Thursday, November 24, 2011

RATIBA YA SHEREHE YA MAHAFALI YA THELATHINI NA SABA (37) YA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA TAREHE 25 NOVEMBA 2011

              Graduation Ceremony  

 Source www.ifm.ac.tz. 24th Nov. 2011

MUDA
TUKIO
MHUSIKA
Saa 3.00 Asubuhi
Mazoezi (Rehesarsals)
Wahitimu/Msherehe Mkuu (MC) /Wakuu wa Vitivo na Idara/ Kamati ya Mahafali
Saa 8.15 Mchana
Wahitimu kuchukua nafasi zao
Msherehe Mkuu /Kamati ya Mahafali

Saa 8.30 Mchana
Wageni waalikwa wawe wamekaa
Msherehe Mkuu /Kamati ya Mahafali

Saa 8.35 Mchana
Kuwasili kwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo
Mkuu wa Chuo / Menejimenti
Saa 8.50 Mchana
Milango ya Kuingia Viwanja vya Mahafali kufungwa
Kamati ya Mahafali
Saa 9.00 Alasiri
Kuwasili kwa Mgeni Rasmi, Waziri wa Fedha na Uchumi
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo /Mkuu wa Chuo/ Menejimenti.

Saa 9.05 Alasiri
Msafara wa mgeni rasmi kuelekea viwanja vya mahafali
Mgeni Rasmi/ Mwenyekiti wa Baraza la Chuo/ Mkuu wa Chuo/ Menejimenti/ Brass Band
Saa 9.15 Alasiri
Kuundwa rasmi kwa Mahafali
Mgeni Rasmi
Saa 9.20 Alasiri
Salamu za makaribisho na kumkaribisha Mwenyekiti wa Baraza la Chuo kutoa hotuba
Mkuu wa Chuo
Saa 9.25 Alasiri
Hotuba ya Mwenyekiti wa Baraza la Chuo
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo
Saa 9.40 Alasirii
Hotuba ya Mgeni Rasmi
Naibu Waziri wa Fedha

Saa 10.00 Jioni
Kutoa zawadi kwa waliofanya vizuri
Mgeni Rasmi
Saa 10.20 Jioni
Kutunuku Vyeti
Mgeni Rasmi

Saa 11.00 Jioni
Kuvunjwa rasmi kwa Mahafali ya 37
Mgeni rasmi

Saa 11.15 Jioni
Mwisho wa Sherehe
Msherehe Mkuu



Sunday, November 13, 2011

Je wewe unaonaje?


kwa mfano ninaposema KUMKICHWA NI wewe, sijui kuwa huwa naelewekanaje!
ninavyojua  maisha yetu yameegemea katika HARAKATI  ZA kutafuta kidogo kitu,
kwa zama za zamani za MAPINDUZI YA viwanda ambazo zimeshapita,
kwa sasa tumeshaweza KUJIKOMBOA kwa zama za habari au za mfumo wa digital.
sasa ili tuweze kuwa huru KIFIKRA NA pia kuondoa ugumu wa maisha,
Hembu jitazame kimaisha na KIJAMII. kwa jicho la tatu,
na kwa namna tofauti kwa upeo wako wewe.
Kisha ukipata JIBU tuilia nalo.


Sio vibaya kwa mwandishi kuanza kwa kuwauliza wasomaji wake swali na sio vibaya pia mwisho wa makala zake mwandishi huyo kuwapa jibu. Hi ni kawaida kwani panapo swali huwa pana jibu lake. Je wewe unaonaje?. Katika mfululizo wa mashairi, makala na picha nilizozitoa ziko kwenye mfumo wa kuuliza kisha kuchambua kwa vipengele mbalimbali husika na kichwa cha habari ama lengo husika la kilichohusika, iwe ni makala, ushairi ama picha. Ukizitazama kwa makini basi utakua umeona uhusika wa ninayoyasema. Ila swali limenijia je wewe huwa unazionaje? Je unaona zaidi ya niliyoyaona ama nilivyochambua? Je kwa upande wako unaona sivyo ama ndivyo? Je? Je? Je?. Yote haya ni maswali ambayo wewe kama msomaji unatakiwa uyatambue kwa uhalisia wako kisha ujiulize na kupata majibu ambayo yanatokana na uhusika wako katika dunia hii.

