Je! ni wapi tulikosea? |
Tulisali dhambi zilipozidi, ukame ukapotea,
baraka za mvua zilipozidi, mafuriko yakatokea,
maisha yakapotea, Je! ni wapi tulikosea?
Tukajenga kwenye miinuko, wakasema tumekosea,
kila mahali tulipo, alama ya x imekolea,
maisha yanapotea, Je! ni wapi tulikosea?
Pazuri ndio kwao, kicheko kirefu wameotea,
kwetu mabondeni vilio, jamani huku tunaelea,
maisha yanapotea, Je! wapi tumekosea?
Utawasikia hameni mabondeni, kukaa huko mnakosea,
Mara unasikia kaposho haka kadogo jamani, sio vibaya tukikaongezea,
maisha yakapotea, Je! ni wapi tulikosea?
Nakosea bure bila senti, natupwa Jela nikafundishwe,
wamekwapua fuko la vijisent, wanaunda Tume wasafishwe,
maisha yakapotea, Je! ni wapi tumekosea?
Japo hasira zetu ni kali, misaada yenu tutaipokea,
nyie mpini sie makali, sauti ya vuta ikitokea,
maisha yatapotea, Je! ni wapi tutakosea?
Bora maisha niyaonayo, kuliko maisha bora ya ndoto
Za mjomba kama Mpoto, za kudanganywa kama toto,
ninaposema tena kumkichwa ni wewe! Je! utasema nimekosea?
by Abeid Kajia on Thursday, December 29, 2011 at 9:11am ·
No comments:
Post a Comment