Tuesday, July 10, 2012

"ViJANA NA UJANA"-Sehemu ya pili (Vizuri na Vibaya)


Amka, Elimika, Imarisha, Okoa, Unganisha

II.    Vizuri na vibaya (Najaribu/Jaribu kisha nitaacha- ingia kisha toka)
 
                  Kundi hili ni la wale vijana wanaopenda kujaribu vitu vyenye kuhatarisha, kundi lililo karibu na maji ya moto na lililo makini kwani linajitambua kua maji haya ni ya moto na yanaweza kuwaunguza wakati wowote, kundi hili liko karibu sana na bora wakati wakutaka toba na hapenda kuutumia Ujana wao kwa mambo ya kujaribu ili kujua kipi chenye kufaa na kipi kisichofaa kwa manufaa ya baadae ya maisha yao.

Hufikiria kua kama wakikosea wataomba tu msamaha, kwakua wanajua watasamehewa.

Kundi hili katika makundi ya vijana huwa linaonekana bora kwakua kundi la juu la wasiojaribu huwa halionekani kabisa kwani huwa wanajificha au ni wachache.

Pia halionekani kwani katika kundi hili kuna makundi tofauti kutokana na aina ya kitu kijana alichoamua kukijaribu. Kuna makundi ndani ya makundi, kuna waliojaribu hiki na wasiotaka kujaribu kile, kuna waliojaribu kile na wasiotaka kujaribu hiki. Huwa ni kundi la kufundishana, kuonyana, kushawishiana na kutahadharishana kuwa acha hiki jaribu kile acha kile jaribu hiki

mfano: “rafiki yangu uongo sio mzuri, acha uongo” na rafiki yake atamwambia “rafiki yangu acha wizi, wizi sio mzuri”. Wote wako katika hatari ila hatari zinazotifautiana. Na wengine wataonyana kwa kushawishiana “kuliko uibe bora udanganye” huku mwenzake atamwabia “kuliko udanganye bora uibe”.kumkichwa ni wewe!

Kundi hili ni la wale waliojaribu kisha wakaacha walichokifanya kwa kuona hatari zake. Kundi hili huwa linawafunza wenye kutaka kujaribu kua sio vizuri kuingia humu, wengi wa vijana walio katika kundi hili hujikuta wameshikilia kitu kimoja kama ndio kinachowasaidia katika kufanya mambo yao yaende sawa, namaanisha pasipo kurudia tena anachokifanya hataweza kuendelea, ila ni kundi ambalo hufika mahali na kusema basi nimechoka kua mtumwa wakudanganya, nimechoka kudhulumu, nimechoka na wizi, nimechoka na kuwaumiza marafiki zangu.

 Changamoyo wanazokutana nazo:-
“wakati ni ukuta” baadhi ya watu kundi hili hukutana na changamoto ya muda kwani hujikuta wanajaribua wakati muda wao wakujaribu umeshapita. Hujikuta bado wanaendelea kuchezea matope ukubwani.

“I was young and foolish” “nilikua mdogo na mjinga” Baadhi yao hujikuta ni wenye kukosea na huishia kujilaumu kwanini walifanya na kujaribu pasipokuangalia ni yapi matokeo ya wanachotaka kujaribu/kujifanya. Huwa wanahatarisha maisha yao kipindi hiki cha maji ya moto na pale yanapopoa huishia kusema nilikua mdogo na mjinga, sikujua hatari iliyokua mbele yangu, kwakua nilifurahia nilichokua nakifanya.

“Follow your heart” “fuata moyo wako” kundi hili hupenda kufuata moyo unavyotaka, moyo huu kwa makala hii ni “nafsi”, nikimaanisha kufuta nafsi yako vile inataka hata kama ni kitu kitakacho hatarisha maisha yako. Eti kwakua nafsi imetaka uweke kidole kwenye moto wewe weka tu kwakua unafanya vile nafsi yako inataka.

“Have fun life is short” “furahi maisha ni mafupi” kundi hili pia hujikita katika wakati mgumu kwakushindwa kwao kuelewa baadhi ya maneno yanamaanisha nini. Inaposemwa kua furahia maisha haimanishi hatarisha maisha eti kwakua ni mafupi. Kundi hili huishia kujaribu kila kitu, na mwishowe pale wanapo poa wanakosa cha kufanya kwakua wameshafanya kila kitu, kinachofuata ni ugomvi na mwenzako, kwakua mlifanya kabla ya wakati.

“Mbona nani hii alifanya/anafanya” kuna hii kauli ya kujitetea kua mbona Yule anafanya na hajapata madhara yoyote, mbona Yule alijaribu na hajaumia?. Kundi la kutazama nani kafanya nini na mimi nifanye nini, lakini bila kujua kwanini Yule kafanya vile na kwanini yeye hajapata madhara au hajakamatwa.
 