Tumeumbwa katika upekee ambao unamfanya kila kiumbe kiwe na muono wake tofauti na wengine. Ila pale panapokua na uhusika halisi na asilia wa kitu basi wote tupate jibu moja, iwe ni ndio au hapana, ama iwe ukweli au uongo. Inategemea na wewe umeonaje.

Ninaposema umeonaje namaanisha, baada ya kukiona kitu ama jambo kisha ukalichambua kwa makini kutokana na namna ulivyokua/ulivyokuzwa kwenye mazingira yako, watu uliokutana nao katika ukuaji wako, vitu/mambo uliyojifunza, tabia zako, malengo yako, umuhimu wake katika maisha yako, unakipenda/haukipendi, unakitambua/haukitambui, hasira, chuki, wivu, uwezo wako ama mapungufu yako. Vyote hivi vinahusika katika kuona na kujua kua unakionaje ama unakichukulia vipi.

Kuna upekee katika vitu, kuna mafunzo, kuna kuweza na kushindwa. Ukiamua kuona utaona, ila je unakionaje? Zaidi ya unavyokiona ama haina haja ya kuona zaidi. Ulichokiona kwa mtu ama kitu ni zaidi ya ulichokiona. Mfano hii ni kalamu. Je kwa matumizi yake unaweza ukaona kua utakitumia kwenye nini?. Kalamu sio kuandika tu, kalamu inaweza ikawa silaha tena hatari sana, ila inategemea umeionaje na umeamua kuitumiaje? Jiulize matumizi zaidi ya kalamu.

Tazama kisu matumizi yake ni kukatia vitu. Lakini kisu kinamatumizi mengi. Mazuri na mabaya. Yenye manufaa na kwa yasiyo na manufaaa. Wewe umekionaje? Je unaweza kukitumia zaidi ya matumizi yake husika. Mfano unataka kufunga screw ila hauna screw driver, kama una kisu unaweza kutumia. Ila matumizi ya kisu sio kufungia screw. Inategemea na mafunzo na mahitaji yako. Je wewe unakionaje? Lengo la makala hii ni matumizi yetu kwenye vitu ama watu katika maisha yetu. Je tunavitumiaje, je tunavichukuliaje? Je tuna vionaje? Namna tunavyoviona na namna tunavyovikuchulia ndio vinapounda matumizi yake na matokeo yake yanatokana na maswali hayo.

            Katika dunia ya sasa ya Zama za Habari “Information Age/Information Revolution /Computer Age/Digital Age” ambapo zimefanya mabadiliko makubwa na kuifanya Zama ya Viwanda kupotea kabisa kwenye ramani. Zama hii mpya ya habari inahusisha sana matumizi ya mtandao katika kurahisisha njia za awali zilizotumika katika zama za viwanda.  Utakubaliana nami kwamba zama za sasa zimefanya mawasiliano kuwa marahisi sana kuliko kipindi cha nyuma. Ukitaka  kufanya biashara, kusoma, kutoa habari ama kupata habari yoyote sasa hivi basi wewe tumia mtandao na utazipata kwa haraka sana. Hii ni kutokana na mfumo mpya wa digital. Ila sasa isiwe tija sisi kuwa katika mfumo huu mpya. Swali langu liko pale pale wewe unaonaje nikimaaniasha wewe unautumiaje huu mfumo mpya wa maisha katika kurahisisha shughuli zako za kila siku na katika kijiletea maendeleo yako, familia yako, jamii yako, taifa lako na duniani kwa ujumla. 

             Hembu tazama mifano ya watu hawa na kwa kutumia mtandao wa jamii wa FACEBOOK. 

MSANII: - Kama kuna msanii yuko kwenye mtandao wa facebook, msanii huyu ataona facebook kama sehemu ya kutangazia jina lake, kutolea nyimbo zake, kuwajulisha mashabiki wake nini kinaendelea juu yake, pia kujua idadi ya mashabiki wake. Anaweza pia kuitumia kama sehemu ya kuwavuta mapromota ili waweze kumpa dili la kufanya kazi nae. Pia kwakua msanii huyu ni kioo cha jamii basi sehemu hii msanii anatakiwa aiheshimu kwani matumizi ya kioo ni kutazama, sasa kama huyu msanii atachafua kioo hiki basi asilaumu mashabiki wake watakapo mkimbia.

