Friday, October 22, 2010

ZAiDi YA JiNA! ViPi HESHiMA?Tunapotega masiko yetu katika redio lengo ni kujua nini kimejiri katika taifa letu kwenye taarifa ya habari, ama tunapotazama runinga zetu wakati wa taarifa ya habari lengo ni kujua nini kimejiri, wakati huu ndipo binadamu anapoheshimu hisia zake ili aweze kupata ujumbe au taarifa kwa wataalamu wa habari, na wengi wao hupata taarifa walizozitegemea kutoka katika chombo alichokiheshimu.
Sasa chombo hiki kimeheshimika kwasababu kinatoa taaarifa ya habari iliyo sahihi na iliyochambuliwa na wataalamu wahabari nakupitishwa kuwa moja ya habari bora zilizochaguliwa kusomwa na mtaalamu wa kusoma habari. Baada ya taarifa ya habari kunakua na matangazo ambayo yanaletwa kwenye runinga na redio ili kuwajuza watu kuwa kipi kimeundwa na wataalamu ili kiweze kutangazwa na kuweza kuheshimika na lengo ni  kiwafikie wasikilizaji na watazamaji walio wengi.
Pale mtu anapoamua kufanya kitu ujue kwamba alishakifikiria, hivyo anataka afanye kitu kilicho bora na kuweza kuvuna na kujivunia  kilivyo bora, mtazame mkulima anaanza kwa kutayarisha shamba, baadae anapanda na baadaye kuvuna, na kwa kipindi chote hicho amekua analitazama na kulilinda shamba lake kwa umakini mkubwa sana, huwa anaitwa mkulima kwakua anaelewa nyakati za kufanya ukulima wake, yeye ni mtaalamu wa kulima ndio maana anaitwa mkulima, pia ni mtu huyu anayeheshimika kwasababu anaheshimu taaluma yake, kwasababu anayeheshimu sana shamba lake, jembe pamoja na mbegu. Huwezi kukuta mkulima anacheza na jembe wakati wa kulima, au anachezea mbegu wakati wakupanda, huwezi labda kama sio mkulima,  ila kama wewe ni mkulima basi utaheshimu ukulima wako.
Kwa hiyo kama wewe ni mwanafunzi, daktari, mwalimu, mfanyabiashara, mwanamuziki, mwanasiasa au mtu mwenye utaalamu fulani lazima uheshimu utaalamu wako na ufanye jitihada kusoma nyakati ili usije ukapotea katika dira ya utaalamu wako. Unapoona ama kusikia mtu anaitwa mataalamu ujue ni zaidi ya jina na ni mtu mwenye elimu, ustadi au ujuzi  wa fani au jambo fulani maalumu , mwenye malengo na upendo na utaalamu wake.
Kiukweli dunia ya sasa imebadilika, imekua dunia ya wataalamu na mwenye utaalamu ndiye anayepewa kipaumbele katika mipango iliyo endelevu. Itafika kipindi watu tutakua tunaaminiana sana kutokana na kila mtu amekua mataalamu wa jambo fulani, inafika kipindi kunakua na sehemu maalumu ya kuwakuta vijana wa Kitanzania wakiwa wanajadiliana kitaalamu kua tunataka tufanye jambo la kimaendeleo ili kuliletea Taifa letu maendeleo kwa heshima zaidi ya jina.
Hii inawezekana kama vijana wa kitanzania tukiamua kuheshimu hisia zetu, wewe kama kijana unataka uwe nani hapo baadae? Baada ya hapo uiheshimu mipango yako, “kwasababu tukiamua kwamba tunaweza kisha tukajifikiria kwamba tutaweza  basi tumeweza”.  Vijana wengi tunashindwa kutimiza malengo yetu kwasababu hatuheshimu mipango na malengo yetu, wengi wetu tunajikuta tunaishia katika fani ambazo sio zetu, hivyo tunazidi kulipotosha taifa letu kwa utaalamu usio katika fani na ndoto zetu alimradi tusife njaa.
Siku zote ukitaka kufanikisha na kufanya kitu kikawa kizuri, basi kifanye wewe mwenyewe kwa moyo wako na kwakupendo wako toka moyoni mwako, ni vizuri tukaheshimu hisia zetu kwa kufanya kazi tulizoziota tokea utotoni. Tusiishie kukimbilia bora fani ila tupiganie kupate fani bora
Pia sisi kama vijana kama tunataka kuwa watu hapo baadae, yatupasa  tuheshimu taaluma zetu ili tuje kua wataalamu wa fani mbalimbali, tusiwe watu wakutizama  upeo wa macho na pua bali  tutazame mbele wapi tunaenda na wapi tuna taka kufika, ni malengo gani tumejiwekea, pia tusiwe wataalamu bora kwakuongea sana bali wataalamu bora kwakutenda kwa vitendo. Najua ni vingi vinahitaji mabadiliko ila anza kwa kujibadilisha wewe mwenyewe, angalia nini kinachohitaji mabadiliko ndani ya moyo na fikra zako, tusiwe watu wa kuacha mambo yaende kama yalivyo, bali watu wakubadilisha mambo yaende kama tulivyo na namna tunavyotaka yaende, tusiendeshwe wakati tunaweza kuendesha,  tutasubiria mapaka lini mkombozi arudi, wakati wakombozi ndio sisi wenyewe na nafsi zetu. Kijana "kujikomboa kifkra na kiroho, ndio ukombozi wa mkombozi aliyesema atarudi". kijana wa leo jitazame zaidi ya jina kwamba wewe ni nani? vipi heshima iko pamoja na wewe? unaheshimu taaluma yako? Je wewe ni zaidi ya wanavyokutazama? nakusihi kijana mwenzangu kwamba kutafuta taaluma ndio heshima ya kwanza, jina litakuja wakikuhitaji. Watakuita tu....ULAMAA KUNA KAZi TUNATAKA UiFANYE..!Kumbuka kwamba kumkichwa ni wewe!

Thursday, October 21, 2010

Wednesday, October 20, 2010

KUMKiCHWA CLUB

JE! UNAiJUA kumkichwa.blogspot.com.WAKATi WA MAPiNDUZi SASA UMEWADiA.TUMUOMBE MUNGU ATATUSAiDiA.......kumkichwa.....