Thursday, May 17, 2012

"MTO HUU WENYE MAMBA"

Baada ya kuvuka mto wenye mamba

Mto huu una mamba wengi,

walio na madhara mengi,

wenye kutaka vingi,

vyenye gharama nyingi,

kivipi utafika ng'ambo?

 

Ng'ambo ya mto vizuri vingi,

vyenye manufaa mengi,

kupata vizuri ni kujitolea vingi,

kwa umoja huu wa kutafuta wingi,

kivipi utafika ngambo? 

 

Silaha uliyonayo kigingi,

maswala unayoyafanya ya msingi,

malengo uliyonayo mengi,

mamba wanaokutamani wengi,

kivipi utafika ngambo?

 

Daraja upitalo ni la kamba,

sio lipana ni nilembamba,

upitapo usiwe unajigamba,

ukiiga unapasuka msamba,

kivipi utafika ng'ambo?

 

Waliovuka walishasema,

vyema ukifanya yaliyokutuma,

usijaribu kufanya kwa kupima,

ukichanganya malengo na mtima.

Kivipi utafika ng'ambo?

 

Wakasema usajaribu ndumba,

kuuvuka kudra za muumba,

wala usichoke kumuomba,

Ndiye atakayekuvusha viumba, 

Vya Mto huu wenye mamba.

 

Kajiabeid(c)2011

by Abeid Kajia on Friday, February 4, 2011 at 3:07pm ·


No comments:

Post a Comment