Thursday, September 6, 2012

Breaking News from Watengwa Recs


Watengwa Recs
       Habari zilizotufikia hivi punde kwa Kumkichwa kutoka kwa Producer Daz Naledge wa Watengwa Recs pale Kijenge Juu Arusha Tanzania ni kwamba...........
 
       "Watengwa records imepoteza data zoooote baada ya fundi wa Computer aliyepewa dhamana ya kuifanyia Machine/Computer matengenezo yenye data za Studio kuiformat machine nzima....Jambo la ajabu na la kushangaza ni kwamba siku tatu zilizopita Hard drive zilizokua zimeungwa kwenye machine hiyo zilizimika kabisa...mpaka sasa moja imekubali kufanya kazi ila haina data zinazohitajika....tatizo hilo ndio sababu iliyopelekea computer hiyo kupelekwa kwa wataalamu wa Computer (Jr eletronics) kwa matengenezo.. 

      Hapo ndipo jamaa aliyeachiwa Computer hiyo kufuta partition zote wakati yeye alipewa maagizo ya kuondoa Windows iliyokuwepo na aweke nyingine.

      Kutokana na tatizo hilo project ya fulu ile laana Vol.2 imepoteza nyimbo 7 japo kwa bahati nzuri data ambazo hazijafanyiwa editing zipo salama...

      Pia project ya Nyota Njema ya Mtaa (Album ya Chaba) na mixtape ya Wa2 wa Wa2..na nyingine zoooote zime corrupt/futika ...

      Hivyo kutokana na tukio hili tuliwajulisha wahusika hali halisi na tunashukuru kila mmoja alikubaliana na matokeo. Hivyo kwa sasa watengwa recs itafungwa kwa muda...Tutafanya matengenezo na tukirudi kila kitu kitakua BRAND NEW. 


Ahsanteni 

Daz Naledge


Daz Naledge


No comments:

Post a Comment