MFANYABIASHARA: kama kuna wafanyabiashara katika mtandao wa facebook basi hawa watakua wanaiona kama sehemu muhimu ya kuwafikia wateja wao kwa kutangaza biashara zao na pia kupata maoni namna ya kuboresha huduma na bidhaa zao. Pia ukiwa na idadi kubwa ya watu waliojuinga katika ukurasa wako kama wateja pia inamfanya mfanyabiashara huyu kujua bidhaa yetu imesambaa mpaka wapi na wapi tunatakiwa tuifikishe.  Hii inategemea na mfanyabiashara huyu ameuonaje mtandao huu.

MWANASIASA: - kwa wanaojihusisha na siasa wanaweza kuhamisha jukwaa lao kuwa kurasa kwa kueleza sera zao kupitia mtandao. Hii inatokana na kuwa mtandao huu unakua kwa kwasi kuliko soko lingine kwa dunia ya sasa. Anaweza kupata pia habari za nini kifanyike kwa wanachama wake, pia aweza kuona mtandao huu kama sehemu ya kujua idadi ya wanachama wake.

Ila kuna hili kundi la vijana wa kike na kiume, kundi hili limekua na tabia nyingi tofauti kutegemea na matumizi ya mitandao hii ya jamii. Kundi hili mara nyingi liko katika mafunzo ili waweze kupata upeo wa kuweza kukabiliana na maisha yao wakati wao utakapofika. Lakini kundi hili nadhani wanashindwa kutofautisha matumizi ya kisu na kalamu. Wanatumia kisu kuandikia na kalamu kukatia. Kundi hili litakuja kuamka wakati jua linazama au litakumbuka shuka wakati jua ndio linachomoza. Nimejaribu sana kutafuta njia ya kuliongoza kundi hili katika kuona utofauti wa mambo na kuona vitu tofauti na vinavyoonekana ila inavyoonekana kwamba inaweza ikapelekea kamvunja samaki huyu anayejilazimisha kukauka kwa kujaribu kwangu kutaka kumkunja angali mbichi na mbishi. 

Hivyo kwa kutumia maandishi haya, najaribu tena kuwapa mwongozo wa namna ya kutazama kitu ama jambo tofauti na linavyooneka ama linavyosemwa. Kwa mfano ninaposema kumkichwa ni wewe, sijui kuwa huwa unanielewaje? Au unaona kuwa kumkichwa  ni kumkichwa tu kama ilivyo kumkichwa. La sio hivyo, hembu itazame kumkichwa kwa namna tofauti kwa upeo wako wewe. Kisha ukipata jibu tuilia nalo. Dunia ya sasa imekua ya mapinduzi ya mtandao kwa mtandao. Unajua kua mtandao wa YOUTUBE unaweza ukafanya Tanzania ya leo ikabadilika sana tofauti na unavyoiona. Tazama kwa makini matumizi yako ya simu ya mkononi ni zaidi ya kupiga picha na kusikiliza muziki, hembu zama zaidi unaweza ukapata jibu la swali langu kuwa je wewe unaonaje, kwa matumizi ya vitu na watu unaowaona. Kumkichwa ni wewe!

Saturday, November 5, 2011

Naandika





"Kalamu ni bora kuliko upanga" haya sio maneno yangu bali ni nukuu ya wahenga, ikimaanisha ukichagua kalamu ama elimu wewe ni bora kuliko aliyechagua upanga. Maswali yataibuka kwanini una andika? Sababu moja kubwa ndio iliyonifanya/inanifanya niandike. UPENDO WA DHATI. Sijui kwanini napenda kuandika ila huwa najikuta naandika makala mbalimbali na huwa najikuta ni mwenye furaha pale ninaposoma makala zangu au makala iliyoandaliwa na mtu yoyote, awe ni rafiki au mtu yoyote yule.

