IMENZISHWA: 2000
INAHUSIKA NA: KUTENGENEZA MUZIKI KWA AUDIO NA VIDEO (SHOOTING& EDITING), KUPIGA PICHA ZA MNATO (STILL PHOTOGRAPHY), GRAPHICS DESIGNING, LOGO DESIGNING, BROCHURES, PROMO CD’S, BUSINESS CARDS, T-SHIRTS NA LABELS.
AINA YA MUZIKI: Bolingo, Reggae, R n B HiP HoP
ENEO ILIPO: NGARENARO ARUSHA
NCHI:Tanzania
Grandmaster Records ni studio iliyoanzishwa mnamo mwaka 1999, lakini ilianza rasmi shughuli za muziki mwaka 2000, ilianzishwa na wanafamilia watatu watoto wa Mzee Blass Mallya ambao ni
John Blass Grand (John B) ,Dennis Mallya na Alphonce Blass Mallya. Wazo la kuanzisha studio hii lilitokana na kwamba vijana wengi walipenda kwenda nyumbani kwa Mzee Mallya kukaa na kuimba nyimbo zao kwakutumia ala zilizokua kwenye kinanda, kundi la Terrible Clan lilikua la kwanza, na walianza kuimba kwa kutumia kipaza sauti cha redio kwa beat ya ala zilizokua kwenye kinanda hicho. Ilikua ni mwishoni mwa mwaka 1999 ambapo Dennis na Alphonce waliposafiri kwenda nchini Botswana na kukutana na rafiki wa familia aliyefahamika kwa jina la Solo, ambaye alikua mtayarishaji wa muziki nchini humo. Solo aliwapa wazo la kufanya muziki na aliwapa mfumo wa ndani wa kinakilishi, ambayo waliitumia katika kutengenezea mapigo ya muziki (beat). Wazo lingine la kufanya muziki, walilipata kwa binamu yao
Joachim 'Master-j' Kimaryo mmiliki wa studio ya Mj Production, bila kumsahau motisha waliyoipata toka kwa Deo Mhumbira aliyekua amesomea masuala muziki na pia ni mwimbaji wa nyimbo za kwaya (Gospel).
|
John Blass akiwa studio za GM mwaka 2000 |
Mwaka 2000 ndipo walipoanzasha rasmi studio ya Grandmaster, wakichagua jina la mwanamuziki wa kimarekani Grandmaster Flash (Joseph Sadler), ambaye John B anasema GrandMaster Flash aliwavutia mioyoni katika kujishughulisha na muziki. Walianza na Kompyuta moja ya Pentium 1 na kipaza sauti kimoja cha redio na kinanda kimoja. Chumba walichokichagua kuwa studio kilikua ni chumba cha kufanyia mazoezi (Gym) iliyokua nyumbani kwao. Nyimbo ya kwanza kutengenezwa ilikua inaitwa “Nani anayetaka kupambana” ya dakika sita (6) ya wasanii kumi na mbili wa kundi la Terrible Clan, beat ilitengenezewa Grandmaster na kisha kuchanganywa nyumbani kwa
Gsan Rutta wa
X Plastaz. Nyimbo nyingine zilizofuata ni “Nipe Tano” ya msanii wa Hip Hop
Umbwa Lotuno (Chindo Man), ambapo kwenye mashairi yake ya wimbo wa “
Nimesota Sana-Chindo ft JCB by Grandmaster Productions" (2010) anasema “mwaka 2000 mi ndo MC wa kwanza kurekodi Grandmaster ‘nipe tano’, kipindi hicho naimba toung twister fasta”.
Mwaka 2001 ndipo ulitengenezwa wimbo wa kwanza wa
Aptii Mohamed Ismail ulioitwa “Life Story”, na mwaka 2002 Aptii na Snaff walifanya wimbo mwingine ulioitwa “Jimama” na pia msanii Rama B alifanya wimbo wake ambao ulitamba katika vituo mbalimbali nchini, wimbo huo uliitwa “Mtarajiwa” . Chindo Man naye alifanya tena wimbo mwingine wa “Weekend”.
