Thursday, March 7, 2013

SHAIRI LA SIKU YA MWANAMKE DUNIANI 8TH MARCH.2013


NI WEWE

..wa kike kiumbe uliyeshushwa toka mbinguni,

kwa nguvu ya Maanani,
ukatoka kwangu ubavuni,

mwanga ukapata niangazia njia,
kwa maneno yako ya faraja hata iwe mchana kila Adam anaweza pata kusinzia,

ni wewe,
mwanamke wa kuvutia,
uwe mweupe ama mweusi,
hakika sitoacha kukusifia,

kwetu waume umetuangazia nuru,
kwa furaha basi tukeshe kupiga ndulu,

si mwengine wa kumshukuru,
wetu Mungu pekee ndiye tunapaswa kumshukuru,

mwanamke leo ni siku yako,
mwanaume apaswa aingie jikoni aje kukupikia SATO,

sema chochote utakacho,
furahia siku yako,

mwanamke wewe humu duniani,thamani yako katu isifanyiwe utani,

yapaswa dunia ikulinde,dunia ikutunze kizazi na kizazi nacho kikutunze,

heshima,na hekima,
nidhamu isiyo na hatamu, uturithishe wanaadamu,

watoto wahitaji mwangaza wako,wakue chini ya uangalizi wako,

utiifu uwafunze mkija kuwa wazee vijana wenu waje wawatunze,

mwanamke,leo ni siku yako,
kaa zako tu kitako upate kula rosti ya Sato,

tuwe na mioyo yenye amani,ni kama tumeshukiwa na upako,

kila kijana kwako ni kama mwanako,

waume tunakosea tunapojidai vidume,
kuwaita wanawake wetu magume gume,

manyumbani kwetu tunajivika ufalme,
kama vile haitoshi tunajifanya mitume,

makazini tunapelekeshwa na waajiri mfano wa n'gombe mazizini,

tuludipo nyumbani tunakuwa visirani kama tumekalia pini,

wake zetu twawakosea adabu,
kwa ujuha wetu tunawapa adhabu,

yanini tunawapatia taabu,
wanawake wetu waliojaa thawabu,

twawakwaza wakati tunajua jawabu,

tuwapende na kuwaheshimu wanawake wote,
sio tu kuwapiga piga kama waume wanaotokea kwa kina Bhoke.

-Kyomushula.

No comments:

Post a Comment