Monday, November 12, 2012

DUNIA RANGI RANGILE ( 8 ) Sehemu ya Nane


                              
  Mtunzi : Lasima Nassoro 

Tulipoishia ..Bwana Kanjubai ameafiki Kibe Kuacha kazi,ila kuna jambo kimemkumba bwana Kanjubai? unataka kujua ni nini?...endelea....

   Teresia akavuta pumzi ndefu kisha akasema, "toka niongee na Samson, wiki imekwisha".
Kanjubai akatoa kitambaa toka katika mfuko wa suruali yako, akasafisha miwani yake, alipoona imetakata akaivaa na kwenda kuegemeza mikono yake nyuma ya kochi alilokaa Teresia, akamuambia Teresia,
"unaweza ukanifikiria kuwa pengine nina over react but i'm not, kwani toka Samsom asafiri ni muda gani umepita?".
"nafikiri ni wiki tatu na siku kadhaa,lakini nilipoongea nae aliniambia kuwa biashara si nzuri huko alipo", hayo yalikuwa maneno ya Teresia. Kanjubai akatoka pale alipokuwa ameegemeza mikono yake na kwenda kukaa kochi lililokuwa limegeukia alipokaa Teresia.
"dont make me laugh, so ana claim kuwa biashara sio nzuri ndio maana hataki kuwasiliana na mimi?,c an you believe toka atoke hapa siku zote hizo hajawahi kunipigia simu?, and he says biashara sio nzuri, kwani nilimtuma akachuuze kama mchicha?".
Teresia akaanza kutokwa na kijasho chembamba, akamjibu Kanjubai, "kusema ukweli mimi sijui mapatano yenu kama ulimtuma akachuuze au la".
"nilimuamini sana Samson hadi kufikia kumtuma kwenda kupeleka mzigo wa millions of shilings, sijui ni ibilisi gani aliyeingia kichwani mwake".
"au pengine amepatwa na matatizo huku sie twamlaumu tu", Teresia alimuambia Kanjubai huku akikwepa kumuangalia machoni.
"siku zote nikimtuma Lilongwe namuambia apeleke mzigo kwa mr Makuya, but Mr Makuya nimewasiliana nae anasema hajamuona, mwanzo nilifikiri kama ulivyosema kuwa pengine amepatwa na matatizo so nikaamua kutumia my souces kujua ukweli... Teresia akamkatisha Kanjubai.
" kwahiyo umegundua kuwa hana tatizo lolote?".
"listen to me Teresia and listen good, mimi naitwa KANJUBAI, nobody and when i say nobody I MEAN NOBODY can double cross Mr Kanjubai and get away with it, kama utawasiliana na Samson, muambie kuwa kama anataka usalama wake apeleke mzigo wangu kama alivotoka nao huku bila kupungua hata chembe amkabidhi mr Makuya na haya yote tutayasahau kama yalitokea na maisha yataendelea kama ilivokuwa hapo awali, kama hatafanya hivyo, hahahaa tell him kuwa he will pay big time, and this is  not a threat,  it’s a fact, muambie kuwa know nimeshajua alipo, infact hiyo simu uliyonikuta nikiongea nayo wakati unaingia hapa, ilikuwa inatoka kwa one of my man, so asifikiri kuwa anaweza kujificha na
nisimpate".
"sawa bwana Kanjubai, nitajitahidi kama nitampata nitampa ujumbe wako".
Kanjubai akasimama, akasema , "please do that,if you will excuse me nataka nijiandae kuelekea uwanja wa ndege, na muambie Samson huwa nikisema kitu huwa sirudii mara mbili".
Teresia akanyanyuka na kuaga,bwana Kanjubai wala hakumjibu kuonyesha ni jinsi gani alivokasirika. Teresia alifika kwake bila kujua amefikafikaje kwakuwa alikuwa amejawa na mawazo kuhusu mambo aliyoelezwa na Kanjubai, 'kweli tamaa mbele ni mauti, Sam my dear, ni sheitwan gani aliyekuingia hadi kufiria kutoweka na mzigo wa watu?, kwani ulikuwa hutosheki na pesa uliyokuwa unapata?', hivo ndivo Teresia alivyokuwa anawaza, hakujua la kufanya maana alijaribu kupiga namba ya simu ,Samson aliyompigia mara ya mwisho lakini jibu alilopata ni kuwa namba hiyo haipatikani.
Teresia akaamua kuwa siku hiyo hataenda kufungua kibanda chake cha biashara,alijihisi kuwa hatoweza kuongea na wateja. Akaamua kutegesha saa kila baada ya nusu saa iwe inapiga kengele ili awe akijaribu kumpigia Samson simu. Saa kumi jioni ilipofika akastuka kuwa toka anywe kikombe kimoja cha uji asubuhi, hajatia kitu kingine tumboni, akaamua kwenda jikoni kuangalia kuwa ni kitu gani anachoweza kupika kwa haraka. Akakuta kuna viazi alikuwa amenunua na kuviweka katika jokofu, akaamua avimenye apike na kipande cha samaki mkavu. Wakati anaendelea kumenya mawazo yake yote yakahamia kipindi
alipokutana na Samson,akakumbuka siku ile ambayo Samson alikuja kibandani kwake kula chakula, baada ya kuagiza wali na maharage na mboga za majani, akamuuliza Teresia,
"hivi umeanza lini kuuza chakula hapa, maana mara ya mwisho niliposafiri hiki kibanda hakikuepo".
