Wednesday, July 4, 2012

"ViJANA NA UJANA"-Sehemu ya Kwanza “Makundi”


"Vijana na Ujana"
Niliposikia wahenga wanasema "Ujana ni maji ya moto" nilipata wakati mgumu sana kuwaelewa wanamaanisha nini kuhusu msemo huu, nikajaribu kuuchambua ili nijue lengo lake ni nini hasa. Nilianza kwa kuigawa hii sentensi katika aina za maneno:-

 Ujana/ni/maji/ya/moto,
 nikapata nomino mbili ( Maji, Moto)..
viunganishi viwili (ni, ya)..
vielezi vitatu Ujana kielezi cha namna/wakati, (ni maji) na (ya moto) vielezi hali.

Ninakajaribu kulichanganua kwa kuandika

(ujana ni maji):- kwa ninavyoyafahamu maji ni kitu kilicho katika hali ya kimiminika, yanaweza kua katika hali ya baridi au ya moto.

halafu nikapata tena

 (Maji ya moto):- ikimaanisha kimiminika kilicho katika hali ya moto au joto kubwa sana, ikimaanisha yamechemka na yaliyo na hatari kama hayatatumika katika hali iliyokusudiwa.

 Nikaamua kutoa (Maji) na (ya)

nikapata (Ujana ni Moto):- ikimaanisha kitu kilicho katika hali ya kuunguza ama kuungua, ambacho ni hatari kwa kuimbe kama hakitatumika katika kusudio lililotarajiwa.

 Mwisho wa kuchanganua nikaamua kuliunganisha tena na kupata msemo wa mwanzo wa wahenga ambao ni:-

“Ujana ni maji ya moto”

 Kwa maana ya kua maji ya moto ambayo ni ujana mtu akifikia katika hatua hiyo basi atakua yuko kwenye hatari ya kuungua muda wowote na madhara ya yake yakadumu kwa muda mrefu. Nikajiuliza kama ujana ni maji ya moto basi ukiwa bado mtoto ni maji ambayo yaliyowekwa kwenye jiko au? na Je! ukiwa Mzee ni maji yaliyopoa au?. Hapo sikupata majibu ila kwa ninavyojua kabla ya umoto ni ubaridi na baada ya umoto ni kupoa tena na kua baridi. Ila nikagundua kua Ujana ni maji na pia ni moto: unaweza ukazama au ukaungua, unaweza ukawaka kisha ukazima kwa maji. Hatimaye nikapata hitimisho la kua Ujana ni muunganiko wa hatari nyingi zinazofananisha na maji na moto au maji ya moto, na katika msemo huu lengo ni kuwakumbusha wale walio katika hali hiyo ya Ujana kuongeza umakini kwani wameafananishwa na mtu aliye karibu na maji ya moto ambapo asipokua muangalifu na makini basi  mtu huyu anaweza kuungua wakati wowote na maji hayo.


Ujana = Maji + Moto


Makala hii ni maalumu kwa vijana wenzangu ambao kwa pamoja tuko karibu na maji ya moto ambayo tunayachezea kila wakati pasipo kujua kua yanaweza kutuunguza na pia tunachezea moto pasipo kujua twaweza kuungua wakati wowote.

Ukitazama maandiko mengi ya kidini yanawasihi na kuwaasa vijana wawe karibu na m/mungu ili waweze kupita usalama katika kipindi hiki kigumu, ambacho kwa vijana wao hawaoni kama ni kigumu, ila kwa wale vijana walio makini na wenye malengo na upeo wa kuona mbali watakua wamenielewa na watakua wameziona hatari hiza zinazowakabili na wanajifunza kwa namna wanavyokabiliana nazo.

Ningependa kuwagawa vijana hawa walio katika hatari hizi makundi matatu..

                      i.        Usijaribu/sintojaribu- sintoingia (excellent and good)- vizuri sana na vizuri
                     ii.        Najaribu/Jaribu kisha ntaacha- ingiakisha toka (Good and bad)- vizuri na vibaya
                   iii.        Nimejaribu nimeshindwa kuacha- ingia kisha shindwa kutoka (bad and worse)-vibaya  na vibaya sana

                           I.      Vizuri na vizuri sana (sintojaribu,sintoharibu,sintoingia)

Kundi hili ni la wale vijana wasiopenda kujaribu vitu venye kuhatarisha, kundi lililo karibu na maji ya moto na lililo makini kwani linajitambua kua maji haya ni ya moto na yanaweza kuwaunguza wakati wowote, kundi hili ni bora na halipendi kuutumia Ujana wao kwa mambo yasiyo  na faida katika maisha yao ya baadae.

