Friday, December 7, 2012

Breaking News kutoka kwa Ordinally Almando



 
Lunch, mchana wa leo, niko na mwanangu Niga C, ni pacha wangu tunapendana sana, vilevile, nafurahi kuwajulisha mashabiki wetu kwamba yule mchizi wetu tuliyekuwa naye kwenye kundi mwenye ndevu kama osama tumeamua kumfukuza kazi katika kundi kwa sababu zifuatazao:-

 1. Anatuchafulia Jambo Squad kwa tabia ya kuendekeza wizi, nikiwa na maana kwamba kama umeshawahi kuibiwa simu/laptop katika club/pub zifuatazo ujue ni yeye na kundi lake la vibaka, wakiwa wamevalia kama mabishoo kumbe ni wezi tu!
AQ, Masai Camp, Empire, Babylon, Pinpoint; na pia ni dalali mzuri wa vitu vya wizi.
Yeye ndiye aliniibia baiskeli yangu, pia blackbery ya Niga C na nashangaa wanapomwingiza mama mzazi wa Niga C kwenye mambo ambayo hayamhusu; kama ni kumdis yeye wamdis Niga tu , mama wa nini?

 Haitoshi, anamtumia Niga watu wampige, pia wanawadanganya djs na watangazaji kwamba Niga kawatukana kumbe ni uzushi tu, chalii yangu yuko peace tu!...
Kinachouma zaidi, kwa kuwa waliijua password yangu ya fb wameandika status kama vile ni mimi, nikimdis Niga kumbe si mimi.

 Kutokana na ukweli pia kwamba yuko chini ya kiwango katika kurap, tumeamua kumweka kando, kwani hatuwezani na wezi na wanaotegemea kubebwa kiutendaji. Kama yeye ni mkali, AFANYE KAZI YAKE, aache blah blah Ordinally, na Niga C kama mapacha, FOR LIFE! MUZIKI KAZI, WIZI WA NINI?
JAMBO SQUAD FOREVER, EE MUNGU TUSAIDIE! kutoka kwa Ordinally John

 

No comments:

Post a Comment