Thursday, June 16, 2011
"Kwa miaka 50 ni fikra masikini na sio nchi masikini."
“Umasikini wa fikra ni umasikini mkubwa na hatari sana kuliko umasikini wowote hapa duniani” hii ni kauli ya marehemu Baba wa Taifa. Tokea mwaka kumi na tisa sita na moja mpaka sasa mwaka wa ishirini moja na moja, wimbo wa pili wa taifa umekua "Tanzania, Tanzania ni nchi masikini", lakini kiukweli Tanzania sio nchi masikini, sisi wananchi ndio masikini, tena sio masikini wa vipato, bali masikini wakubwa wa fikra.
Katika kujua/kutambua zuri au baya mtu binafsi aliye na akili timamu ndiye huweza kutiliwa maanani pale anapofanya maamuzi, na maamuzi haya huwa yanafanywa kwa fikra sahihi za mtu huyo na panapotokea mapungufu katika fikra hizo basi ujue hata maamuzi yatakua na mapungufu. Tumekua tukiwalaumu sana watu wengine kwa maamuzi wanayoyafanya wao bila kutambua kua wakulaumiwa sio wao bali ni sisi tuliofanya maamuzi kabla ya kufikiri na kutafakari maneno yao kwa umakini. Kwakua baba wa taifa alishasema "SiASA Ni MCHEZO MCHAFU", sintopenda makala hii ihusishwe na siasa.
Katika fikra zetu kama wanajamii tunatakiwa tuwe ni watu wakufanya maamuzi endelevu yenye vyanzo vyenye uhalisia wa maisha yetu kama watanzania, yawe ni maamuzi ambayo yanaweza kujadiliwa na wanajamii, kukubalika na kisha kufanyiwa kazi na kuleta matokeo endelevu na sio potevu. Hivyo pale tutakapokaa na kuanza kutoa lawama kwa mwingine tujitambue ya kwamba tunakataa uhalisia kwamba wakosaji ni sisi, lakini pale tutakapokaa chini na kutaka kumjua mchawi ni nani, tutaishia kujikamata wenyewe.
Fikra masikini ziko na sisi kwakua tunajihusisha na umasikini ambao hautaki kua karibu na sisi. Nchi yetu sio masikini ila wananchi wake ndio tuna fikra masikini. Hakuna hata siku moja Tanzania itaitwa nchi tajiri kama wananchi wake hatakua na fikra za kitajiri, kwakua fikra masikini zinaleta umasikini, na fikra tajiri zinaleta utajiri. Fikra masikini hizi hazina tofauti na fikra za mrengo wa kushoto ama fikra hasi na pia fikra tajiri ni mrengo wa kulia ama fikra chanya.
Kwa miaka mingi sasa watanzania tumekua ni watu wakukata tamaa na kupoteza malengo kwa kuwa tunajidhania ni masikini, na tukijisahau kwamba kama tukijifikiria kuwa hatuwezi tunajiondolea matumaini ya kutokuweza, je! ni sera ngapi na mipango imekwisha pitishwa bila kufanikiwa?, yote haya yamepotea kama mvuke kwakua hatuna tole la matumaini, tunajiona kwamba hatuwezi, ila kama mtu angetambua umuhimu wa tone moja la maji ya mvua, basi angeheshimu maji ya dimbwi. Tumekua ni watu wakujidharau kana kwamba ni tone moja katika bahari hivyo halitaleta mabadiliko.
Tutambueni umuhimu wetu ndio unaunda kitu, umoja wetu ndio nguvu yetu, sasa kwanini hatutumii mwanga wa jua kuona, tunasubiri mpaka kiza kiingie ndipo tutoe lawama kwa mtengeneza kandili. Tumekua watu tegemezi sana, tunachezea nguvu na mali kazi zetu, tumekua waongeaji sana kuliko kutenda, wengi wa lawama kwa wao na sio kwa sisi, tumekua sio wenye kujifunza tunapofanya makosa. Tazama asiyejua kusoma anajitamba kwamba anajua kusoma, na asiyetaka kurekebishwa. Tazama asiyejua hataki kufundishwa, tazama anayejua anakataa kumfundisha asiyejua. Tunajiona bora kuliko wabora. Tumekua watu wa bora jana, leo sijui itakuaje, leo ikija, kesho mwenyezimungu ndiye atakayeipanga, jamani kesho haifiki kwakua kuna jana, ila leo ipo kila leo.
