Saturday, May 28, 2011

"MUDA GANi?"



1.Utasimama kama mwenye haki anayedai chake kwa haki?

2.Utakaoacha kulalamika wakati nguvu akili viko ndani yako?

3.Utatambua ulivyo ni matokeo ya vitu na mambo uliyoyafanya kwa muda uliopita na ndio yanayokufanya uwe hapo ulipo katika muda huu na ni kwa namna gani unatakiwa ufanye mambo kwa muda ingawa haujui ni kwa muda gani.

4.Utakubali kuwa wewe ili uendane na muda wako uliopewa kukamilisha na kufanikisha wajibu wako.

5.Utakao kua chini ukifikiria kupanda juu na muda gani utakua juu na utakumbuka kwa muda gani ulikua chini ili muda wakua juu ukiisha usirudi chini kwa muda usioujua.

6.Utathamini kila kiumbe kilichokujia kwa muda kukamilisha ukurasa wa kitabu chake na chako bila kuwakwaza kwa kutotambua muda gani aliyekuumba atakileta kwako hicho kiumbe.

7.Utakaothamini muda na kwenda nao sambamba bila kupoteza dakika moja yenye uzito wa sekunde sitini.

8.Utakua umejiaandaa kuondoka katika dunia hii na kutarajia mema kwa wema uliyofanya na mabaya kwa baya uliloyafaya.

9.Utakao tambua kwamba maisha ni mtihani unao ufanya kila siku bila ya wewe kujua.

10.Utathamini ulichonacho na kuacha kutumbulia mimacho cha mwenzako kisicho chako.

11.Utagundua kuwa muda gani ni muda huu unaoutumia kufikiria ni muda gani utatenda vilivyo ndani ya Muda gani na kwa muda gani? Kumkichwa ni wewe!

Kajiabeid©2011

No comments:

Post a Comment