Fikra hizi ni nyeupe, ni kwa weupe na weusi, fikra hizi pia ni nyeusi, nyeusi kwa weusi na weupe. Mweupe hawezi kuwa na fikra nyeusi zakumkomboa mweusi. Ingawa mweusi kwa fikra nyeusi anaweza kumsaidia mweupe. Ni jukumu la mweusi kujikomboa mwenyewe kwa fikra nyeusi za utu mweusi tokea uzao wake mweusi, asitegemee mweupe atakuja na mbinu nyeupe kumkomboa mweusi. Asilia yako na uhalisia wako ndivyo vitakavyo kukomboa. Usiwaige weupe kwa kujaribu kuwa mweupe. Bali shindana na mweupe panapo mwanga mweupe. Usiwatukuze weupe kwakua wamefanikiwa kwa fikra zao nyeupe kwani weupe wengi wanatumia fikra nyeusi kuwatumikisha weusi. Mweusi pia anaweza kufanikiwa kwa fikra zake nyeusi panapo weupe na weusi, kwani hakuna kisichofanikiwa panapo matumaini.
Elewa ya kwamba kama mweusi hawezi kuwa na fikra nyeusi za kumkomboa mweupe, sasa kivipi mweupe awe na fikra nyeupe ili amkomboe mweusi. Tazama vivuli hivi, mweupe ni mweusi panapo weupe na mweusi ni mweupe panapo weusi. Pia mweupe huwa mweusi panapo weusi japo ni mweupe lakini atabadilika na kuwa mweusi. Na mweusi huwa mweupe panapo weupe ingawa ni mweusi. Mweusi kutimiza matakwa ya mweupe ni tabia ya mweusi na ni kawaida ya mweupe kumtumia mweusi kwanza. Ili pale mweusi atakapotimiza matakwa ya mweupe ndipo mweupe atatimiza matakwa ya mweusi.
Kuna kamchezo kaweupe kuwatumia weusi, na weusi kuwatumikia weupe bila weusi kujua kuna kadoa keupe panapo weusi ambapo ukikagundua unaweza kumfanya mweupe akakutumikia kwa fikra nyeupe na nyeusi, hapo ndipo ujanja wa fikra nyeupe panapo weusi unapozidia, kuwaficha weusi panapo weupe. Tazama weusi wanapowatumikia weupe kwa fikra nyeusi, eti ndio ujanja wa mweusi panapo weupe ,ingawa weupe huwa wepesi kugundua kamchezo haka keusi panapo weupe. Mweusi analala panapo weupe, anaamka panapo weusi, mweupe anaamka panapo weusi na anaamka pia panapo weupe. Lini watakua sawa, siku mweusi akiamka panapo weupe atakuta mwepe alishaamka siku nyingi kwakua alishazoea kumtumikia mweupe panapo weusi.
Katika mchezo wowote huwa kuna mbinu zinatumika, mmoja kumzidi mwenzake ni jambo la kawaida panapo mchezo, sababu kila mmoja anataka matakwa yake yatimie panapo mahitaji baina ya pande mbili. Je! mweusi ametimiza matakwa yake ama anatumiwa tu na weupe, na kivipi mweusi ataimiza matakwa yake kama atakua anamtukuza na kumtumikia mweupe. Mweusi elewa ya kwamba: Utapomtukuza ujue utamuogopa, kama utakapomuogopa ujue utamtumikia, na utakapomtumikia utakubali kila atakachokisema. Ukikubali kila atakachokisema utakua mtumwa wa vitendo, ukiwa mtumwa wa vitendo inapelekea kuwa mtumwa wa kifikra. Mwishowe utaishia kuwa mtumwa mweusi panapo weupe. Ni bora uwe mtumwa mweusi panapo weusi kwa wakati mweusi, kuliko mtumwa mweusi panapo weupe kwa wakati mweusi. Utaonekana na kujiletea matatizo panapo weusi. Kwa weusi utakuwa umewadhalilisha kwani umeshindwa kusoma nyakati, na kwa weupe itakua faraja kwao kwani walikutafuta muda mrefu panapo weusi.
Mweusi amka panapo weupe, mweusi acha kumsubiria mweupe ashuke, mweupe halali panapo weupe wala panapo weusi. Mweusi chapa kazi panapo weupe na panapo weusi. Usikubali kuachwa na mwanga mweupe wa jua, weusi wa giza hautakusaidia panapo mapambano ya wakati mweupe. Weupe wa kibatari panapo giza hautakusaidia katika mapambano. Amka mapema kabla wakati mweupe haujakuacha, una nguvu na akili nyingi ndani yako, acha kujidunisha kuwa hauwezi, hakuna asiyeweza kama ataweka mipango thabiti na kuifanyia kazi panapo mwanga mweupe, weka mikakati ya wakati weupe na weusi mapema. Ingawa saa inazunguka na kurudi ila muda ukikuacha hautakurudia tena. Muda ndio huu, wakati ndio huu, acha fikra za jua likizama nitafanya kesho, acha fikra za kesho ikifika nitamalizi ya leo. Unapolala wakati mweupe ni kama unapiga teke fuko la dhahabu. Amka kwakuona kuwa weupe ni Jua na weusi ni Giza. Je Fikra nyeupe na nyeusi ni zipi? KUMKiCHWA Ni WEWE!
Kajiabeid©2011
No comments:
Post a Comment