Kuna hadithi moja ya mtu alienda kuiba kisha wakati anaondoka akadondosha kitu, kelele zikasikika na mwenye nyumba akaamka kauliza nani?, jamaa akajibu “nyaaauuu”. Mwenye nyumba akasema kumbe nyau kisha akapuuzia. Yule mwizi akaondoka na vitu na kwenda kumhadithia mwenzake. Mwenzake alivyosikia vile naye akaenda kuiba kwenye nyumba ile ile, nae wakati anaondoka bahati mbaya akadondosha sufuria ikatoa kelele mwenye nyumba akauliza nani? Yule mwizi wa pili akajibu “mimi nyau”, mwenye nyumba akamkamata na kumpatia kichapo cha paka mwizi. 

Hivyo tusijaribu vyenye kuhatarisha kwakua Yule kajaribu, kumbukeni ya kwamba tunatofautina kiakili, kiujuzi, busara hekima na heshima. Usije ukajikuta wewe umeshindwa lakini mwezako kaweza kisha ubaki unajilaumu “why me?”

Ukweli kuhusu kundi hili:-
Ni kundi lililo katika hatari kubwa sana kwani haliamini kua hauwezi kuacha kuajaribu. Ni kundi lenye kubeba vijana wengi wa sasa na wengi wao hushindwa kujimudu na huishia katika kundi la nimejaribu nimeshindwa kuacha.


Kundi hili pia linaona ni ufahari kujua vitu vingi vyenye kuhatarisha, na huwaona ambao hawajajaribu kua ni watu waliopitwa na wakati. Ni kundi lisilo bora mbele ya aliyobora ila wao hujiona ni wabora kuliko aliye bora.
 

Kundi hili hujisahau na walio wengi wao hukumbuka shuka wakati jua ndio linachomoza.

Kundi hili huwa na malengo mazuri ila wengi wao hishia kusema nilifikiriaga kuafanya ila nanihi ndio alisababisha nikaacha, halipendi pia kuchukua mzigo wa lawama wa walio yafanya, hupenda kuwabebesha lawama wenzao kwa makosa yao.


Kundi hili hupenda kuona hakuna aliye mbora kushinda wao, hivyo huja na mbinu mbalimbali za namna ya kuwashawishi ambao hawajajaribu waingie katika kundi lao. 


Kundi hili huwafanya walio wema wajione hawana maana na wasio wema wenye maana. 


Kwa walio katika kundi hili huwa wanaamini ipo siku watatoka katika hali ya kujaribu walioamua kuingia, hujikuta wanashinda kutoka hatimaye kudondokea katika kundi la tatu la jaribu kisha shindwa kutoka.


Ushauri wangu kwa kundi hili:-
Kwa minavyojua maisha yakikaribia kifo furaha huwa kubwa, mfano ni mtu anayeendesha gari kwa kasi hujisikia furaha kwakua yuko karibu na kifo na huwa hajitambui kuwa yuko karibu na kifo kwakua furaha hiyo humpumbaza.

Kwa maoni yangu juu ya mienendo ya watu wa kundi hili ni kwamba itafika kipindi wenye makosa watathaminiwa kuliko wale wema walio karibu na m/mungu wao. Kwa hali ilivyo sasa wale wenye kufanya mambo ya ajabu na yenye kuhatirisha kizazi cha sasa na cha baadae wanaheshimika na kuongelewa kana kwama ni mfano mzuri kwa kuigwa najamii.

Kipindi hiki ni  kibaya sana kwani wale walio wema na wenye malengo mazuri na jamii katika kuamsha, kuelimisha, kuimarisha, kuokoa na kuunganisha hawathaminiki katika jamii na hawapewi nafasi ya kuifikia jamii, ila kwa wale wenye kuhatarisha, kuathiri, kupotosha na kuangamiza jamii ndio wanaopea nafasi ya kuifikia jamii tena kwa haraka sana. Na pale mtu anapoona kitu hicho chenye hatari na jamii hukifurahia na kisha kukisambaza kwa marafiki zake kwa ufahari na kisha kitu hicho kuishia kuiathiri jamii nzima.

Sasa ningependa kulishauri kundi hili kua unapopanda changarawe hata ukapalilia vipi utaishia kuvuna changarawe, utakapopanda mahindi na kisha ukayapalia vizuri basi utavuna kilicho bora kwa faida yako na jamii yako.


Tusiwe watu wakuharibu vilivyo bora kwa kuviua vikiwa vichanga, tusiwe watu wa kupalilia visivyobora kwetu na kwa jamii zetu, tutambue ya kwamba mti  bora hutoa matunda yaliyo bora. Kumbuka ya kua kumkichwa ni wewe!

Kwa kua walio katika kundi hili huwa wanaamini ipo siku watatoka, baadi yao hufanikiwa ila kuna ambao hujikuta wanashindwa kutoka na huishia kudondokea katika kundi la tatu la jaribu shindwa kutoka.


Itaendelea....usikose makala hii sehemu ya tatu ya "Jaribu shindwa kutoka"..je unajua nini kinasababisha?...usisite kurudi tena hapa..kumkichwa ni wewe!

No comments:

Post a Comment