Saturday, January 8, 2011

KUKATAA UHALiSiA, NDiVYO TULiVYO




 1.Ukweli ni sumu-Hatupendi kuongea ukweli wala kusikia mtu akiongea ukweli.
 2.Lawama-ni wingi wa lawama,tunapenda kuwalaumu watu hata kwa makosa tuliyoyafanya sisi wenyewe.
 3.Sio wakosaji-tabia ya mwanadamu ni kukosea na kujirekebisha pale anapokosea lakini sisi tunakataa tabia hiyo kwamba sisi sio wakosaji ila yeye na wao, kumbuka hata yeye na wao pia sio wakosaji.
 4.Wajuaji ndo sisi-kila jambo litakalotokea ama kuongelewa sisi tunalijua vizuri sana, utatueleza nini sisi tunalijua, kwakua hatupendi kuongea ukweli basi sisi tunajua  kila kitu.
 5.Kizuri kwangu-kila litakalofanyika lizuri au kila kilichofanywa vizuri kiwe ni zao la kwangu mimi na sio wao au yeye, pia kitu kizuri au jambo zuri litokee kwangu na sio kwako.
 6.Wakurekebishwa ni wewe sio mimi-kwa kua mimi sio mkosaji ni wewe basi hata jambo litakalotendeka wakurekebishwa ni wewe sio mimi, hatupendi kurekebishwa.
 7.Uoga wa kukosea kwa kujaribu- ni kweli hatutaendelea kama hatutojaribu, hatutojaribu kwakua tuna woga wa kukosea, hivyo ili tujaribu na tuendelee, tusiwe na woga wa kukosea kwa kujaribu.
 8.Tamaa-Tunatamaa kwa vitu tusivyokuanavyo kwa kusahau kuwa na shukrani kwa tulivyokuanavyo, ni kweli tumeumbwa na tamaa ili tufikie malengo ila namna tunavyotumia tamaa zetu, kwa uchanya tutafika ila kwa uhasi hatutofika.
 9.Hatupendi kuongozwa- kwa kua ni wajuaji basi hatupendi kuongozwa, pia kwa kua sio wakosaji basi hatupendi kuongozwa ndio maana kukawekwa sheria za kutuongoza, ni kweli zilitungwa baada ya kugundulika ndivyo tulivyo.
10.Sifa- kama hutanipa sifa basi sitakusaidia, kwa kutamani tusivyokuanavyo, tunatamani vya aliyetuumba, sifa zake, je ukisifiwa nini kinaongezeka...ujinga huo.
11.Tuna akili lakini za kijinga-uwezo wa kuchambua jambo ili kuweza kulijua na kupata uamuzi utakaokua sahihi ili kukabiliana na jambo kwetu ni tatizo. Kila binadamu ana ujuzi alioupata kutokana na maisha aliyoishi, na ndipo akili na tabia za binadamu huyo zilipoanzia. 
12.Uvivu wa kujua- ili ukamilike na kuweza kukabili maisha ya sasa lazima tuwe na ujuzi au elimu ya kitu/jambo fulani, lakini sisi ni wagumu kujifunza kwakua ni wajuaji na sio wakosaji, tunajiona tunajua kila kitu kumbe hatujui chochote.
13.Umaarufu-nani asiyependa kujulikana, tunapenda kujulikana na kila mtu kwakua tunatamaa  ya kupata Sifa za aliyetuumba, na pia tunatamaa na tusivyokuanavyo.
14.Ubinafsi-mimi kwanza ndo wewe, kizuri kwangu, sifa zangu uamaarufu wangu, wewe huna chako labda vibaya vyote vilivyobaki ndio vyako wewe.
15.Kukataa uhalisia ndivyo tulivyo sisi wanadamu, ndo maana kuna jambo kama kukosea na kupata, ukikubali uhalisia utaishi maisha yenye uhuru, wewe soma kwa umakini utaona uhalisia kwamba kila jambo nililoliandika na kilichambua linamtegemea mwenzake na pia kila kipengele nilichokigusa utakua unacho au umeshakifanya na kama ukikana basi ndo Mwanzo wa kukataa UHALiSiA NA NDiVYO ULiVYO…….KUMKiCHWA ni wewe……..

KajiAbeid..August 12, 2010

No comments:

Post a Comment