Saturday, December 4, 2010

TUPELEKE CHOMBO ANGANi KiFiKRA

   
         Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimebarikiwa utajiri mkubwa sana wa malighafi mbalimbali duniani, katika Afrika ni nchi ambayo ina eneo kubwa kuliko yote na lenye utajiri wa kila aina. Lakini ukiitazama Tanzania kati ramani ya dunia katika maendeleo Tanzania ni moja kati ya nchi zisizo tambulika ingawa zina malighafi za kutosha. Ukiutaja Mlima Kilimanjaro, Mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti pamoja na Ziwa Victoria utakuta kwamba ni majina yanayotambulika sana duniani.
      Waandishi wengi wa mashairi, wa  vitabu na wasanii wa filamu wamepata kujiongezea vipato katika nchi zao kwa kutumia majina ya nchi kama Tanzania, katika baadhi ya vitabu nilivyosoma mfano “Life on the Edge” mwandishi anaelezea hadithi yake alivyokuja kutembelea mbuga za wanyama za Serengeti, na katika filamu mfano ya Jimmy Carey anaelezea nyoka mbalimbali wanaopatikana Tanzania, na katika wimbo wa Nas na Damian Marley wanajivunia lugha ya Kiswahili kwa maneno “habari gani nzuri sana” hii inadhihirisha kua Tanzania inatambulika vizuri katika uso wa dunia kwamba kuna nchi iliyobarikiwa Afrika inaitwa Tanzania.
          Ingawa tumetambulika sasa isiwe tija lengo ni kwamba sisi vijana tuna malengo gani na nchi yetu ya Tanzania, kama vijana ni taifa la kesho! Je vijana wa leo tunalifikiria taifa la kesho? lengo sio kuwasomesha vijana kwamba tujivunie jina la Tanzania bali tujifikirie kama sisi vijana ni taifa la kesho, tufanyenini leo ili kesho tuweze kujivunia kua tulikua vijana wa taifa la leo. Huu ndo wakati wakulisongesha gurudumu la maendeleo katika taifa letu la Tanzania.
      Vijana wengi wa kitanzania hawajui haki zao hii imeonekana ni swala la kawaida, japokua vijana wengi wakitanzania wana akili pamoja na nguvu ila tatizo tumeshakua na mfumo tegemezi wa kimawazo katika  kujiendeleza.
       Kama kijana wa kitanzania akiwa huru kifikra leo Tanzania ya kesho inaweza kupeleka chombo mwezini, nasema hivyo kutokana na nguvu ya kufikiri tuliyonayo katika ubongo ni kubwa mno, tunaweza kuibadilisha dunia vile sisi tunataka kama tukitumia fikra  sahihi, na  kama vijana wa Tanzania tunataka kupeleka chombo angani basi tunaweza kukipeleka ila tunatakiwa tuwe huru kifikra ili tuwe na fikra sahihi katika kutimiza malengo ya taifa la kesho, kama unataka kwenda mahali usipopajua kifkra panakua mbali, ila kama unataka kwenda mahali unapopajua kifkra panakua karibu, sasa vijana mko wapi?
     Tuamkeni tujipange tunataka kwenda wapi, tusiwe wavivu wa kufikiri, Tanzania inabaki kichwa cha mwendawazimu, na sisi tunafurahia kuitwa wendawazimu? usijisemee kua wewe sio mwendawazimu labda kama haukubali misemo ya wahenga kwamba “akioza samaki mmoja, wote wameoza”. Ni wakati wakumtoa samaki aliyeoza na kuwatengeneza wale walio wazima ili waweze kutumika.
          Vijana nalia  na nyie, sisi  ndio tunaweza kuibadilisha Tanzania ya leo ili kesho ikaitwa Tanzania ya Wazalendo wa "next level" kama tunavyoupenda huo usemi. Sisi ndio tunaoweza kuipeleka Tanzania angani kifikra na kimatendo, najua wengi watashindwa kuielewa kauli hii ila ni wewe mwenye uwezo wa kufikiria mbali na ukafika mbali, ni wewe inayeweza kupeleka chombo angani kwa fikra za kimaendeleo ya kwako na taifa lako. Vijana wa Tanzania tunaweza tukiamua, tusipelekwe tu na mfumo nyonyevu wa fikra. Tubadilike sasa. Kumkichwa ni wewe!