,,,ALLAH ATAILINDA DINI YAKE DHIDI YA waliopandikizwa chuki na kuchafua UISLAM,KWA KUFANYA MAOVU KWA KIVULI CHA UISLAM,WAISLAM WA KWELI NA WENYE IMANI WANACHUKIZWA SANA NA VITENDO HIVYO VYA UVUNJIFU WA AMANI NA UHARIBIFU WA MALI.
 
 Mama ananiambia DINI ni janga la kijiografia utapozaliwa ndipo imani yako itakapoangukia...ukishajua jua hili HAKUNA MATATA. Wakiuana haya, we angalia kwa mbali. Kwa shujaa huenda kilio kwa muoga huenda kicheko...!
         ####KumkichwaSpreadLove####

Toa maoni yako hapa chini kwa facebook au gmail..Ahsante

New Song TUKUTANE MAKTABA_Bonta Concious

New Song Dear God_Kala Jeremia

New Video_Dear God_Kala Jeremia

Breaking News....Taarifa zilizonifikia hivi punde..Kariakoo hali ni tete

Kariakooo
Haya ni maeneo ya kariakoo..hao ni wanajeshi

Jmani kariakoo kumegeuka uwanja wa vita...Ni mabomu tu ndo tunayasikia hapa...Jmani mungu tusaidie hili janga liishe...
Naona pilika pilika hapa posta mpya.. Asogee mtu
Kariakooooo,Posta,Magomeni Si Mchezo!!!!
‎..MUNGU ibark Tanzania Bara..MUNGU ibark Tanzania Visiwani..MUNGU ibark JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA..MUNGU wabark Watanzania..MUNGU ubark MUUNGAN0...
*HUSTLE 1*
Kimenuka kariakoo — at Kariakoo.
Taarifa zilizonifikia hivi punde znasema hivi hali ndg? mtulie majumbani/ ofisi! mwepuke kwenda mjini tayar nimekutana na magar ya FFU yanakwenda mjn wametandazwa asikari wengi sana kuna tetes kuwa kuna fujo badala ya swala ya Ijumaa Asante mjuze na nduguyo
 Endelea kutembelea Blog yako ya kumkichwa for updates

CHUO KIKUU CHA HIP HOP T-shirts On Sales Now...get ya copy





Call Natty Now +255 716 057 537 visit Natty Dreadz  for more info

THE BLACK N WHITE SHOW DONE IN KIGAMBONI

UJUMBE WA YUZZO KWA MA MC WOTE DUNIANI

Chindo/umbwa mzee ni Mc ninaefeel kuliko Ma Mc wote DUNIANI.
Big up blood!

  • Davan Trappe Namkubali sana Chindo pia!

    Kingston Bagamoyo saaana tena saana kwa kweli.nawatakia watengwa kila la kheir najua ipo ck tutawaona tena tz.ijumaa njema washaaaaabic woote wa hip hop bon kijenge1970 arusha kwa bingwa wa dunia wa ma mc chindo na shukrani saana jcb kwa kusaidia vichaa wa kitaa na babu daz kwa kuwa na sua vijana walionasa na umasikini kijenge juu vijana wanakaza afadhali mateja wamesanda.bagamoyo pia bendera inapepea dunia nzima.peace upon you.sisi sio manyani

    Askari Xygote Jombíì! The one n only...styles,vocal duuh! Yuko pekeee yuzo

    Biggie Roggie Shirima Now we are in the same team

    Hamisi Mohamed dap true rast jah bless watengwa

    Umbwa Lotuno Salute sana bro...Wewe pia kamanda wangu Nnaekukubali kwa mziki na Harakati Dunia mzima...Harakati zako Ni deep.

    Sajo Mwaiteleke umbwa mzee ndo anabweka feki Mc'z wote wanafyekwa

    Man Fure Nikweli yuzo umbwa nishaida niko magetoni saizi na msikiliza.! Xalute xana chindo?