Mwaka 2003 ulitengenezwa wimbo wa Babu Ally “Ni Moto”.Mwaka huo wa ndipo mafanikio pia yalianza kuonekana kwani wimbo wa msanii CK “Picha halisi” ulifanikiwa kuchaguliwa kati ya nyimbo tatu bora zilizoshinda TUZO ZA KILIMANJARO kwa mkoa wa Arusha. Miongoni mwa nyimbo za kwanza kabisa kuonesha mafanikio Grandmaster ni pamoja na wimbo wa CK ulioitwa “Anasakwa na Polisi”. Ushindi wa CK katika tuzo hizo za KLM kuliwapa moyo, kwani kulikua na ushindani mkali sana katika tuzo hizo. CK ni msanii pekee kutoka lebo yao aliyefika mpaka nafasi ya mwisho. Kwani makundi mengie mawili yaliyokuwa chini ya lebo yao yaliyoingia katika kumi bora katika mashindano hayo yalitolewa na CK ndiye aliyepita katika tano bora pamoja na wakali Mandojo na Domokaya, lakini mpaka nafasi za tatu za mwisho ni CK alikuwemo.
|
John B(katikati) akiwa na CK mwenye brown leather Jacket, wa pili kushoto |
Mwaka 2004, vijana wa kundi la Black Unit walitengenezewa wimbo ulioitwa “Nimeadhirika” ambao ulidhaminwa na CHAWAKUA kwa ajili ya kutahadharisha watu kuhusiana na ugonjwa hatari wa UKIMWI. Mwaka huohuo palitokea tamasha kubwa jijini Arusha ambalo lilishirikisha wasanii wengi wa mikoani, ambapo wasanii kutoka kundi hilo Salim (Sally B) na Frank (Son/Sad P) waliokua wanajulikana kwa jina la Space Unit walialikwa ila kutokana na ukweli kwamba nyimbo walizokua nazo zilikuwa ni kwaajili ya uelimishaji rika, iliwabidi waingie studio siku hiyohiyo ya tamasha na kurekodi wimbo wao uliojulikana kwa jina la ‘’Miss Tabasam’’ kisha wakaufanyia mazoezi hapo hapo studio huku maandalizi ya tamasha hilo yakiendelea. ‘’Miongoni mwa vitu ninavyovutiwa navyo kazini ni pamoja na kushiriki katika furaha na mafanikio wanayopata wasanii, mapokezi ya vijana wa Space Unit yalikua mazuri sana, wasanii kama
Sir Juma Nature na wengine walionesha support kubwa sana, ilikua moja ya kumbukumbu muhimu sana kwani pale tuliona kwamba na sisi tunafanya kazi na zinapokelewa na kuheshimika’’ alisema John B. Mafanikio yalijionesha pia katika marudio ya wimbo huo wa “Miss Tabasam” wa kundi hilo la Space Unit. Kundi hili lilifanikiwa kuwa wasanii wa kwanza wa studio hiyo Kushinda Tuzo hizo za KLM kwa wanamuziki wa mikoani kwa mwaka 2004. Ndio pia ukawa wimbo wa kwanza kutengenezewa video mkoani Arusha ukichanganywa na baadhi ya video za onesho walilofanya katika utoaji wa tuzo hizo mwaka 2004. Kundi hilo lilijizolea umaarufu na pia walilitangaza vyema jina la GrandMaster Records. Mwaka huu walifanikiwa kuongeza vifaa vipya kwenye studio kama Computer, Software na kipaza sauti kimoja.