Kuna maandiko yanayotoka kichwani na yanayotoka moyoni. Maandiko yote haya yana umuhimu sana. Kwa maandiko yanayotoka moyoni mwa mwandishi haya huingia moyoni mwa msomaji, na kwa maandiko yanayotoka kichwani nayo pia huingia kichwani kwa msomaji. Kwa maandiko yanayotoka mdomoni mwa mwandishi bila kuchanganywa na hisia ama akili za mwandishi, haya huishia machoni ama masikioni mwa msomaji au msikilizaji. Hivyo sababu kubwa ya kuandika ni hisia toka moyoni zikichanganyika na akili za kichwani zinazonisaidia kupanga mfuatano visa na maneno yatakayotumika ili wasomaji waweze kunielewa na hata kupata hisia ya nilichokiandika.

Kwa maisha yalivyo kuna vitu vingi sana vya kuandika ili kuwajuza wasomaji, na pia kutumia ulichonacho ama unachokifahamu. Unaeza kuwa na makala hata mia moja zinazongumzia kitu kimoja lakini katika nyanja mbalimbali. Unaweza ukawa una sauti kubwa kusikika ila sauti yako ikashindwa kuwafikia walengwa. Unapoongea waliokuwepe ndio watakao kusikia ila hawatafikisha ujumbe wako kama ulivyo, wapo watakao ongeza na watakao punguza baadhi ya maneno ambapo hupelekea kupoteza utamu na uhalisia wa ujumbe wako. Lakini unapoandika, kwanza ujumbe halisi humfikia mlengwa, pia maandiko haya yatakaa na kudumu muda mrefu katika kumbukumbu.

Kwa sababu napenda kusoma zaidi ya ninavyofundishwa. Maisha ni kujifunza na katika kujifunza kuna baadhi ya vitu huwa tunavigundua katika maandishi ya waandishi. Mwandishi mzuri ni yule anayetumia muda wake kusoma maandishi ya waandishi wengine. Hauwezi kwenda benki ukatoa fedha ambazo haujaziweka,na hauwezi kutoa kiasi kikubwa zaidi ya ulichokiweka. Basi utakubaliana nami kuwa huwa tunatoa tulivyoweka.

Siridhishwi na mwenendo wa mambo unavyoenda, hivyo pale ninapoandika kuhusu jambo ambalo haliniridhi huwa najisikia huru kwani nimeongea na fikra zangu na moyo wangu kwa maandishi. Ukiangalia makala zangu nyingi nimendika kuhusu matatizo ya jamii zetu. Hasa pale mambo yanapokwenda kombo. Hivyo pale matatizo yatakapokwisha ndipo nitaacha kuandika na matatizo huisha pale binadamu anapo ondoka katika dunia hii.

Napenda kuwashauri marafiki, ndugu, wanafunzi wenzangu, walimu, wakubwa zangu hata na wadogo zangu. Andikeni, andika kitu chochote kile, utapata amani ya moyo nafsi na akili. Andika chochote unachodhani kina umuhimu na heshima mbele yako kabla hakijafika mbele za wasomaji. Andika kuhusu maisha yako katika nyanja zote.Tambua katika kila kiumbe kuna somo la kujifunza kwa aliyojifunza au kwa alivyoishi. Anza wewe kwa kutambua ya kuwa  KUMKiCHWA NI WEWE! 

Friday, November 4, 2011

The 37th GRADUATION CEREMONY OF THE IFM



The 37th Graduation ceremony of the Institute of Finance Management (IFM) will be held on Friday, November 25, 2011. At 1400 hours at the Karimjee Hall. The Minister for Finance and Economic Affairs Hon Mustafa Mkullo will be the Guest of Honour.
Those who wish to participate in the aforesaid ceremony are requested to observe the following:

1.       Inform the Rector in writing of their intent to participate in the ceremony before 10th November 2011. Only those who will confirm their participation in the graduation ceremony will be considered   for hiring graduation gowns.
2.       Graduands  who wish to hire graduation gowns will sign an agreement and pay TZS 50,000/= to the Finance officer or use the clearance form available at the Department of Student records to commit themselves that the fees should be deducted from their caution money.
3.       The cost of hiring the gown is TZS 45,000/= and TZS 5,000/= as deposit. The deposit will be refunded when the gown is returned.
4.       Graduation gowns must be returned within seven days after the graduation ceremony. Failure to return the graduation gown on time will result in a penalty of TZS 10,000/= per day for all additional days. All Graduation gowns will be issued at the IFM Council Chamber as follow