    Erick Masasi Hakuna swari wala daught juu ya nyang'au,pamoja man

New Track Po'ah by Anto'Neyo [ The Artist ] - (Produced By quanBeatz)


Msanii wa Wanene Entertainment kutoka Marekani The Artist. Ambaye amefanya track ya Take Off pamoja na G Nako na AY amerudi na track yake mpya inaitwa Po'Ah iskilize hapa
 

Soon pia nyimbo zake pamoja na C'Pwaa Godzilla, One The Incredible, Lord Eyez, na Mabeste .inakuja

Thursday, October 18, 2012

DUNIA RANGI RANGILE ( 6 ) Sehemu ya Sita

                                              Na Lasima Nzao
   Mzee Songoro ndio hatunae tena..kibe bado hajapata taarifa za Kifo cha baba yake..je nini kitatokea..endelea

  Baada ya mazishi ya mzee Sosongo,Teresia alirudi mjini kuendele na shughuli zake. Baada ya wiki kuisha akaenda kwa bwana Kanjubai kumpa taarifa za msiba wa baba yake Kibe.
"sasa wewe nataka hii kijana irudi kijijini, yeye ilishaanza zoea kazi".
hayo yalikuwa maneno ya Kanjubai akimueleza Teresia. Teresia akamjibu,
"nimekuambia kuwa baba yake mzazi amefariki hivo lazima aende nyumbani akamuone mama yake na pia aone alipozikwa baba yake, baada ya hapo si atarudi aendelee na kazi yake?".
"hapo sasa mimi iko elewa wewe, kesho Moris atakwenda chukua yeye alete hapa, kwani siataweza kwenda menyewe huko kijijini?".
"akipakizwa katika gari la kuelekea huko kijijini atafika bila shida, sasa si utampa pesa za rambirambi?".
"Teresia!, Teresia!, wewe nafikiri pesa iko okotwa?, yeye anapata mshahara hiyo inatosha yeye".
"nafahamu kuwa anapata mshahara,lakini hii ni shida iliyompata mfanyakazi wako bwana Kanjubai, ni kiasi gani unachopata kutokana na kazi anayokufanyia?, ukijali masilahi ya mfanyakazi wako nayeye atajali na kujituma kwa bidii kazini".
"wewe iko maneno mengi sana, basi nitaangalia chakufanya but this because of you otherwise i wouldn't give him a dime".
"nashukuru kama umenielewa, sasa nataka mzigo mwingine maana ule wa mwisho haukukaa sana".
"hii ni kazi ya Moris, subiria yeye arudi toka huko alipoenda then atakupa".
"sitamsubiri nina haraka, kama wewe huwezi kunipa basi akija mueleze aniletee pale kijiweni kwangu".
"unataka akuletee kete ngapi?".
"mwambie aniletee kete tano".
"no problem, kwaheri".
"kwaheri Kanjubai". Kibe baada ya kujifanya uchunguzi kwa muda mrefu hakuna jibu alilopata, siku moja baada ya kazi akaambiwa kuwa ni zamu yake ya kusubiria watakao chukua malighafi ya siku hiyo.
Akiwa amekaa katika gogo huku akiwaza jinsi wazazi wake wanaendelea,Fabian akamfata pale alipokuwa, "inakuaje mtu wangu, mbona waonekana kama umehamia ulimwengu mwingine?".
"ooh bwana Fabi, niko poa mtu wangu na nafikiria kuhusu haya maisha".
"wanasema kuwa maisha ni kama kitabu kila siku unafungua ukurasa mpya".
"kweli mtu wangu, vipi huko juu kazi inaendaje?".
"huko shwari, unajua toka siku ile uniulize lile swali lako nimekuwa nakuchunguza ili nione kama we ni mtu wa siri au la".