|
Kuanzishwa kwa Video Production |
Mwaka 2007, Dennis Mallya aliyekua akisomea GRAPHICS DESIGNING alikuja na wazo la kuanzisha kitengo cha Video Production. Na ndipo walipoanza kutengeneza video kwa wasanii mbalimbali, ikiwemo shooting ya wimbo wa “Arusha” ya
JCB ft Arusha All Stars na
Charlotte Hill O'Neal (Mama C), Nauza kura yangu ya Bonta, Kila kitu Nyerere – Bonta, Style tatu ya
Stopa Rhymecca Yokoi (Jerome) na nyinginezo.
|
John Blass akiwa studio za Master J (MJ Production) |
Mwaka 2008 John alipewa nafasi ya kwenda kwa binamu yake Master J kutengeneza albamu ya msanii wa kundi ka “WATUKUTU” Joni Woka. Miongoni mwa nyimbo zilizokuwemo katika album hiyo, ni pamoja na “Nikikupata(Nieleze)” ambayo baadaye Dennis alitengeneza video yake maeneo ya Arusha na Dar es Salaam. Wimbo huu ulipata kurushwa na vituo vingi vya redio na runinga, na ulijipatia umaarufu mkubwa na kuzidi kulitambulisha jina la Grandmaster. Pia ilikua ni albam ya kwanza ya John kuitengeneza chini ya studio za Master J na Grandmaster. Album hiyo ilisambazwa na Mamu Stores ambayo ni kipande cha kampuni ya GMC, pia ilishirikisha wasanii wengine wakubwa kama Chelea Man, Bambo, Mtanga, Kingwendu, Wagosi wa Kaya, Keisha na Danny Msimamo.
Mwaka 2009 John anasema ni mwaka uliompa faraja zaidi pale wimbo wa msanii Naba B “Mwanaume wewe” uliposhinda katika tuzo za Kilimanjaro. Anasema siku hiyo alikua anaumwa lakini kwa kua alimuahidi Naba B kwamba atamtengenezea wimbo huo, ilimbidi atengeneze hivyo hivyo akiwa anaumwa mpaka saa tatu usiku. Naba B alipata wakati mgumu kufika na kushiriki lakini alifakiwa kushiriki na kubuka mshindi. John alipokea taarifa za ushindi wa Naba B akiwa Hospitalini. Hivyo ikampa John moyo wakuendelea kufanya shughuli za muziki kwani ilimdihirishia kwamba akiongeza jitihada basi ataweza kufika mbali.
Mwaka 2010 aliendelea kufanya muziki na wasanii wa kundi la “Watukutu”, ambapo John anasema kuwa siku moja walikua mawekaa nje ya studio yeye, Ras Lion na Joni Woka, walikua wakitaniana, katika matani Ras Lion akasema Hii kitu hii, kweli inaleta matatizo’’ Ndipo Woka akamwambia iyo kitu bonge ya idea, John akajua wanafanya utani, kesho yake wakaja na mashairi ya wimbo huo ukaanza kufanyiwa kazi, wakatoa wimbo huo wa “Hii Kitu”, ambao baadae Dennis Mallya aliutengenezea video. Ni moja kati ya nyimbo zilizopata kurushwa hewani na vituo vya runinga na pia kuchezwa katika redio mbalimbali nchini. Wimbo huo ni moja kati ya nyimbo zilizopamba album yao ya pamoja iliyojulikana kwa jina la “Sumu ya panya”.
Mwaka 2011 ni mwaka wetu naweza kusema ingawa bado sijaachia nyimbo nyingi redioni ila kwa mikakati tuliyonayo na nyimbo tulizotengeneza, unaweza ukawa ni mwaka wa mafanikio kwetu sisi na wanamuziki waliofanya muziki katika studio yetu ya GrandMasters. John alisema yeye akishirikiana na matayarishaji mwenzake wa muziki wa
Noizmekah Productions Arusha anayefaamika kwa jina la
Def Xtro, kwa pamoja wanaandaa Project “GrandNoiz” kwa lengo la kuwainua na kuwapa kipaumbele wasanii wa Arusha katika tasnia ya muziki, kwani wanaamini ya kwamba mkoa wa Arusha una wasanii wengi na wenye vipaji ila wamekosa tu mwongozo mzuri.