Sasa twatimiza miaka hamsini kwa teknohama za wenzetu wakati zakwetu twaogopa kuzitoa eti ni za kishamba!, sasa zipi ni za kiofisi ama za kiwanja ama kijanja,ni fikra tu ndizo zinatufanya tijifikirie vibaya, kwanini tunalionea sana shamba, hakuna mjanja wala mshamba katika ubunifu wa kuleta maendeleo, wenzetu mashamba ndio yayofanya teknohama zinaibuka, sisi mashamba yetu tumeeyaacha tunakimbilia mjini kufanya biashara ya kuuza alichotengeneza jirani yetu. Sisi tumekua wanunuzi wa kila kitu, kuanzia kifaa ,elimu ya kutumia, spea, vifaa vya kufungia.Yaani tumetawaliwa kifkra na kusahau kua ukitawaliwa, mkombozi wako ni wewe mwenyewe kujiondoa kwa mtawala huyo. Kuna umuhimu mkubwa sana wa sisi kua wazalishaji kuliko kung’ang’ania kuwa wauzaji na wanunuaji, tunapunguza kipato chetu kwa kununua kuliko kuzalisha.
Ukitazama kwa makini utatambua kwamba sisi sio watumwa katika utumwa ule wa zamani, ila sisi ni watumwa wa kileo wa kifikra, tunatafuta kazi kwa mabwana/watwana ili tuwazalishie malighafi zetu, kisha wanatupa ujira, ujira huo tunaenda kununua tulichokizalisha kwa bwana yule, kesho tena tunarudi kuomba kazi, yaani ni kautumwa kaliko kwenye fikra zetu kwa kuwa tumekua wavivu wa kufikiri na kuunda njia mpya za kujikwamua kiuchumi. Hivi ni kwamba nchi yetu haina wataalamu wakuweza kubuni njia ya kuwapatia ajira vijana? Hata kuwamilikisha mashamba kwa vikundi ni jambo lenye tija, kisha wakishalima serikali iyanunue mazao yao kisha iyapeleke kwenye viwanda au serikali iwatafutie masoko nje ya nchi. Au iwawezeshe kisha vijana watafanya watakavyoona ni sawa kufaanya kwa sera za vikundi vyao.
Watanzania tunaweza kubadili fikra zetu na kisha kuiletea nchi yetu maendeleo. Kuna usemi kwamba “sijafika pale nilipotaka kufika ila ninashukuru hapa nilipofika”, ila kama ndipo hapa tulipo mimi nasema bado kwa sababu kuna wakati hapo nyuma kuna kitu kilienda ndivyo isivyo. Ila kwa miaka hii hamsini ni miaka ya wananchi wenye fikra masikini na sio ya nchi masikini wala ya wananchi masikini. Kumkichwa ni wewe!
Kajiabeid©2011
Tuesday, June 14, 2011
ifm career day
boys in black n purple |
importance of insurance and social protection |
kumkichwa brothers |
kumkichwa signing the guest book |
2nd winners BSc.IRM and BSc.SP |
kumkichwa n his brother Hamiru |
kumkichwa n his homegirl Julieth |
welcome |
kate,chichi n sandra |
Mr. Mpinzile, Mr. Mkisi, Mis Gama n Mr.Kajia Kumkichwa |
Our Guest of Honor Addressing at IFM |
ready to conquer the industry |
( BBF) 1st winner's pic with the guest of Honor |
BSc. IRM n SP 2nd winners |
our babu |
the insurance house |
posing with babu |
Mis Kate ,Mis Gama & Mis Sandra |
Sunday, June 5, 2011
“FiKRA HiZi!!!”
Fikra hizi ni nyeupe, ni kwa weupe na weusi, fikra hizi pia ni nyeusi, nyeusi kwa weusi na weupe. Mweupe hawezi kuwa na fikra nyeusi zakumkomboa mweusi. Ingawa mweusi kwa fikra nyeusi anaweza kumsaidia mweupe. Ni jukumu la mweusi kujikomboa mwenyewe kwa fikra nyeusi za utu mweusi tokea uzao wake mweusi, asitegemee mweupe atakuja na mbinu nyeupe kumkomboa mweusi. Asilia yako na uhalisia wako ndivyo vitakavyo kukomboa. Usiwaige weupe kwa kujaribu kuwa mweupe. Bali shindana na mweupe panapo mwanga mweupe. Usiwatukuze weupe kwakua wamefanikiwa kwa fikra zao nyeupe kwani weupe wengi wanatumia fikra nyeusi kuwatumikisha weusi. Mweusi pia anaweza kufanikiwa kwa fikra zake nyeusi panapo weupe na weusi, kwani hakuna kisichofanikiwa panapo matumaini.