·         Faculty of Accounting, Banking and Finance (FABF) – 11th -15th November 2011 from 1500-1800 hours.
·         Faculty of Economics and Management Sciences (FEMS) -16th and 17th November 2011 from 1500-1800 hours.
·         Faculty of Insurance and Social Protection (FISP)- 18th and 21st November 2011 from 1500-1800 hours
·         Faculty of Computing, Information Technology and Mathematics (FCIM)- 22nd and 23rd November 2011 form 1500-1800 hours.
5.       There will be a rehearsal at Karimjee Hall on 24th November 2011 from 0900-1200 hours. Those who will not show up for rehearsal will be barred from attending the graduation ceremony and will graduate I absentia.
6.       Upcountry graduands are expected to make their own travel and accommodation arrangements.
For more information contact:
The Dean of Students
IFM Block D Room 006,
Tel +255 0222112931-4 ext  239/423                        
Fax +255 022 2112935
Source: The Guardian, Friday 4 November 2011

Wednesday, November 2, 2011

"Usijaribu kubisha! Jaribu kuelewa"

MEDITATION



          Katika tafakuri zetu za kina za kila siku kuna ukweli ambao miongoni mwetu tunatakiwa tuukubali kama ulivyo. Ingawa miongoni mwetu huwa tunapingana nazo kwa kutaka ziende vile nafsi zetu zinavyotaka, na kwa tafakuri hiyo tunajikuta tunapingana na ukweli ulivyo kwakua tuna katabia kanachoitwa ubishi wa kubishia nafsi zetu palipo na ukweli. Sasa hembu tujaribu kutazama palipo na ukweli na kisha tuukubali kwa kuuelewa ukweli huo ili tufanye maisha yetu yawe marahisi, kwani kwa namna tunavyokataa ukweli wa tafakuri za kina ndipo tunapoyafanya maisha yetu ya kila siku kuwa magumu na yenye matatizo tunayo yatengeneza sisi wenyewe na kisha kuyatupa kama lawama kwa wao, yeye ama wewe, kunapopelekea kuunda tatizo lingine. Hembu tafakari kwa kina kuhusu haya niyasemayo kisha ujaribu kuelewa. Kwakua wewe ni binadamu kama mimi najua utabisha kwani binadamu tumeumbwa na hulka zifuatazo.

                Kusahau:- ni hali inayomtokea mwanadamu na kumfanya asiwe na ufamu wa jambo kila wakati, kupoteza picha halisi ya tukio ama jambo fulani, hii inatokana na kuwa binadamu hupitiwa na mawazo mengine ambayo humfanya binadamu asiwe na kumbukumbu ya jambo fulani kila mara. Kiwango cha kusahau huwa kinatofautina baina ya mtu na mtu kutokana na umuhimu wa jambo ama hicho kitu kwa mtu huyo. Kusahau kunaendana na kukumbuka, huwezi kuzungumzia kusahau ukaacha kulitamka neno kukumbuka. Ni vitu viwili vinavyotegemeana sana. Sasa kwanini tunasahau na kwanini hatukumbuki. Tuuchukulie mfano wa KIFO ambao ni kitu kichungu na kinachompa mwanadamu wasiwasi na uoga juu ya maisha yake. Ukimwambia mtu kinyume cha kusahau atakuambia kukumbuka tena kwa furaha, lakini ukimwambia kinyume cha kuwa hai atajibu kifo huku nusu ya furaha yake ikiwa imepungua. Tujaribu kuelewa kuhusu kukumbuka na kusahau pia kuwa hai/kuishi na kufa ama kifo. Huwa tunafiwa na wale tuwapendao lakini pia huwa tunawakumbuka sana kwa kua walikua wana umuhimu katika maisha yetu ya kila siku. Lakini kuwakumbuka kwetu sio kama ilivyokua siku waliotutoka. Kifo hakisahauliki ila huwa kikiwa ni kwako wewe huwa unakisahau. Kwakua tafakuri hii inakusuhu wewe basi utakubaliana nami kua huwa tunajisahau kuwa ipo siku tutaondoka katika dunia hii. Na hii ni hulka ya mwanadamu aliyopewa na muumba wake ili asisononeke sana pale anapo fiwa ama anapokumbuka kuwa kuna siku nitakufa. Hembu tujiulize ni tabu gani tungeipata kama tungekua na hulka ya kujua kua kesho ndo siku yangu ya kufa. Jaribu kuelewa na usikariri. Kusahu kupo na kuna umuhimu wake katika maisha yetu ya kila siku. Ila kumbuka kumuomba muumba wako ili siku hiyo ikifika uvune vinono ulivyovipanda ingawa najua kuwa utasahau..