"sikiliza nikuambie Fabian, mimi nilikwenda jando na jambo muhimu  tuliyofunzwa ni kuwa msiri, yale yote tuliyoelezwa yaliishia kulekule porini, hivyo kama hilo ndio lililokuwa linakupa hofu, shaka ondoa".
"shaka sina tena, ndio maana leo nataka nikueleze ujue kinachoendelea hapa, kama utataka kuendelea kufanya kazi hapa hiyo itakuwa juu yako".
"sawa, nitegulie kitendawili na unieleze yote".
"poa, siku ile uliniuliza kuhusu haya majani munayotwanga kila siku yana kazi gani,au sivyo?".
Kibe alipoambiwa hivo,akamsogelea Fabian hadi wakawa wanagusana
mabega,akamjibu, "haswaa". Fabian akatabasamu kisha akaendelea, "umeshawahi kusikia mmea uitwao coca?".
"sijawahi ila najua soda iitwayo coca".
"basi kuanzia leo ujue kuna mmea uitwao coca na yale majani munayotwanga ni majani ya huo mmea".
"kwahiyo soda ya coca hutengenezwa na haya majani tunayotwanga kila siku?".
"acha papara, umeuliza swali sasa tulia kama unanyolewa ili upate majibu".
"ni ile shauku  ya kutaka kujua maana nimesumbua kichwa hadi nimechoka, endelea kaka".
"sasa yale majani yanatengenezea cocain,si unajua cocain kuwa ni nini?".
"sijui na sijawahi kusikia hilo neno, kwani ndio nini hiyo?".
"umewahi kusikia madawa ya kulevya?"
"ndio si wanaita unga au hashishi?".
"baasi huo unga ndio cocain au mandrax, sasa yale majani mukitwanga hapa yanachukuliwa na kupelekwa kuchemshwa hadi yatoe nta, hii nta huchanganywa na dawa nyingine pamoja na mafuta ya taa hadi mwisho unapatikana unga mweupe pee kama poda, hiyo sasa ndio cocain".
Baada Fabian kumaliza kumuelezea Kibe,Kibe hakusema kitu, alihisi mwili kumtetemeka.
Fabian alipoona kuwa Kibe ameingiwa na woga, akamuambia, "oyaa mbona umekuwa mpole ghafla kama umemwagiwa maji ya baridi?"
"sio hivyo kaka hizi habari ulizonipa zimeniogofya, kusema ukweli sikutegemea kuwa kazi nifanyao ni haramu"
"haya sasa umejua, na usije ukamuambia yeyote nilichokueleza maana hiyo ni siri kubwa ukiitoa ujue unakaribisha mauti yako".
"usijali kaka, nilishasikia sana habari za wauza unga, sasa hata hamu ya kufanya kazi tena imeisha".
"kazi lazima ufanye maana huumwi, we fanya kazi huku ukitafakari niliyokuambia kisha uamue kama utataka kuendelea ama la, na kama ukiwaambia kuwa hutaki tena kazi yaweza ikakuletea madhila maana watakuuliza kwanini unaacha kazi".
"ngoja nifikirie kwanza maana hizi ni habari nzito sana kwangu, nikuulize swali?".
"uliza tu"
"hii cocain wanauzia wapi? na ushawahi kuionja kuwa ni tamu ama la?"
"unataka uionje?"
"siwezi na sitowahi kutumia hiyo kitu,nijibu basi swali langu".
"kuhusu sehemu inapouziwa sijui ila soko lipo tena kubwa sana na kuonja niliwahi kuionja, sio tamu, ladha yake niya uchachu".
"sasa kama ni chachu, wanapata raha gani kuitumia?"
"kile ni kilevi ndugu yangu, unanusa au unalamba kidogo baada ya muda unajihisi kuwa upo ulimwengu mwingine wenye raha zote za dunia hii".
"kwahiyo bado unatumia, maana unavyoielezea yaelekea umzoefu".
"hahaha,nimekuambia nilionja nikifikiri ni tamu kama glucose lakini sijawahi kuitumia, najua madhara yaletwayo na hizo dawa hivyo siwezi kutumia"