"nina kama miezi mitatu toka nianze kufanya biashara hapa, kwani wewe unakaa maeneo haya?".
"nakaa mtaa wapili toka hapa,mwanzo ulikuwa unafanyia wapi biashara? maana msosi wako mtamu sana".
"asante na kama umegundua kuwa mapishi yangu ni mazuri basi wakaribishwa hapa 'LISHE BORA KIOSK', sijawahi kuuza chakula sehemu nyingine, hapa ndio pa kwanza".
Samson huku akichota chakula na kukijaza mdoni, "usinishangae kula yangu, nina haraka natakiwa saa nane niwe uwanja wa ndege". "unasafiri?", Teresia alimuuliza Samson.
"hapana kuna mgeni wa boss wangu naenda kumpokea".
"basi angalia usije ukapaliwa hadi ukashindwa kwenda huko uwanjani na mie sitaki kulaumiwa kuwa nimefanya uchelewe kwa kukuongelesha wakati unakula".
Samson akameza chakula kilichokuwa mdomoni kisha akamuangalia Teresia kitambo kidogo bila kusema kitu. Teresia alipogundua kuwa anaangaliwa,akamuambia Samson, "mbona wanikodolea hivo hadi najihisi kama vile sijavaa nguo?, maliza chakula uwahi huko ulikotumwa la sivyo kibarua kitaota nyasi".
Samson akatabasam kisha kaendelea kula bila kusema neno, alipomaliza kula akaomba maji ya kunywa, baada ya kunywa akasema, " na hayamaji, yamechemshwa kweli?, nisije nikaumwa na tumbo hapa nikashindwa kwenda kumpokea mgeni".
"aka babu wewe, maji yangu nimechemsha kisha nikayachuja, ukiumwa tumbo usije ukasingizia maji, pengine ni umekula kiporo asubuhi".
"hahaha,kwanza mimi sio babu, usinizeeshe bure mtoto wa mwenzio, pili sijala kiporo, labda kama huu wali ulionipa ndio kiporo".
"usijali hapa kila kitu ni fresh, sipiki chakula kingi sana hadi kibaki".
Baada ya Samson kulipa pesa ya chakula alichokula, akamuuliza Teresia, "hivi waitwa nani vile?"
"unauliza kama vile unanifahamu, naitwa Teresia"
 Samson akatabasamu, akasema huku akitingisha kichwa kwenda juu na chini,
"Teresia,Teresia,Teresia,jina zuri sana, mbona hujaenda kuwa mtawa?".
"hahaha, jina langu na utawa vina uhusiano gani?".
"unajua jina Teresia, au Teresa, watu wengi wenye jina hili ni
watawa,kwani hujawahi kusikia mother Teresa?".
"nimewahi ila jina ni jina tu halihusiani na imani au kazi afanyayo mtu".
"anyway, mie naitwa Samson, Samson Makereba".
"hahahaa" Teresia aliangua kicheko.
Samson akamuangalia hadi alipotulia,"sasa wacheka nini?".
"nacheka hilo jina 'MAKEREBA', jina lawapi hilo? limekaa kama jina la spare part, hahahaa".
"jina la heshima hilo, watu wanalilia we unacheka".
"kama kuna wanao litamani ni shauri yao".
"haya bana,kama wacheka jina langu bora niondoke".
"sema unachelewa na sio vile nilivyo cheka ndio kuna kufanya uondoke".
"ngoja niende ila nikipata muda nitakuja tena kula maana huu msosi unaopika, mmh si mchezo, sijui ulipoondoka huko kwenu ulipitia kwa bibi akakupa kandumba kidogo kakuchanganyia ili watu wakila tu wanogewe ili warudi tena?".
"hapa hakuna cha ndumba wala nini, ni upishi wa mwanamke aliyefunzwa akafunzika namna yakuandaa maakuli".
"kwaheri maana yaelekea umuongeaji mzuri, ndio nimekuona leo tu lakini waongea kama twafahamiana kwa muda mrefu".
Teresia akatabasamu kwakukumbuka siku ile alipokutana na Samson. Baada ya kutayarisha chakula chake akala kisha akasafisha vyombo alivyotumia. Saa moja usiku ilipofika, akajaribu tena kupiga simu ya Samson lakini jibu likawa ni lilelile, haipatikani. Akapata wazo kuwa awasiliane na Moris amuulize kama ana mawasiliano na Samson. Alipompigia simu, Moris akamjibu kuwa hajawahi kuwasiliana na Samson toka aondoke. Teresia akaanza kukata tamaa ya kumpata Samson tena,' sijui wameshamuua? na kama Kanjubai alivyonieleza kuwa anajua alipo ni kweli, ooh Samson,k wanini umeamua kucheza na maisha yako?', hayo yalikuwa mawazo ya Teresia. 'afadhali Kibe alivyoamua kutorudi kufanya hii kazi, kila wakati mtu unakuwa na wasiwasi kuwa utakamatwa,hata sijui nilikubali vipi kushiriki hii biashara,ama kweli majuto ni mjukuu'. Teresia akaamua kuwasha tv, akaweka stesheni ya malawi kuangalia kama kuna habari zozote zinazoweza kumhusu Samson, lakini hakuona, akaamua kuangalia wanyama.
Je ni kweli Samson amekimbia na mzigo wa Bwana Kanjubai? je samson amekimbilia wapi? je nini kitatokea akigundulika alipo? usikose sehemu ya tisa ya hadithi hii...itaendelea....

No comments:

Post a Comment