Wednesday, April 25, 2012

(Coming Soon)..Kinakuja kipya kupitia Kumkichwa Blog...(It's All About Kumkichwa)

kinakuja...kinakuja...je unataka kujua nini kinakuja?....
     
       Makala hii ni maalumu kwa wote wapendao mabadiliko yao wenyewe kabla ya kuwabadilisha walio karibu yao, hii pia ni maalumu kwa wote wapendao ukweli na wapendao kupitia, kusoma, na kujua nini kinaendela katika fikra za wanajamii wetu kwa maandiko yaliyo katika blogu yetu ya jamii ya Kumkichwa. Imeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuwakumbusha na kuwashukuru wale wote walioshirikiana nasi kwa njia moja au nyingine kuandika makala zetu, picha pamoja na muziki wao na kwa wale waliotoa maoni yao nini kifanyike, kipunguzwe ili kumkichwa iweze kuwafika walio wengi. Pia bila kuwasahau wote waliochangia kuandika makala zao mbalimbali kwa moyo mkunjufu ili kuonesha uhalisia wa maisha yao kwa kutaja majina yao hata bila kutaja majina yao kwani mchango wao mkubwa umetuweza kuwafikia wengi. Tunapenda kuchua nafasi hii pia kuwashukuru wote wenye nia nzuri na Kumkichwa na kwa wale wenye nia tofauti na hii tunawaombea wafunguke penye ukweli ili watambue kua vita ngumu sio ile ya kushindana na nafsi na fikra za mwenzako bali ni kushindana nafsi yako na fikra zako. Tunawashukuru wote kwani ushirikiano wenu katika kutujenga na katika kutusukuma umetupatia changamoto zilizotujenga na zilizotuimarisha mpaka hapa tulipofikia. Hivyo umuhimu wenu katika harakati hizi tunautambua sana na mbarikiwe sana.

         Kwa muda mrefu tulikua kimya kwa upande wa makala za kiswahili pamoja na za lugha ya kigeni ya kiingereza. Kukaa kwetu kimya kulikua kwa manufaa kwani tumeweza kujua hasa ni kivipi tutaweza kwa pamoja kulikomboa jahazi letu linalotaka kuzama kwa kutokujua kwetu ni wapi tulipotoka, wapi tulipo na wapi tunapotaka tufike. Hivyo tungependa kuwajuza kuwa kuna kitu kitakuja hivi karibuni, kitahusisha nyanja mbalimbali za jamii yetu ya Kitanzania, mfumo wetu utakua ule ule kwa njia ya makala na kwa njia ya kuwatambulisha wale wote wanaoihusu jamii yetu ya kitanzania kwa njia ya uchanya ama kwa maana nyingine ni kukosoa kwa kujenga kwa njia ya uchanganuzi wa kina kwa kile kilichotokea na kinachoendelea, kinachofanyika na kinachotaka kutokea katika jamii yetu ya Kitanzania.

        Kingine kipya ni kuhusu vijana, lengo kuu la kuundwa kwa kumkichwa kama kioo cha jamii ni kusimama na vijana. Na kinachokuja ni kwa ajili ya vijana wa Kitanzania, lengo likiwa ni lilelile la kuchanganya akili za kuzaliwa na kile tunachoambiwa. Kumkichwa ni ya vijana na kumkichwa itakua mstari wa mbele kusimama na vijana. Wewe kama kijana utatakiwa usimame kama wewe kwa uhalisia wako ili kuweza kuwa mmoja kati wa wanakumkichwa waliotayari kusimama kwa ajili ya kufanikisha na kufikia kile kilichodhamiriwa ambacho ndicho kinachokuja. Ukitambua hilo basi ujijue tayari umeshakua mjumbe wa kumkichwa. Kwani Kumkichwa ni ya kila mtu haina haja ya kusema unajiunga bali ujumbe ukikufikia basi ujue umeshahusika katika harakati hizi.