|
JAMBO SQUARD |
|
Albam Ya Dislimination ya Dcee na Slim |
Wimbo mwingine ni “Life dili”, uliowashirisha wasanii kama
JCB (
watengwa recs),
Stopa Rhymecca Yokoi (Jerome) (Waturutumbi) na Joes (
North Dwellers 144), ambao audio imeshakamilika ila kwa video bado kuna vipande havijamaliziwa. Project nyingine tuliyonayo ni ya wimbo wa “Making History” iliyowashirikisha wasanii kama Roma, Stopper Rhymes, Dojo, Jose Mtambo na , ambao uko kwenye audio. Project ya “Dislimination” ya
Dee Cee - Tanzania Hip Hop Artist na Slim ambayo imeshakamilika, iko sokoni, ambapo ukinunua T-shirt ya “Dislimination” unapata CD yao Bure.
‘’Kazi ni nyingi ila naomba tu fans na wasanii waniwie radhi kwani kuna mengi kwa ajili yao ila muda unabana sana kwasababu ya masuala ya shule’’, alisema John.
|
JOHN BLA$$ |
John mabaye kwa sasa ni mwanafunzi wa mwaka wa nne katika chuo kikuu cha Nairobi, akisomea degree ya masuala ya biashara (B.Com), alisema “napenda sana muziki, kwani huwa unanipa furaha pale ninapo shughulika nao” alisema zaidi ya kutengeneza beat yeye anaweza kupiga kinanda, ingawa anatamani kujifunza code za kupiga gitaa. Katika changamoto zinazomkabili John hakusita kuzungumzia ushirikiano baina ya watu, alisema “Hakuna faida ya mimi kushindana na wewe ila kuna faida ya mimi kushirikiana na wewe” Ushirikiano umetutoa mbali na nina mategemeo utatufikisha mbali zaidi kwani unachangia kujifunza mambo mengi na kufungua milango mingi sana kwenye muziki na katika maisha kwa ujumla. Pia alizungumzia chuki kama moja ya kitu kinachorudisha maendeleo nyuma, Kuhusu mgao wa umeme John alisema “Nimeshuhudia kwa macho yangu, na naweza kusema kuwa uhalifu umeongezeka na utazidi kuongezeka Jijini Arusha, hali ya kimaisha imeshuka sana na vijana wengi waliojiajiri kwa kupitia nishati hiyo wanapata wakati mgumu kimaisha”.
|
JOHN BLA$$ |
MAFANIKIO (Runners up in Tanzania kili Music Awards)
2003: CK- Picha Halisi
2004: Space Unit- Miss Tabasam
2005: Contagious
2007: Naba B- Mwanaume wewe
2010: Ras Magere- Sauti ya Rasta
: Warriors from the east- Misingi ya Rasta
Washindi wa Tuzo za Kili kwa mwaka 2004- (Space Unit) na mwaka 2007- (Naba B)
|
Studio za GM kwa sasa |
Baadhi ya Albamu na kazi zilizotengenezwa GrandMaster
1. Nikikupata - Joni Woka
2. Sumu ya Panya/ Hii kitu – Watukutu
3. Maalmando wa Jambo – Jambo Squad
4. Sauti ya rasta – Warriors from the East
5. Trinity – Warriors from the East
6. Ingoje Ahadi – Judicate Mariki
7. Natembea na Yesu – Kristu Mfalme Choir Ngarenaro
8. Respect my Struggles – Tippin South
9. Msifu Mungu – Mr D
10. Cecilia Choir Kondoa
11. Dislimination – Dee Cee and Slim
Nimeitwa na Bwana – Grace Kimathi