                 Kutoridhika:- ni hali ya kutokutosheka na ulichonacho ama ulichokipata wakati unatafuta. Binadamu ana hulka ya kutokuridhika na hii inatofautiana baina ya mtu na mtu. Kuna wengine watasema huwa naridhika ila hata upewe kila kitu bado utataka kitu kwakua haturidhiki. Kuna hulka ya kutafuta zaidi ya ulichokipata kwakua ni hulka yetu kutokuridhika. Masikini haridhiki anapopata riziki, tajiri nae haridhiki kwakua nae anataka riziki zaidi ya aliyoipata. Yote hii inatokana na kusahau na kutokuridhika. Katika tafakuri za kina ukilitazama tumbo namna mwenyezi mungu alivyoliumba hata ulipe nini haliridhiki ila huwa tunaridhisha kwa kutoa shukrani kwa tulochokipa. Ila baada ya muda huwa tunalipa tena yoyote riziki ilituweze kutafuta kingine kwakua haturidhiki. Kwakua haturidhiki basi tunatakiwa tutoe shukurani kwa tulichokipata. Ili tutafute kingine chenye Baraka kutoka kwa muumba wetu. Tukumbuke kutoa shukurani kwa tulichopata kwakua kina ubora kuliko tulichokikosa. Hivyo jaribu kuelewa na wala usibishe ingawa najua kuwa pia utasahu kwakua haturidhiki.

                 Kutafuta:- ni hali ya kutaka kupata kile unachotaka na unachodhani kuwa kina umuhimu katika maisha yako ya kila siku. Katika kutafuta kuna kupata na kukosa, na katika kupata kuna kushukuru ama kukufuru, halikadhalika unapokosa unatakiwa ushukuru na sio kukufuru. Binadamu huwa anatafuta kisha anapumzika, kisha anaanza tena kutafuta. Kwakua tuna hulka ya kusahau na kutokuridhika, basi yatupasa kutafuta kwa moyo mmoja na kwa hali na mali. Hali ikisimama kwa maana ya uwezo wako wa nafsi na mali kwa uwezo wa vitu vinavyokuzunguka. Lakini ili kuweza kufanikisha haya katika kutafuta binadamu huwa anajisahau kuwa hata akipata anachokitafuta kuwa hataridhika. Hivyo binadamu huyu anaishia akitafuta anachokijua na asichokijua. Jaribu kuelewa na wala usibishe kwani usiposahau utaridhika na ukiridhika hautatafuta. Muombe muumba wako akuongoze katika kutafuta.

                 Matatizo:- ni hali ya kutokua na utulivu wa nafsi, moyo na akili. Ni sehemu ya maisha yetu kwakua tunajisahu, haturidhiki na hatuchoki kutafuta. Huwa tunafikiria kuwa matatizo ndio yanamkuta mwanadamu, sio kweli kwakua kunachokukuta basi kitakuacha, lakini ukifanya tafakuri ya kina utagundua kuwa banadamu ndio anayoyakuta kisha anayaacha. Tatizo sio matatizo ila tazizo ni binadamu. Binadamu na vitu vilivyopo katika dunia hii ndio matatizo au ndio tatizo. Matatizo hayajitengenezi ila sisi ndio tunayatengeneza matatizo. Hivi unajua kuwa kiumbe kilichokufa ama ambacho bado hakijazaliwa hakina matatizo. Basi elewa kuwa sisi ndio matatizo. Kwaku tunasahau, haturidhiki na tunatafuta kwa hali na mali. Hivyo kutokukamilika kwetu ndio kunakotuletea matatizo na ili kuweza kufanikisha haya yote yakubidi kuelewa na sio kukariri kwani maisha ni marahisi ili sisi ndio wazito katika kuyaelewa.