"kumbe ina madhara? mie nilifikiri ni ulevi pekeyake".
"ile kitu ukianza kuitumia kuiacha itakuwa shida, na usipoipata wakati itakapokuwa imekuzoea, utakuwa hoi kwa ugonjwa, kila kiungo kitakuwa kinauma".
"duuh! sitaki hata kuiona, nashukuru sana Fabi, kwa kunifumbulia fumbo lililokuwa linanitatiza toka nifike hapa".
"hakuna shida mtu wangu chamsingi haya niliyokueleza yaishie hapahapa, kama utataka upigwe risasi ya kichwa basi utoe hii siri, usije ukasema sijakuonya".
"shaka ondoa kaka,ngoja mie nirudi kwenye makazi yetu nikaoge maana nimechoka sana"
"poa, kwaheri Kibe"
"kwaheri kaka".
Kibe alipofika katika makazi yao, akamkuta Moris akimsubiria. Moris akamuambia kuwa amekuja kumchukua maana Teresia amerudi toka kijijini na Mzee Sosongo anaumwa sana hivo Kibe anatakiwa aende. Kibe akajitayarisha kisha wakaondoka na Moris. Alipofika mjini akapelekwa kwa Teresia.
Teresia alipomuona machozi yakaanza kumtoka, akamkumbatia Kibe kwa muda bila kusema lolote huku akilia kwa kwikwi. Kutokana na hali ile Teresia aliyoionyesha, Kibe moyo ukamuenda mbio, wazo likamjia kuwa baba yake atakuwa hayupo tena duniani, akajikaza kiume na kumuambia dada yake,
"dada mie ni mtoto wa kiume kama kuna lolote baya we nieleze tu maana mabaya na mazuri tumeumbiwa sie wanaadamu".
Teresia akatulia kisha akaenda kukaa katika kochi, Kibe akamfata pale alipokaa, akakaa pembeni yake na kushika viganja vyake akamuambia,
"kwanza shemeji yupo wapi?". Teresia akavuta pumzi ndeefu,
"shemeji yako amesafiri jana atarudi baada ya wiki mbili".
"sawa dada nipe hali halisi uliyoikuta huko kijijini na usinifiche maana mie sio mtoto mdogo".
Kibe akatabasam na kumuangalia machoni,"oooh Kibe mdogoangu, kifupi nikuwa baba hatunae tena, mzee Sosongo ametutoka". Kibe alipoambiwa hivyo alihisi kama amekatwa maini,alikuwa anahisi
kulia,lakini machozi hayakutoka, akabaki kuangalia tu dari, Teresia akamkumbatia na kumuambia,
"usiogope kulia mdogoangu, lia maana itakusaidia kutoa uchungu rohoni".
Teresia alimalizia tu maneno yake, akaanza kulia tena kwa sauti. Kibe hakutokwa na machozi ila alihisi kuishiwa nguvu, wakati Teresia anaendelea kulia huku akiwa amemkumbatia Kibe,alihisi kuwa Kibe
amekuwa mzito ghafla, akamsukuma ili amuangalie machoni lakini alikuwa amelegea.
Teresia kuona vile akamlaza katika kochi kisha akafungua vifungo vya shati nakuanza kumpepea, baada ya muda Kibe akafungua macho, Teresia akampa maji yenye glucose akanywa.

Baada ya muda akarudia hali yake ya kawaida na akamuuliza Teresia,
"baba amefariki lini?"
"hii ni wiki ya pili toka afariki, nilipoenda kipindi kile nilipokutumia taarifa kuwa naenda kijijini,hali yake haikuwa nzuri".
"sasa mbona sijapewa taarifa pindi tu alipofariki?"
"Kibe mdogoangu, wafahamu vema mazingira ya kijiji chetu, na hupo unapofanyia kazi hakuna simu hadi mtu atoke huku aende huko kutoa taarifa".
"sawa dada,kesho asubuhi nataka niende nyumbani".
"sawa mdogo wangu".

................itaendelea wiki lijalo....