Kundi hili katika makundi ya vijana ni bora kwani huwa linachanganua na kuchambua kabla ya kufanya maamuzi na huwa sio kundi la watu wa kukurupuka. Huwa wanaonekana kama ni watu waliopitwa na wakati kwa vijana walio makundi ya chini (waliojaribu). Kundi hili huheshimika na hujiheshimu, halikubaliani na usemi wa “najifunza/ntajifunza kutokana na makosa”.

Ni kundi la watu wenye msimamamo na wanaojua ni nini wanachofanya, wengi wao hujitenga na makundi ya waliojaribu kwakua hawataki washawishike katika kujaribu.

Ni kundi lisilo na tamaa ya kutaka kujua ni hatari gani itakayotokea na hata kama litajaribu litaishia kutaka kufanya lakini likazishinda nafsi zao na fikra zao kwa pamoja.

 Pia ni kundi lisilokubaliana na usemi kua “nitaomba msamaha kwakua nitakosea”, ila huomba msamaha hata kama hawajakosea. Hujihisi ni wakosefu ingawa sio wenye kuendekeza makosa.

Kundi hili pia hushawishika ila ni kundi gumu katika kufanya maamuzi katika yakufanya kwa kujaribu chenye kuhatarisha, hivyo wanaowashawishi hukata tamaa na kuwaacha kua kundi lenye msimamo.

Kundi hili lina vijana wachache sana, kwani wengi wao huishia kwenye kundi la nimejaribu nikatoka.

Changamoyo wanazokutana nazo:-
“Uzeeni utakuja kufanya yale ambayo haukufanya wakati wa Ujana”. Sijawahi kuuthibitisha huu usemi kwa upande wangu ila kwa walio wengi walojaribu huutimia huu usemi ili kuwashawishi ambao bado hawajajaribu waingie katika kundi lao kwa kujaribu kwani watakuja kuchezea matope wakiwa watu wazima, nadhani hii ni kauli ya waliojaribu na ambao hawataki kuona aliye bora kuliko wao ambaye hajajaribu.

“Hakuna aliyebora ila kuna walio karibu na ubora” kundi hili kama hawata jaribu basi wanaweza kuwa wabora katika kundi la vijana wenzao, na pia kundi hili huwa na uoga wa kujulikana kwamba hawajawahi kujaribu, hivyo wanachokifanya huwa ni kuongea sana kuhusu wao kua wameshajaribu ili wasionekane wadhaifu kwa waliojaribu, ingawa kuna ambao hawajawahi kujaribu na huwa majasiri katika kusema kua hawajawahi na hawatajaribu. Hawa ndio wazuri sana na kwa wale wanaoficha hao ni wazuri tuu.

Ukweli wa kundi hili:-
Kwa walio katika kundi hili ningependa wawe wakweli kwa nafsi zao, kwani wanaweza kujificha wanapofanya na wanaweza kudanganya kwamba hawajawahi kufanya ila ukweli ukabaki ndani ya nafsi zao kua wamefanya sana kuliko waliojaribu kufanya. Wanaweza wakaamua kuonekana wabora lakini sio wabora kwa nafsi zao. Ukweli ni kwamba lazima kuna waliojaribu kisha wakomba msahamaha. Hivi ni kweli haujawahi kuiba? haujawahi kusema uongo? na haujawahi kutamani kisicho chako? Hajawahu kudhulumu? Je kula riba? Haujatoa ahadi ya uongo?. Ni kweli kwamba hakuna aliye bora ila kunawalio karibu na ubora. Usichezee matope kama hautaki kuchafuaka kwakua unajua maji na sabuni yapo utajisafisha..Je! kama haviko utafanyaje? Kumkichwa ni wewe!

Ushauri wangu kwa kundi hili:-
Akili kumkichwa ni kwa kichwa chako wewe, “aliyefanya ana tofauti kubwa sana na ambaye hajafanya, ila ambaye hajafanya akifanya tu atakua yuko sawa na aliyefanya, na aliyefanya hawezi kujirudisha ili awe sawa na ambaye hajafanya” hivyo kwa wewe ambaye haujajaribu chochote chenye kuhatarisha basi usijaribu chenye kuhatarisha kwani utakua sawa na aliye katika hatari. Usikubali ukashawishika kwa maneno matamu ya aliye katika hatari. Ila kwakua kumkichwa ni wewe kumbuka kutumia Akili yako katika kuamua lakufanya kabla ya kufanya. Majaribo mengine ni yenye kuhatarisha, unaweza ukajukuta kwenye hatari kubwa kuliko yule aliyejaribu kwakua alijaribu kwa umakini wewe ukajikuta umevamia bila tahadhari ya kujua mchezo unanendaje. Soma mchezo kabla haujaomba sub(haujaingia uwanjanikuucheza...

usikose kusoma sehemu yaPili ili ujue kundi la pili la "nimejaribu kisha nikaacha" likoje?...je wewe uko kundi gani?itaendelea...

No comments:

Post a Comment