                Uchungu:- ni hali inayoleta maumivu katika kitu ama mtu, uchungu unaumiza na hasa kitu ama mtu mwenye uhai ndiye anayepata uchungu huu. Kwenye Agano La Kale imendikwa “mwanaume atatafuta kwa uchungu ana mwanamke atazaa kwa uchungu”. Je ni uongo ulioandikwa kwenye vitabu hiki? Sidhani, kama ukibisha au unataka kubisha, fanya tafakuri ya kina na kisha utazame hali halisi ya maisha yetu ilivyo ndipo ubishe kua huu ni uongo. Ni kweli kwamba atakayeamua kutafua atatafuta kwa uchungu na atakayeamua kuzaa atazaa kwa uchungu. “Penye uchungu pana utamu na penye utamu pana uchungu” jaribu kuelewa na usikariri kisha ukabishana na ukweli wa tafakuri za kina. Inaleta uchungu pale mtu anaposahau jambo lenye umuhimu na pia inaleta furaha pale mtu anaposahau jambo lenye uchungu. Tafuta kwa uchungu, ukipata najua pia hautaridhika ila endelea kutafuta tena kwa uchungu.

                 Kufanikisha:- ni hali ya kupata kile ulichokua unakitaka/unakitafuta, kiwe ni kidogo ama ni kukubwa, ukikabiliana nacho ukakishinda basi ujue umefanikisha, ama kinachokutatiza katika kupata amani ya nafsi, moyo na akili kisha ukaweza kuondoa ukinzani huo basi umefaniakisha. Kwa mfano ikihisi njaa unakosa amani ya nafsi na akili, lakini ukishatatua tatizo hilo basi umefanikisha, lakini chakula utakipata wapi ili utatue tatizo hilo, nao pia ni ukinzani, ukitatua nalo umefanikisha. Hivyo matatizo ni ukinzani kwa mwanadamu, mwanadamu hapendi alichonacho anapenda asichonacho, lakini akikipata asichonacho hakitaki tena, binadamu huyu anajisahau, banadamu huyu haridhiki, banadamu huyu anatafuta, binadamu huyu anapata uchungu, binadamu huyu anafanikisha. Lakini hajui kua amefanikisha kwakua anasahau, haridhiki, anatafuta, anauchungu anataka kufanikisha kila kitu. Jaribu kushukuru pale unapofanikisha hata kitu kidogo usijisahau sana eti kwakua hauridhiki na kwakua unatafuta kwa uchungu mpaka ufanikishe.

                     Hivyo nataka ukubaliane nami kua sisi binadamu hatujakamilika, ingawa kulirudia neno banadamu hatujakamilika ni kuonesha ni namna gani sisi binadamu hatujakamilika kwakua tumeshakubali kua hatujakamilika. Tunasahau, haturidhiki, tunatafuta kwa kushindana kuukimbiza upepo ama kukimbizana na upepo, tuna uchungu ambao hatuwezi kuuondoa bali tunaushahau kwakua hatujakamilika, tunafanikisha ingawa sio vyote tunavyovifanikisha kwakua huwa tunasahau kutoa shukurani tunapofanikiwa ama tunaposhindwa kufanikisha. Kwa hiyo tunapofanya tafakuri ya kina (meditation) yatupasa tukubaliane na ukweli, pale tunapopata tafakari ya kina yenye ukweli basi tuikubali kama ilivyo, wala tusijaribu kuipinda ikawa ni uongo, kwani “kuna ukweli ambao hauwezi kuwa uongo na uongo ambao hauwezi kuwa ukweli”. Ukikubaliana nami kuhusu haya basi utakuwa miongoni mwa watu wanoishi maisha marahisi yenye furaha kwakua wanajaribu kuelewa na sio kukariri na kubishana na ukweli wa nafsi zao. Ni rahisi kumbishia binadamu mwenzako na ukamshinda ila ukibishana na nafsi yako utashindwa. Tuzidi kumuomba muumba/mola/mwenyezi mungu atusamehe makosa yetu wakati kabla ya kuanza tafakuri na wakati tunamaliza tafakuri zetu kwani hapo ndipo tunapogundua mabaya na mazuri tuliyoyafanya. Tubu na utasemehewa. Kumkichwa ni wewe!