Elewa ya kwamba kama mweusi hawezi kuwa na fikra nyeusi za kumkomboa mweupe, sasa kivipi mweupe awe na fikra nyeupe ili amkomboe mweusi. Tazama vivuli hivi, mweupe ni mweusi panapo weupe na mweusi ni mweupe panapo weusi. Pia mweupe huwa mweusi panapo weusi japo ni mweupe lakini atabadilika na kuwa mweusi. Na mweusi huwa mweupe panapo weupe ingawa ni mweusi. Mweusi kutimiza matakwa ya mweupe ni tabia ya mweusi na ni kawaida ya mweupe kumtumia mweusi kwanza. Ili pale mweusi atakapotimiza matakwa ya mweupe ndipo mweupe atatimiza matakwa ya mweusi.
Kuna kamchezo kaweupe kuwatumia weusi, na weusi kuwatumikia weupe bila weusi kujua kuna kadoa keupe panapo weusi ambapo ukikagundua unaweza kumfanya mweupe akakutumikia kwa fikra nyeupe na nyeusi, hapo ndipo ujanja wa fikra nyeupe panapo weusi unapozidia, kuwaficha weusi panapo weupe. Tazama weusi wanapowatumikia weupe kwa fikra nyeusi, eti ndio ujanja wa mweusi panapo weupe ,ingawa weupe huwa wepesi kugundua kamchezo haka keusi panapo weupe. Mweusi analala panapo weupe, anaamka panapo weusi, mweupe anaamka panapo weusi na anaamka pia panapo weupe. Lini watakua sawa, siku mweusi akiamka panapo weupe atakuta mwepe alishaamka siku nyingi kwakua alishazoea kumtumikia mweupe panapo weusi.
Katika mchezo wowote huwa kuna mbinu zinatumika, mmoja kumzidi mwenzake ni jambo la kawaida panapo mchezo, sababu kila mmoja anataka matakwa yake yatimie panapo mahitaji baina ya pande mbili. Je! mweusi ametimiza matakwa yake ama anatumiwa tu na weupe, na kivipi mweusi ataimiza matakwa yake kama atakua anamtukuza na kumtumikia mweupe. Mweusi elewa ya kwamba: Utapomtukuza ujue utamuogopa, kama utakapomuogopa ujue utamtumikia, na utakapomtumikia utakubali kila atakachokisema. Ukikubali kila atakachokisema utakua mtumwa wa vitendo, ukiwa mtumwa wa vitendo inapelekea kuwa mtumwa wa kifikra. Mwishowe utaishia kuwa mtumwa mweusi panapo weupe. Ni bora uwe mtumwa mweusi panapo weusi kwa wakati mweusi, kuliko mtumwa mweusi panapo weupe kwa wakati mweusi. Utaonekana na kujiletea matatizo panapo weusi. Kwa weusi utakuwa umewadhalilisha kwani umeshindwa kusoma nyakati, na kwa weupe itakua faraja kwao kwani walikutafuta muda mrefu panapo weusi.
Mweusi amka panapo weupe, mweusi acha kumsubiria mweupe ashuke, mweupe halali panapo weupe wala panapo weusi. Mweusi chapa kazi panapo weupe na panapo weusi. Usikubali kuachwa na mwanga mweupe wa jua, weusi wa giza hautakusaidia panapo mapambano ya wakati mweupe. Weupe wa kibatari panapo giza hautakusaidia katika mapambano. Amka mapema kabla wakati mweupe haujakuacha, una nguvu na akili nyingi ndani yako, acha kujidunisha kuwa hauwezi, hakuna asiyeweza kama ataweka mipango thabiti na kuifanyia kazi panapo mwanga mweupe, weka mikakati ya wakati weupe na weusi mapema. Ingawa saa inazunguka na kurudi ila muda ukikuacha hautakurudia tena. Muda ndio huu, wakati ndio huu, acha fikra za jua likizama nitafanya kesho, acha fikra za kesho ikifika nitamalizi ya leo. Unapolala wakati mweupe ni kama unapiga teke fuko la dhahabu. Amka kwakuona kuwa weupe ni Jua na weusi ni Giza. Je Fikra nyeupe na nyeusi ni zipi? KUMKiCHWA Ni WEWE!
Kajiabeid©2011
Subscribe to:
Posts (Atom)