Saturday, May 28, 2011

"Kwa Walio Juu na Chini"



Utamu wa Maisha hujitokeza kwakua kuna misukosuko inayotufanya tujitambue kwa mapana na marefu. Mfano wa misukosuko hiyo ni juu na chini, yaani leo uko chini na kesho upo juu,leo umepata kesho umekosa, leo kipo kwako kesho kwa mwenzako. Kamzunguko kanakoashiria uhalisia kwamba mamlaka yakupanga hayapo mikononi mwako. Tazama uhalisia wa usiku na mchana,vinapo pokezana ikifika Asubuhi Jua linachomoza kisha tunapata mwanga wake na ikifika Jioni giza linaingia na tupata mwanga hafifu wa Mwezi kuashiria hauwezi kukosa vyote. Kwenye giza la Usiku unapata mwanga toka kwenye Jua kuashiria urafiki bila chuki. Na ndivyo ilivyo kwenye maisha yetu haya ya kila siku kwa wenye urafiki bila chuki.

Ukikubali kuna kusini pia ukubali uwepo wa kaskazini, iweje utambue uwepo wa mashariki lakini hutaki kutambua uwepo wa magharibi. Jambo la muhimu na la msingi ni kukubali uhalisia katika maisha yako, kama umeona jua linachomoza leo, jitahidi na kesho ulione, ukiliona wakati linazama usihuzunike kwani kuzama kwake leo ndio kuchomoza kwake kesho.

Mwanzo ni mwisho na mwisho ni mwanzo wa mwisho mwingine. Hii ni hesabu ndogo hata mtoto mdogo anaweza kuielewa na kuijibu, kusingekuwepo na giza tusingekua na mwanga mwingi. Kama hakuna giza basi na mwanga usingekuwepo, sababu giza linategemea uwepo wa mwanga, kama maisha na kifo vinavyotegemeana ndio hivyo ilivyo kwa walio juu na walio chini wanavyotegemena.

Aliye juu sikuzote hatamani kwenda chini, na sio kwa mapenzi yake yaliyomfanya awe juu bali mamlaka ya aliyetuumba. Aliye chini ndoto zake ni lini atafika juu, huwa anatamani nae afike juu siku moja. Kiuhalisia ukitazama hakuna anayependa kudhalilika, ingawa kudhalilika kunaendana na kuheshimika. Aliyechini anaona aliye juu anaheshimika, na aliyejuu anaona aliyechini anadhalilika ndio maana hatamani kurudi chini. Ni kweli binadamu haturidhiki na tulivyonavyo, aliye chini anaona hana kitu kwa kujifananisha na aliye juu, aliye juu naye anatamani uhuru wa aliye chini. Hakuna anayetambua fikra za upande wapili wa jani kwamba kuna matatizo.

Milango yote inapofungwa hua kuna milango mingine inafunguliwa katika upeo wa macho na fikra zako, ieleweke milango ni nafasi ya kufanya au kuchukua hatua nyingine tofauti na ile ya ya kwanza ambayo imefungwa, mlango wa kwanza utakoupata uko wazi, wapili ule unaotakiwa ufanye juhudi kuufungua, mingine ni ile utakayoifungua kwa kusaidiwa na watu uliowategemea au usiowategemea, uamuzi ni wako. Tambua uwepo wa njaa na shibe, hata uwe na njaa ya siku sita utakua mlo mara moja tu, kisha utasikia njaa tena baadae, mgawanyiko wa viwili unaosababisha uwili kwa mtu mmoja. Ila utakavyo amua ndivyo fikra zako zitapokupeleka, ukiamua kutafua bila kukata tamaa utapata, kwakua vikwazo vipo kila mahali, unapokitaka kitu ili kuwa nacho lazima ukifahamau kwa undani, mafunzo hayo yanaweza kukujenga ama kukubomoa. Tambua kwamba Waroma hawakuijenga Roma kwa siku moja, ila aliye chini anataka akiamka asubuhi ajikute yuko juu, laa sio hivyo wewe uliye chini, lazima upambane kwanza ndipo atakapo ijenga Roma yako, kwani aliye juu naye ataendelee kuimarisha Roma yake.

Hivyo kwa tuliochini tutafika juu siku moja, na kwa walio juu wanatambua kua ipo siku watashuka chini, ila tusiwasubiri washuke na wala tusiwaombee washuke, sisi tupamabane ili tuondokane na firka za chini, tupiganie kilicho chetu kwa haki, tuvune kilicho jasho letu, kwani ukikubali kuonewa ni sawa na umetenda dhambi. Kwa hiyo tuwafate huko walipo, kama unataka kubaki chini endelea kubaki, lakini kama unataka kwenda juu, unatakiwa ujipange leo, utazama mbele, uweke malengo, kisha uyatekeleze, usiyapuuze na wala usikate tamaa panapo ushindi panapotokea na matatizo vikwazo, kwani matatizo na vikwazo ni sehemu ya mchezo. Inapokua ngumu wewe kua mgumu, jitambue wewe ni nyundo mbele ya jiwe, ligonge tena na tena mpaka livunjike. Lakini zaidi ya yote kumbuka kumkichwa ni wewe!

Abeid kajia ©2011

No comments:

Post a Comment