        Kwa kua ujumbe wetu umewafikia wengi na tumepata masikio yakutusikiliza na macho na ubongo wa kusoma na kuelewa nini hasa kinachofanyika katika harakati hizi za kuwakomboa vijana wa kitanzania popote walipo kwa njia ya mtandao na kwa kuwafikia mahali walipo, Kumkichwa inapenda kuwapa nafasi wapenzi na wasomaji wetu kuchangia kwa kuandika makala zao kisha kuzituma kwa email yetu ili na maoni yao yaweze kuwafikia walengwa wote. Tunaimani ya kuwa tukishirikana kwa pamoja tutaweza, hivyo tusisite kutoa tulivyonavyo kwa uoga bali tuvitoe na tujitolee kwa ujasiri wa kuushinda uoga. Ni dhahiri ya kuwa tokea tumeanza tuliamini tutaweza, na sasa tunaamini tunaweza kilichobaki ni kutimiza malengo yetu ili tuwe tumeweza kwa pamoja. Popote ulipo na popote utakapolisikia neno KUMKiCHWA basi ujue wewe kama Mtanzania unahusika katika mchakato huu wa kujikomboa kifikra kwa kutumia uwezo wetu tulionao na kwa kuwaonesha njia kwa kuwashika mkono wale waliopoteza tumaini la kuweza na kufanikisha.

        Kwa ujumla mwanzo wowote huwa mgumu kiasi cha kutaka kukata tamaa kwamba hautaweza ila kama ua linaweza kuvumilia mvua kubwa na jua kali bila ya kujibeba ili kujificha kwakua ndio uhalisia wa ukuaji wake kivipi sisi tujifiche na tukimbie pale matatizo na changamoto zinapotukabili. Ni dhahiri kwamba tumepita kwenye wakati mgumu ambao kwetu sisi tuliona kama ni sehemu ya ukuaji wetu na hakuna sababu ya kukata tamaa wala ya kutetereaka. Tumekua wavumilivu na wajasiri katika mchakato huu wakutaka kufanikisha yale tuliyoyaanzisha na kuhakikisha tumewafikia wote tulio dhamiria kuwafikia. Kwa hili tunamshukuru mola kwakua ametupitisha katika njia iliyosahihi kwa kutupa uwezo wa kuwafundisha na kusema yaliyo ndani yetu bila uoga wowote. Nanukuu moja ya maneno ya Kumkichwa..."uoga uko ndani ya kila mtu ila unatofautina kwakua unategemeana na nani aliyeupa nafasi ndani ya nafsi yake na fikra zake mpaka akawa mwoga kwa kuingiwa na woga"

        Kwa ujumla tumepokea maoni na ushauri tofauti tofauti kutoka kwa mashabiki, wasomaji, watembeleaji, ndugu, jamaa zetu na marafiki zetu na tunawaahidi katika ujio huu maoni na ushauri mliotupa tutaufanyia kazi na tunatumai mtafurahishwa na ujio huu ilio mbioni kutokea katika blogu yetu hii ya Kumkichwa. Tunawasihi mzidi kuwa karibu nasi kwani hata sisi moja ya lengo letu ni kuwa karibu nanyi ili tutazamane na turekebishane kama kioo. Ukaribu wetu ndio utakaoonesha picha nzuri kwenye kioo hiki cha jamii, msisite wala msitetereke kutukosoa, kuturekebisha na pia kutunyoosha pale mnapoona tunakwenda tofauti na mlivyotarajia. Kwakua hakuna kilicho bora ila kuna vilivyo karibu na ubora nasi tunawasihi tuongozane panapo makosa na tuwekane sawa panapo tofauti. Uwepo wenu ndio uwepo wetu na uwepo wetu ndio mwanzo wa kuwatambua uwepo wenu. Gari letu linategema magurudumu yenu ili liweze kusonga mbele, kwa namna mtakavyozidisha kasi katika mwendo wa kutembelea blogu yetu ndivyo nasi tutakavyozidi kuwafikia mapema..nukuu "ushirikiano ndio chanzo cha maendeleo" Hayati Mwl. J.K Nyerere.

       Shukrani za dhati kwa mola aliyetuweka hai hadi leo, pai kwa kutuwezesha kupata mawazo ya kipekee ya namna ya kuwafika wanajamii wetu, tunakushukuru pia wewe uliyeisoma makala hii na kwa wewe uliowahimiza rafiki na ndugu zako waisome hii..hii ni maalumu kwako na kwetu..wahimize na watumie wengi waisome kadiri ya uwezo wako, tuusambaze ujumbe huu na shukrani hizi kwa wana kumkichwa wote....usisite kuandika maoni, shukrani ama pongezi zako hapa chini...je nini kifanyike?,..nini kisifanyike? ...uamuzi ni wetu...tusiogope kujivunia cha nyumbani kwakua cha wageni sio chakwetu...ubora upo kwa kile tulichonacho kuliko kwa kile tukitoleacho macho kwakua hatunacho..tunajivunia kuwa pamoja katika kumkichwa..wewe je...kumbuka KUMKiCHWA NI WEWE!

No comments:

Post a Comment