Tuesday, July 31, 2012

Fahamu Hatua Sita (6) za Kutengeneza Blogu/Blog kutumia BLOGGER


Blog
         Blogu ni teknolojia mpya inayowezesha watu binafsi kuchapa maoni na fikra zao katika mtandao wa tarakilishi. Blogu inaweza kuchukuliwa kama ni shajara pepe. Neno "blogu" ni tafsiri ya Kiswahili inayotokana na neno la kiingereza, "blog." Neno "blog" limetokana na neno jingine, "weblog." Kimsingi, blogu ni aina ya tovuti ambayo huandikwa mara kwa mara na kwa mpangilio wa mambo mapya kutokea ukurasa wa mbele kuendana na tarehe na mwezi.

         Zipo blogu za aina mbalimbali. Kwa mfano, blogu za maandishi, blogu za mkononi, blogu za picha, blogu za sauti, na blogu za video.

         Blogu ya mradi wa Global Voices inaandika muhtasari wa majadiliano na habari zinazojitokeza katika blogu mbalimbali duniani, hasa nje ya Marekani. Mradi huu una wanablogu katika nchi mbalimbali duniani ambao wanaandika juu ya masuala muhimu yanayojitokeza katika blogu za nchini mwao au katika bara lao...soma zaidi kutoka wikipedia kuhusu Blog kwa kiswahili http://sw.wikipedia.org/wiki/Blogu

kwa kiingereza Read more about Blog in English through Wikipedia http://en.wikipedia.org/wiki/Blog


     Zifuatazo ni hatua sita za namna ya kutengeneza Blogu..kutengeneza na kumiliki blogu ni bure...ukitaka kujua faida zake usikose kusoma makala ya Faida na Hasara za blog:


1.Ingia kwenye Google Search
  
 2. Search Blogger kisha chagua Create your Free Blog au Create blog

3. Ingia (Sign In) kwa kutumia Gmail Account Yako na Password yako..hizi ndio zitakua utambulisho wako kwa blog yako.
 

 
4. Chagua Create a Blog 


5. a. Andika Jina la Blog kwa Herufi KUBWA 
    b. Jina Blog Address kwa Herufi ndogo.
    c & d. Kisha Bonyeza Check Availability ikionesha Sorry, this blog is not available basi jaribu jina lingine mpak ioneshe kijani yaani This blog address is available. 

  e.Jaza hayo maneno hapo ili kiunesha kua sio robot bali ni mtu
  f.The bonyeza continue hapo chini kulia kisha kuendelea

 

6. Baada ya hapo utakua tayari umeshatengeneza Blog yako…unaweza kubonyeza New Post ili kuweka habari au picha, au ukabonyeza View Blog ili kujua muonekano wa blog yako.

huu ndio muonekano wa kwanza wa blog baada ya kuitengeneza


Mpaka hapo nadhani utakua umeshafahamu namna ya kutengeneza blog kwa kutumia Blogger...kwa maoni, maswali au ushauri tuandikie hapo chini kwenye sehemu ya maoni....Ahsante Sana Kumkichwa

4 comments:

  1. Kaka mm naomba unijuulishe cfa za mtu anaefaa kua na blog

    ReplyDelete
  2. Kaka mm naomba unijuulishe cfa za mtu anaefaa kua na blog

    ReplyDelete
  3. Mtu yoyote anaweza kumiliki Blogu.. ukiweza kukidhi mahitaji yao basi waweza kumiliki blogu yako.. Ila kwa ushauri ni vizuri ukawa na lengo zuri nayo.. kumbuka Kumkichwa ni wewe!

    ReplyDelete
  4. Thnkx mm natka blogu ya kutngaz biashara Broo nifnyeje?

    ReplyDelete